Poll: Mikataba ya hovyo ya madini na hasara taifa limepata, je nani alaumiwe?

Poll: Mikataba ya hovyo ya madini na hasara taifa limepata, je nani alaumiwe?


  • Total voters
    166
  • Poll closed .
Naona wajanja wajanja wanatengeneza mazingira kuonesha kuwa suala hili liachwe maana litakichafua na kukigharimu chama. Haiwezekani kuwa wanachama karibia milioni 9 wa ccm wote walihusika katika hii mikataba.
[HASHTAG]#Ramadan[/HASHTAG] kareem.


Na washawasha!
 
Update ya poll...
  • Katika kura 122 zilizokwishapigwa hadi sasa kura 118, sawa na asilimia 97% zimeihusisha CCM kama mhusika mkuu katika mikataba ya hovyo ya madini ama moja kwa moja au kupitia Serikali Kuu au Bunge au watendaji wa idara.
  • Ni kura 3 tu zimewalaumu wawekezaji sawa na asilimia 0.025%
  • Na Kura moja imekiri kutojua yupi wa kumalumu.
  • Hakuna kura hata moja imewahususha Vyama vya Upinzani.
Hivyo kulingana na mawazo ya wengi humu ni wazi adui yetu mkubwa Watanzania ni hiki chama cha kitapeli kilichong'ang'ania madaraka hata kama hakina uwezo wala uhalali. Kuendelea kujaribu kuwalaumu wawekezaji peke yao bila kuwahusisha washiriki wao wakuu, CCM na viongozi wake ni ujinga utakaotutafuna mpaka siku tutakapozinduka.

Mkuu kwani kabla ya poll ulijua mhusika mkuu ni nani??

ebu kuwa genuine fanyeni hima kuiondoa CCM na sio hizi sarakasi ambazo mnazipiga kila siku

maamuzi ya juzi ya chadema huko dodoma wewe kama mpigania mabadiliko uliyafurahia?

amin nakuambia....mpaka pale tutakapokuwa wakali na serious kwenye upinzani ndio CCM itaondoka otherwise the best we can do is complaining! discussing....na kuwa na poll kama hizi za kujifariji...nani asiyejua ccm ndio tatizo?

when we speak like this, kuwa tatizo sio ccm ni upinzani tunakuwa maadui
 
Kumbuka mambo yalianza kwa sera ya CCM ya uwekezaji, muswada wa sheria ukawasilishwa bungeni na kupitishwa na Bunge lililojaa wana ndiyo wa CCM. Hakuna namna Bunge lisilaumiwe kwani ni wao walikataa kupitisha sheria ya kutaka mikataba yote iridhiwe na Bunge. Kama walikataliwa walichukua hatua gani? Ni Tanzania ya CCM tu mambo kama hayo yangeweza kufanyika.
Lakini vyama vya upinzani walipoomba mikataba hiyo si serikali ya CCM ilikataa
 
Selikali ya awamu ya tatu ndio ya kulaumiwa! Nashangaa Lisu anakula sahani moja na Sumaye mmoja ya waliotufikisha hapa alafu eti anajifanya kupiga kelele!
Ni kweli chadema walikosea sana kulamba matapishi yao ila muda huu usitumike kulaumiana. Yeyote mwenye solution asikilizwe.
 
mpandaone said:
Namzee Wa joka lamakengeza
Huyo alikuwa mshauri tu Wa serikali. Ushauri unaweza ukafanyiwa kazi au usifuatwe. Hana hatia
Magufuli naye alikuwa ni Waziri tu wa Serikali, hana hatia!

Mkapa naye alikuwa ni Rais tu, hana hatia!

Bunge nalo lilikuwa tu watunga sheria, hawana hatia!

CCM nayo ilikuwa ni chama cha siasa tu, hawana hatia!

...nachoka!
 
Kura ziendelee kupigwa...tarehe 25/6/2017 tutatangaza matokeo tujue wa kumnyooshea kidole kwa wizi uliofanyika kwa muda wa miaka yote hiyo.
 
Wadau hakika inashangaza sana kuona wabunge wetu wanailalamikia Sheria ya Road Licence Sheria ambayo waliipitisha wao.Wabunge hao wao Leo wanajifanya kushangaa Sakata la mchanga wa madini wakati walitunga Sheria hiki in kioja.
 
Utakuja kushangaa pia wabwege wakipinga Sheria ya jeeeeeeeesi??????

Utaratibu wa kupitisha hiyo miswaada pale mjengoni si ushaikumbuka..........ungeeleweka Zaidi kama ungewashangaa wabwege wa Chama Chakavu Milele kulalamikia matunda ya ukilaza wao.
 
Ndiyo.

Ana haki ya kulalamika vizuri tu. Kuna sababu kadha wa kadha;

Moja, sheria hutungwa kutokana na nyakati. Huenda kwa wakati huo wakati Sheria ikitungwa na kupitishwa, sheria hiyo ilikuwa toshelezi kabisa. Lakini kwa sasa kutokana na mabadiliko ya Uhitaji na nyakati, sheria hiyo yapaswa irejewe na kufanyiwa mabadiliko.

Pili, aina ya upitishwaji wa Sheria siyo nzuri. Wengi hupitisha kwa matakwa ya Vyama vyao. Ilimradi tu wamekubaliana wenyewe bila kuangalia athari. Wanaosema ndiyo au Hapana siyo njia njema zaidi.

Tatu, sheria hiyo huenda ilitungwa wakati Mbunge husika hakuwa katika nafasi aliyopo sasa hivi. Hivyo, kwa kupata nafasi na kuelezea hoja zake mujarabu, ana haki ya kulalamikia na kuomba ubadilishwaji wa sheria husika.

Naam, kwa mantiki hiyo ana haki kabisa ya kulalamika.
 
Hasa wema wako utakuwa nini? umekunya wewe, harufu mbaya umeisababisha wewe, haya unajisifia umeondoa harufu, hiyo harufu si umeileta wewe?

Wabunge wa CCM wanajisifu leo eti wanapambana na Wezi wa Madini na Rasilimali za Taifa, Hivi hawa watu? ama ni manyama, Upinzani wamepiga kelele miaka yote mpaka kuwekwa ndani kwa uchochezi kisa kudai Mikataba ipitiwe Upya, leo aliyeingia Mikataba mibovu anajiona mpambanaji.
Tena kwa kukamata Mchanga ambao kimkataba wameruhusu ni mali ya Mwekezaki, Wapinzani wanataka Mikataba iletwe Bungeni na Sheria zilizopitishwa na CCM zibadilishwe, wao wanalia na walipoangukia, hii ni akili kweli?
 
Back
Top Bottom