GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 6,819
- 9,649
Huu ni mfano tu, lakini huenda ukazaa mawazo chanya. Naamini, hitaji kubwa la nchi yetu kwa sasa ni mapinduzi ya fikra.
Chukulia, umeonekana wewe ni mzalendo sana kwa nchi yetu nzuri Tanzania, hivyo katiba ikabadilishwa na kukabidhiwa kiti cha urais kwa kipindi cha miaka mitano. Hutaruhisiwa kuongoza zaidi ya hapo.
Ili kukurahisishia utendaji wako, katiba ikabadilishwa, badala ya kuongoza kwa tarati za kawaida, ukaruhusiwa kuiongoza nchi kwa Presidential decree. Kwa kipindi chote cha uongozi wako, neno lako linakuwa ni sheria. Lengo ni ili kusiwepo na kizuizi cho chote cha kukukwamisha kufikia malengo utakayokuwa nayo ndani ya miaka mitano uliyopewa.
Ikiwa hilo lingetokea, wewe kama
wewe, ungeifikisha wapi Tanzania katika hicho kipindi cha miaka mitano?
Kwa kuwa utakuwa na mamlaka yote, isipokuwa tu ya kuua, utaachia madaraka katiba ikiwa katika hali gani?
Uchumi wa nchi na hali ya maisha ya wananchi itakuwaje?
Ni yapi yanayokukasirisha kwa sasa ambayo ungehakikisha unayarekebisha ukiwa Rais?