Rais ajiepushe kutoa hotuba au kauli makanisani kwa afya ya taifa

ATA MIMI NILIKWAZIKA BAKWATA WALIFANYA KIKAO CHA MASHEHE WOTE WA MIKOA TANZANIA CHINI YA MFUTHI MKUU MKUU WALIFANYA KIKAO MAJUZI

LAKINI HAKUNA KIONGOZI WA AWAMU YA TANO ALIYEKUJA ; WOTE WALIGOMA ATA MWAKILISHI .
Aisee....hivi makamu wa rais anaruhusiwa kuwahutubu masheikh
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia zote,yeye akifika kanisani asali na asepe zake matamko ayatoleee kwenye majukwaa huru
 
Wivu wa kitoto unakusumbua.
Raisi ni wa watu wote wenye dini na wasio na dini.Popote anapokuwa awe kanisani,msikitini,njiani,makaburini,au mahekalu ya mabuda akiwa Raisi ana uhuru wa kuongea nao akipewa nafasi.Ni watu wake na lazima awaambie mambo yake.Ndio maana hata njiani wanamsimamisha aongee
We ni zaidi ya kimeo
 
Mleta mada naona kama huna hoja. Lowassa aliposema kuwa huu uwe ni wakati wa mlutheri kupewa nchi, aliyasema maneno hayo akiwa kanisani au sokoni kariakoo?. Je Lowassa angepewa urais angeshindwa vipi kurudi kanisani na kuongea ikiwa alitumia nguvu kubwa kufanya kampeni kwa kupitia uhusiano wake mwema na kanisa?.
Yapo ya msingi yanayofaa kuongelewa, kuliko hizi siasa za bei rahisi.
Kwani Lowassa ndiye rais?
 
Acha uongo hata akina JK na akina Mkapa walikuwa wakiongea wakipewa nafasi waongee lakini wakienda kusali wasipoombwa kuongea walikuwa wakisali na kuondoka zao
Magufuli sehemu anazoongea ni zile ambazo anapewa nafasi kuombwa aongee kama raisi sio kama padri, shehe au mchungaji .haombi nafasi.Yeye ni muumini anasali maara nyingi lakini akifika mahali kwa mara ya kwanza huwa waumini pale alipowatembelea wanakuwa na kiu ya kumsikia raisi wao wanapenda wamsikie Raisi wao aseme chochote.Na haombi nafasi ila akipewa hawadharau anawaambia anayofanya na kuwaomba wamwombee.

Hata akiwa msibani wakimwomba aongee chochote ataongea hata kama kilichompeleka ni msiba.Wasipompa nafasi anasalimia anatimka zake.
Msemaji wa rais
 
Mkuuu kumbuka, "Two wrongs don't make a right". Lowassa alifanya kosa kubwa. Kosa la Lowassa halihalalishi kosa la JPM. Wote wana makosa, hakuna wa kutetewa hapo.
Commander in chief ni mtu mkubwa sana, inawezekana JK aliamua kuwa humble kwa muda wote wa miaka 10. Hiyo haihalalishi kwamba CIF asiwe na mamlaka kamili kwenye nchi anayoiongoza. Rais wa JMT anao uwezo wa kuzungumza popote pale katika muda wowote anaoona inafaa. Katiba inamruhusu kufanya hivyo.
 
Mfalme ni Mfalme sauti yake husikika hata akiwa Pangoni.Tuache Haya ya Kanisani Kaongea au Msikitini.Kilicho na UMUHIMU AMETOA NASAHA IPI HILO NDIYO LA MSINGI.Hata akiwa safarini Njiani huongea na Raia wake Yeye ni Raisi haijalishi na hana Ubaguzi.Jielewe kuishi ndani ya Tanzania hii soma sana Historia ya nchi hii Uliza kwa lile usilolielewa hili limekaaje .Usikimbilie JF Kuandika vitu katika Utamaduni wa Kitanzania Haviko na katu Havitakuwepo.
 
Commander in chief ni mtu mkubwa sana, inawezekana JK aliamua kuwa humble kwa muda wote wa miaka 10. Hiyo haihalalishi kwamba CIF asiwe na mamlaka kamili kwenye nchi anayoiongoza. Rais wa JMT anao uwezo wa kuzungumza popote pale katika muda wowote anaoona inafaa. Katiba inamruhusu kufanya hivyo.
Mkuu kimpumu ya Jana ilikuwa Kali?naona bado imenasa kwenye masharubu
 
Mwishoni wa ibada kabla kufunga ibada huwa kuna nafasi ya kutoa neno kwa mtu yoyote awe mzee wa kanisa,kiongozi au mgeni yoyote kwa hiyo ni haki JPM kutumia nafasi hiyo pia kama muumin mwingine
 
Commander in chief ni mtu mkubwa sana, inawezekana JK aliamua kuwa humble kwa muda wote wa miaka 10. Hiyo haihalalishi kwamba CIF asiwe na mamlaka kamili kwenye nchi anayoiongoza. Rais wa JMT anao uwezo wa kuzungumza popote pale katika muda wowote anaoona inafaa. Katiba inamruhusu kufanya hivyo.
Mkuu ungeweka na hicho kifungu au ibara ya katiba inayomruhusu raisi kusema chochote na mahali popote anapotaka na kwa muda wowote unaoona unafaa. Itasaidia na wengine wasiojua kama mimi. Sio rahisi wote kujua kila kitu, napenda sana kupata kwa wengine kile nisichokijua.
 
Tafuta katiba ya nchi, jifunze somo la uraia pia. Mmeshazoeshwa mbwembwe za jamii ya kidemokrasia, jifunze mambo mapya maishani.
 
Punguza jazba na uongo
Jifunzeni somo la uraia, msiwe wavivu wa kutafuta maarifa. Huwezi kumpangia rais mahali pa kuhutubia na kuongea. Rais sio diwani wala mwenyekiti wa serikali ya mtaa, ni nembo ya nchi. Ndio maana hata anapokuwa kwenye msafara mtu baki haruhusiwi kumpiga picha, tazama picha zote za marais utaona maelezo kwamba zimepigwa na mpiga picha wa Ikulu. Jifunzeni mambo madogo madogo kuliko kubakia mnajifunza mambo ya nchi za mbali ambayo hayana msaada na maisha yenu ya kila siku.
 
Tafuta katiba ya nchi, jifunze somo la uraia pia. Mmeshazoeshwa mbwembwe za jamii ya kidemokrasia, jifunze mambo mapya maishani.
Mambo mapya mkuu unaweza kujifunza kwa watu wengine wala sio mbwembwe. Sio kila kitu lazima usome mwenyewe. Hata somo la uraia ni watu wanaandaa na kufundisha wengine! Unaona tabu gani kutaja wapi katiba inampa raisi hayo mamlaka?
 
Wanaopanga utaratibu wa Kanisani au Msikitini ndio wanaoamua Rais azungumze au la. Wakimkaribisha azungumze lazima atazungumza. Sioni tatizo lolote hapo.
 
Jifunzeni somo la uraia, msiwe wavivu wa kutafuta maarifa. Huwezi kumpangia rais mahali pa kuhutubia na kuongea. Rais sio diwani wala mwenyekiti wa serikali ya mtaa, ni nembo ya nchi. Ndio maana hata anapokuwa kwenye msafara mtu baki haruhusiwi kumpiga picha, tazama picha zote za marais utaona maelezo kwamba zimepigwa na mpiga picha wa Ikulu. Jifunzeni mambo madogo madogo kuliko kubakia mnajifunza mambo ya nchi za mbali ambayo hayana msaada na maisha yenu ya kila siku.
Watu wengi tu wanampiga picha sio kweli kwamba anapigwa picha na mpiga picha wa rais tu,akija mtaani au eneo lolote wanamfotoa,mbona magazeti yanampiga picha tu?television zinapata wapi video za rais?
 
Back
Top Bottom