Prof. Issa Shivji: Binadamu akifungiwa njia za kutoa/kupokea mawazo anakufa kiakili

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,846
5,057
"Samaki akifungiwa mdomo, anakosa hewa, anakufa kimwili. Binadamu akifungiwa njia za kutoa/pokea mawazo, anakufa kiakili. Inazaa taifa la majuha" - Profesa Issa Shivji

Hapa sijaelewa vizuri kuwa anamaanisha nini?

Ni nini maoni yako kuhusiana na huu usemi wake?
 
Huyu nae kashakua muoga tu, sasa misemo na nahau za nini, si aseme wazi tu anamansha nini?
 

nae anaongea nini huyu, wao si ndio wanaosadia kupumbaza watu wakiambiwa watoe maoni ya kujenga taifa kwa mitazamo ya akili zao wanatoa maona ya mitazamo ya matumbo yao
 
Nadhani kasikia lile suala la TCRA kuhusu watu kama kina Milard ayo wanaotumia youtube kuweka video za habari kutakiwa kuwa na Lesseni! Kuwa prof halafu ukawa nyumbu kama huyu mzee bora nife na masters yangu tu!!!! Mtu wa heshima kama huyu kwenye katiba alituangusha!! Kila siku anakuja na msemo na nahau, anajiita nguli wa sheria juzi kaulizwa swali kuhusu kuvunjwa katiba akapotelea mitini!! Unafiki tupu kama huwezi kuwa mkweli kuisaidia jamii unafiki wako peleka india!!!!
 
Hawa 'vinyonga' tulishaona rangi zao zote kwenye suala la katiba mpya. Wasomi wengi wa nchi hii tatizo letu kubwa ni 'njaa'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…