mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,169
- 1,072
Ni ukweli usiofichika kwamba bado mazingira ya kufanya biashara/ujasiliamali ,kuanzisha biashara/ujasiliamali,kukuza/kunenepesha/kulea biashara/ujasiliamali nchini Tanzania si rafiki na magumu hasa kwa wanaoanza biashara/ujasiliamali/uwekezaji kwa mitaji midogo na kati.Utitiri wa kodi,Utimirifu wa Masuala ya ulipaji kodi ;ukadiriaji /utozwaji kodi;sheria za kodi;ushuru;utitiri wa taasisi zenye kulipwa tozo/malipo;Utitiri wa taasisi zinazofuatilia hili na lile kwa wafanyabiashara/wajasiliamali-viwanda{vidogo,kati} ni sehemu ya mazingira yasio rafiki kibiashara.
Nchi yetu bado ipo nyuma sana kiuchumi hivyo bado ni moja kati ya nchi maskini zaidi duniani.
Tatizo la ajira limetoa fulsa ya wengi kujiajiri katika sekta rasmi na zisizo rasmi kama biashara na ujasiliamali.Elimu ya ulipaji kodi,mfumo wa ulipaji kodi hasa kwa wanaoanza biashara au kujiajiri na kuwa tayari kurasimisha biashara bado una mapungufu makubwa na ni kigingi katika maendeleo ya wananchi maskini.mathalani:Hitaji la kulipa kodi ya mapato katika hatua ya usajiri wa biashara husika kupitia makadirio ya mapato.
Kumekuwepo na hitaji la wafanyabiashara/wajasiliamali {wapya,wa zamani,wakubwa,wadogo} kutakiwa kupata TAX CLEARANCE CERTIFICATE ili waweze kupatiwa leseni mpya waanzapo biashara au mwaka mpya wa kibiashara unapowadia.. Hili ni tatizo linalonyong'onyesha wafanyabiashara wengi hasa wadogo na wa kati kutokana na ufinyu wa ufahamu katika masuala ya usimamiaji mapato,mahesabu,matumizi na biashara kwa ujumla .Lakini pia mara nyingi figisufigisu za baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya mapato {TRA} kuwafanyia makadirio makubwa yakiambatana na vitisho ili kushawishi rushwa kutolewa.
Maendeleo ya kiuchumi ya taifa lolote msingi wake ni wafanyabiashara/wajasiliamali/wenye viwanda wadogo,wa kati..Taifa letu haliwezi kuendelea kwa viongozi wa kisiasa/serikali/TRA kutunga,kusimamia,kutekeleza sera /sheria kandamizi ama zisizo rafiki kwa wadau..yatupasa kulitazama hili kwa jicho la saba tukiiga nchi kama China,Thailand,Brazil,India ambako kutengemaa kwa uchumi kumesababishwa na mchango endelevu wa sekta ya wafanyabiashara/wajasiliamali katika viwanda vidogo na kati.
USHAURI

- Mapato mengi ya muda mfupi yasiwe chachu ya kuua kiu,nia,dhamira,malengo,ndoto,jitihada,ubinifu ambavyo vingeweza kulelewa na kuwa na manufaa makubwa kwa vizazi na vizazi kama kina Mercides benz,Tata,Hitachi,Sony,Toyota,Boeing,Bell,Ipp,Cocacola,Pepsi,...
- Urasimishaji wa biashara nchini Tanzania ni zoezi linaloendelea na lenye tija katika ukuaji wa uchumi na maongezeko ya makusanyo ya mapato kama kodi,ushuru,na malipo mbalimbali.Elimu zaidi inatakiwa ili kuwaelimisha wengi,kuwawezesha wengi na kuwasaidia wafanyabiashara wadogo-kati,wajasiliamali kukua na kuchangia pato la serikali na ustawi wa taifa sasa na baadae.
- Serikari ifute hitaji hili kwa biashara mpya na zinazoendelea na kuruhusu mamlaka/halmashauri/taasisi zinazotoa leseni kutoa leseni kwa masharti ya kupatiwa udhibitisho wa kulipa kodi/kutodaiwa kodi/kuwa safi ktk masuala ya kodi.
- TRA waweke utaratibu maalumu wa kutoa provisional tax clearance huku wakitoa muda maalumu kumwezesha mteja/mfanyabiashara/mjasiliamali/mwekezaji kukamilisha taratibu/mahitaji ya kikodi/kutatua madai ya kodi huku akiendelea kufanya biashara na kukuza uchumi kwa namna moja au nyingine {ajira,mzunguko wa fedha,n.k}
- TRA iweke utaratibu rafiki sana na maalum wa kuwasaidia,kuwaelimisha wafanyabiashara/wajasiliamali/wawekezaji wa ndani namna ya kutekeleza,kumudu,kusimamia compliance ya masuala ya kodi kwa kuajiri maafisa biashara watakaokuwa na jukumu la kuwazungukia/kuwatembelea/kuwaelimisha/kuwawezesha wadau husika kwa ufahamu,weredi,amani na uzalendo.
- TRA iweke maafisa biashara/maafisa elimu maalumu katika kila mamlaka ya utoaji leseni kwa ajili ya elimu,uwezeshaji kiufahamu,miongozo,utaratibu,ufafanuzi wa taratibu/sheria/kanuni..n.k kama ambavyo wanafanya ktk maonyesho ya 77,88,utumishi wa Umma n.k ambako mamilioni hutumika pasipo tija stahiki kwa wadau sahihi.