Profesa Ibrahim Lipumba awaomba radhi Wazanzibar, yupo tayari kuachia Uenyekiti wa CUF

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, leo Jumamosi tarehe 12 Februari, 2022 amesema nafasi yake iko wazi…

"Natoa wito na kuwahakikishia wanachama kwamba, hii nafasi ya mwenyekiti iko wazi kwenye uchaguzi unaokuja, kwa maana kwamba kila mmoja anaweza kugombea nafasi hiyo.

“Nawaomba radhi Wazanzibar niliowakwaza katika mgogoro, nawakaribisha tujenge chama. Kwa upande wangu wakati wa mgogoro hawakunitendea haki na kunielezea mambo yasiyo ya kweli niliyoyasikia na nisiyoyasikia, nimewasemehe yaliyopita si ndwele.

“Nasisitiza vijana tujitokeze kugombea nafasi zote ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti wa Taifa, kwamba Lipumba hajawa na hatakuwa kikwazo kwa watu kujitokeza kugombea nafasi hizo,”- Lipumba.

Lipumba.jpg


Prof. Lipumba awaomba radhi Wazanzibar, yupo tayari kuachia Uenyekiti wa CUF

Prof Ibrahim Lipumba aomba radhi

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, leo Jumamosi tarehe 12 Februari, 2022 amesema nafasi yake iko wazi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza leo Februari 12, 2022 akiwa anazungumza na vyombo vya habari, amabao amesema kauli anaitoa kufuatia kuwafanya Wanachama wa Chama hicho kufahamu kuwa nafasi hiyo hipo wazi kwa yoyote anayetaka kugombea.

Pia Prof. Ibrahim Lipumba amewaomba radhi watu wote waliokwazika kwenye mgogoro uliojitokeza baina yake na Maalim Seif Shariff ambaye alikuwa katibu Mkuu wa Chama hicho kufuatia Lipumba pamoja na wenzake tisa kufukuzwa, kabla ya kutambuliwa na Ofsi ya Msajili wa Vyama vya siasa kuwa ni Mwenyekiti halali wa Chama hicho.

"Natoa wito na kuwahakikishia wanachama kwamba, hii nafasi ya mwenyekiti iko wazi kwenye uchaguzi unaokuja, kwa maana kwamba kila mmoja anaweza kugombea nafasi hiyo.

“Nawaomba radhi Wazanzibar niliowakwaza katika mgogoro, nawakaribisha tujenge chama. Kwa upande wangu wakati wa mgogoro hawakunitendea haki na kunielezea mambo yasiyo ya kweli niliyoyasikia na nisiyoyasikia, nimewasemehe yaliyopita si ndwele.

“Nasisitiza vijana tujitokeze kugombea nafasi zote ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti wa Taifa, kwamba Lipumba hajawa na hatakuwa kikwazo kwa watu kujitokeza kugombea nafasi hizo,”- Lipumba.

Kwa muda mrefu chama hicho kimekuwa kikiandamwa na migogoro isiyokwisha kitendo kilicho pelekea aliyekua katibu mkuu wa chama, Hayati Maalim Seif Shariff Hamad kuhamia chama cha ACT Wazalendo.

Hatua ya Prof.Lipumba kutangaza utayari wake wa kuachia nafasi hiyo inatajwa kua ni dalili ya kuwavuta wanachama waliokimbia chama hiko ambao siku chache zilizopita walitangaza kujiondoa ACT Wazalendo.

Prof. Lipumba amewataka wanachama wa chama hicho watakao kuwa tayari kuwania nafasi ya Mwenyekiti kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2022 kujitokeza kwenye kinyanganyiro

Chanzo: www.tanzaniaweb.com
 
Baada ya ccm kumtumia kama toilet pepa sasa katupwa chooni..ametumika kuharibu juhudi za ukawa..kaharibu juhudi za urais wa marehemu maalimu Seif huko zenji..katumika kukigawa nakuua chama chake..leo anakuja na ngojera za kitoto.

Kiufupi katumika kuua demokrasia nchini..hastahili kabisa kuomba hata huo msamaha..mana ni kama dharau.

Kiufupi haaminiki tena na cuf imeshapoteza mvuto wake...kweli profesa lipumba...fu.

Naona moyo unamuuma sana kuona act wazalendo inastawi huko zenji huku yeye akiishi kula nyasi..

Aliwahi kumwambia polepole kuwa njaa ikihamia kichwani ni mbaya sana...yeye njaa yake ndio imemmaliza kisiasa.

Shetani hanaga urafiki atakutumia kisha atakuacha ukiadhirika.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ashakwama sasa anajaribu kutafuta popularity, alifkiri akimnyanganya maalim seif chama ataondoka na jopo la wazanzibari, Never..! kaachiwa chama na ofisi pale bugurun labda na meza na viti viti tu piriad..,
 
Ni habari mbaya kwa ACT wazalendo.
Lipumba amesoma alama za nyakati na kuamua kwenda na upepo unapovuma.
Kisiasa tunasema ameamua kuzichanga karata zake upya.
Sio maamuzi yake. Ni maelekezo, ili kukipa uhalali chama kile kwenye chaguzi zifuatazo, kuelekea 2025 ni kama vyama vingine ikiwa na pamoja na ACT jinsi vinavyotumika.
 
Back
Top Bottom