Pendekezo: Utunzaji wa garden za Dar, wakabidhiwe Jeshi

Magufuli amesikia kilio chenu, akawateua wajeda kuwa wakuu wa wilaya. Guess what, Mmemkejeli sana humu humu kwenye forum! Watanzania hatujui tunataka nini.
 
Nashauri jukumu hilo wapewe NBC bustani yao ya ,NBC makao makuu inayoitazama bandari ni nzuri
 
baada ya hapo tutasema sukari wauze na kusambaza wajeda, then bandari Wakabuthiwe JWTZ, baadae tuwape shule zote wafundishe ili kuongeza ufaulu.....mwisho kabisa kuwakabidhi nchi
 
mkuu ya lugalo umefanikiwa kuiona??
Wenye jukumu la kutunza bustani za jiji ni halmashauri kinachotakiwa wafanye kazi hiyo kwa ufanisi tusikimbilie kuwapa majukumu vyombo/taasisi ambazo siyo jukumu lao la msingi kutunza bustani.
 
Ile Bustani kwa kweli ni nzuri sana,ila nasikitika kuwatangazia kuwa mradi wa BRT utaibomolea mbali.

Wangefikiria kufanya mwendokasi ya majini badala ya kuharibu hizo barabara hazijamaliza hata miaka mitano vinginevyo hizo barabara za mwendokasi mpya zijengwe pembeni mwa hizo zilizopo na vituo vyake vijengwe kwa utaratibu wa kupishanisha kwakuwa bilions of money zimeshateketea hapo
 
Jamani siwakatishi tamaa ila mbona hiyo bustani ya lugalo barabarani ni ya kawaida sana haijavuka viwango vya kusifiwa?
Bustani na mandhari ni jukumu letu sote, ni kitu inaanzia mioyoni mwetu wote, hakutakuwa na maana kama tunadhani jeshi ndio wa kulinda bustani.

Tazama barabara ya posta kuanzia moroko, eti wameweka minyororo kuzunguka hicho kinachoitwa garden, garden yenyewe chafu hata haina mvuto sasa tuna protect nini, au ilikuwa ni tenda tu ya kulindana maana hivyo vichuma vya bendera ya TZ na nyororo kama wameachafua tu.

Nashauri haya mambo yaanzie mioyoni mwa watu
 
Back
Top Bottom