Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 45,345
- 63,873
Nimeona Rais Samia anatangaza msiba wa Mwinyi (akielekeza sehemu ya hotuba yake ifutwe pasipo kujua yuko live, kwa hili kwanza kurugenzi ya mawasiliano ikulu ilitakiwa ivunjiliwe mbali na waajiriwa wote katika hicho kitengo wakiongozwa na Zuhura Yunus watimuliwe kazi).
Pia hivi karibuni Rais alikuwa mstari wa mbele katika mipango ya mazishi ya Edward Lowassa, Hata waziri mkuu Majaliwa alipofika kutoa salamu za rambirambi kwa mara ya kwanza alisema anamwakilisha Rais!
Magufuli alihusika kutangaza kifo cha mkapa na Mkapa pia alitangaza kifo cha Nyerere. Sina uhakika vifo vya makamu wa Rais na mawaziri wakuu waliopita walipofariki vilitangazwa na nani na nani alikuwa mhusika mkuu katika mipango yao ya mazishi.
Kwa maoni yangu Rais aliye madarakani angehusika kutangaza vifo vya baadhi ya viongozi tu vinapotokea tena wale ambao wanakufa wako madarakani/katika nafasi na kuwa muhusika mkuu katika misiba hiyo. Viongozi hao iwe ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mkuu wa majeshi, Jaji mkuu na Spika wa bunge tu.
Matangazo ya vifo na mipango ya misiba mengine yote hususani ya viongozi wastaafu waachiwe Msemaji wa serikali, Makamu wa Rais, Waziri mkuu na familia zao kushughulika nayo na kuwa mstari wa mbele.