Rais ana mamlaka kisheria ya kumfukuza mtumishi wa umma yeyote kwa maslahi ya umma

moma2k

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
1,091
1,405
Sheria ya Utumishi wa umma ya mwaka 2002, na kanuni zake,inampa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania uwezo wa kumfukuza mtumishi wa umma yeyote bila hata kufuata utaratibu.

Kifungu cha 24(1) cha sheria hiyo kinampa mamlaka hayo Raisi.Lugha inayotumika ni "The president may remove any public servant...for the 'Public interest'.Maana yake sababu ikiwa ni kwa masilahi ya umma, Raisi anaweza kumfukuza mtumishi wa umma bila kufuata due process ambayo ipo katka kifungu cha 23 cha sheria hiyo.

Msingi wa kifungu hiki cha 24 ni ibara ya 36 ya katiba ya JMT inayompa raisi mamlaka ya kutengeneza serikali.Ajira zote za utumishi wa umma msingi wake ni uteuzi wa raisi.Raisi ndo mkuu wa serikal(executive arm) kadiri ya ibara ya 33 ya katiba ya JMT.

Serious note:Wanaohoji mamlaka ya raisi kuwatumbua watumishi 900 wenye vyeti feki, wanapiga propaganda kama kawaida yao. Wananchi muwapuuzeni.Raisi amechukua uamuzi huo kikatiba na kisheria ili kulinda masilahi ya umma. Vyeti feki ni kosa la jinai ambalo pia ni lina compromise the public interest.
 
Kwanini asitumie mamlaka hayo hayo kumfukuza kazi Daudi Bashite ambaye ana tuhuma ya kuiba cheti cha kidato cha nne cha Bw. Paul C. Makonda?

Mkuu, hoja yako haijasimama kwa miguu miwili! Unataka kusema kuwa mtu akihukumiwa kwenda jela kwa kosa la wizi anaweza kujitetea kwamba hasitahili hiyo adhabu kwa sababu bado kuna wezi wengine wako huru mitaani?
 
Reactions: e2n
 
Duh yaani watu wanaajiriwa kwa veti feki wakifukuzwa nayo mnalalamika? kudadadeki nyie noma tena wapuuuzi sana.
Ajabu ni hao hao ambao walikuwa wanalalamika kuwa zoezi la uhakiki lilikuwa danganya toto, [HASHTAG]#bongonyosso[/HASHTAG]
 
Hayo maneno kwenye BOLD, hayapingani kweli?

HALAFU HAPO KWENYE VYETI FEKI, Mbona mwanasiasa mmoja anajulikana kuwa anavyo KAACHWA?
 
ni kweli mkuu hatukatai, katiba ya nchi imempa uwezo wa "kimungu" rais wetu.
lakini sheria ikitumika vibaya (hata na rais) inakosa uhalali (legitimacy). inazaa kichanga kinachoitwa chuki.
rais anao uwezo wa kupora mke wa mtu akitaka na hakuna wa kumuuliza. nitapenda ije siku uje uporwe mkeo kwa style hii ili hili somo langu ulielewe vizuri.
anaweza kumkweza mhalifu (yule aliyevamia kituo cha habari) na kumkandamiza mtafuta haki (yule aliyemsaidia kufunga goli la mkono). katiba inampa uwezo huo lakini haimpi uhalali. inamwongezea tu idadi ya wahasimu!
 
Unajenga hoja yako HEWANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…