Poleni mashabiki wa Ali Kiba, hatimaye leo amepost!

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Ali Kiba ni Msanii anae kumbwa sana na kurushiwa Maneno kuwa ana Dharau sana! Hii inatokana na vitu anavyo fanya! Sina uhakika kama ni kweli anadharau au vipi

Akiwa na Followers Million 1 huku yeye akiwa hajamfollow mtu yeyote yule Amekaa takribani wiki moja bila kupost chochote katika ukurasa wake Wa instagram! Mashabiki wengi walionekana kulalamika sana kuwa hawatendei haki Followers wake na mashabiki wake wanao mfuatilia kwani amekuwa akipost vitu kwa pozi sana katika ukurasa wake wa Insta

Hatimaye leo amepost video ya Dj akipiga wimbo wa unconditionally club! Nafikiri atapost tena baada ya siku mbili au wiki tena!

Poleni kwa walio mfollow alikiba poleni kwa mashabiki mnao mfuatilia alikiba kupitia Ukurasa wake wa Insta! Jaribuni kumzoea na kumvumilia,hata kama hatoi mipango yoyote ya mziki wake wala mipango ya show yoyote! Labda tumsubiri Hadi msimu wa sikukuu!

Huu mchezo hautaki hasira!
 
kugundua kitu nafsini mwa mtu~huwaga ni suala la kisaikolojia.
** ~
to determine personally something over somebody it's about psychologically matter.
 
Mi nnavyojua sio mastaa wote wanapost binafsi kwenye account zao. Wengi wanakua na managers wanao oversee social media zao na kuwapostia vitu muhimu.

I guess kiba hana hy ndo maana inambidi apost mwenyewe akipata nafasi
 
Kiba hana cha kupost kwa kua hayupo bize na muziki,kila afanyacho anagongesha mwamba unategemea nini?
Kiba size yake babu ayubu kwa sasa
 
Kiba mimi namkubali kuwa ni nguli na. 2 hapa nchini katika muziki wa kizazi hiki. Sitokubali kusikia yupo juu ya hapo so chini yake kwa kipindi hiki.

Namshauri awe makini kuna vijana wanakuja kasi watamshusha tu na kubaki na heshima ya mdomoni.

Kiba amepata pesa nyingi, tatizo ni kuwa na familia kubwa yenye watoto wengi. Anachokipata lazima akigawe kwa mama wa watoto wote hao kwa sababu watoto wote wanaishi na mama zao.

Hili liwe funzo kwa wasanii wengine kuhakikisha wanautumia ujana wao katika kutafuta pesa na siyo kuzaa hovyo.
 
Teh teh teh,
Nimefurahi kuona unamfatilia kwa makini hatua kwa hatua,
Inaonesha ni jinsi gani UNAMKUBALI KIAINA,
Nimefurahi pia kuona,
UNAM-MISS SANA.

#KingKiba4Real#
Baada ya kuona Mashabiki wake wanalalamika sana sehemu mbali mbali kuwa Jamaa anawaangusha ikabidi niende kuangalia kunani huko! Angalia post ya mwisho kupost kabla ya jana mashabiki wake wanavyo lalamika utawaonea huruma wanaomba jamaa apost hata kama akiwa anakula!
 
Kuhusu kipaji sina tatizo na Ali kiba, jamaa ana kipaji cha pekee, huwa hakosei anapopita juu ya mdundo.

Nje ya muziki Kiba ana tatizo huo ndio ukweli, bahati mbaya sana hilo tatizo ndo linamfanya hivi sasa ana role na akina Nuhu Mziwanda... daah sio level yake kabisa ila ndo hivyo.

Nilikubali sana Kiba, nilisimama kila nilipoona anasemwa vibaya ila sasa naweka siraha chini, nimechoka!

Kiba bingwa wa kuchezea nafasi halafu anaona sifa, hajiongezi hata kidogo. Kipaji bila juhudi na maarifa ni upuuzi tu! Na akae akijua hard work beats talent, if talent fails to work hard. Chibu ana kipaji cha kawaida ukilinganisha na Kiba ila tazama sasa, Chibu inabidi tu afanywe balozi wa kiswahili duniani maana hamna namna.
 
Mi naona Kiba si tatizo tatizo mashabiki,Kiba ameshakua kwenye game zaidi ya miaka kumi Ni Kama vile Zama zake zimepita naweza kumlinganisha na kina Jide,Ay,lakini wanafanya mziki wao watu tunasikilza tunaburudika wala hawashindanishwi Na mtu na maisha Yao yanasonga.

Tatizo mashabiki wa Kiba wanashindanisha wanamchanganya,hata huyo wanayemshindanisha naye yani Dai pengine baada ya miaka mitatu au mitano wataibuka vijana wengine Zama zake pengine zitakwisha sasa ni wakati wake.
 
Kiba yupo chimbo anaandaa mabomu ya maana, mcheki mwezi wa tano utanielewa...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…