Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,170
- 5,528
Kituo cha Utafiti cha Jeshi la Polisi kilichopo Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kwa kushirikina na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) imeendelea na mafunzo awamu ya pili kwa kundi la wanafunzi wa kozi ya uofisa ambayo yamelenga kuwajengea uwezo na maarifa mapya katika kupambana na ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa kitengo cha utatifi cha Jeshi la Polisi ndani ya chuo hicho Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ralph Meela, amesema kuwa kazi kubwa ya kituo hicho ni kufanya tafiti na kushirikiana na Taasisi za Elimu ya Juu katika kuwaongezea uwezo Maafisa na Askari wa Jeshi hilo.