Pendekezo Korofi: Wabunge na Madiwani Wakatazwe Kufanya Hili

MMM zile post zako ambazo wadau huwa tunajifunza mambo zimeenda wapi? Siku hizi post zako ziko chini ya kiwango mkuu.
 
Hujamjua huyo! Hapo anamtafuta Nasari kwa vile kanunua vitanda vya hospitali kule Arumeru. Huyo jamaa ni hatari sana anapoamua Kutumika katika propaganda. Issue ya Nasari kujitolea kwa moyo wake kuna watu imewaumiza

MMM siku hizi post zake ziko sawa na Jingalao, yaani ameporomoka kwa kasi. Mbunge kuwasaidia wananchi wake kosa liko wapi?
 
Naamini misaada inayotolewa na viongozi wa kisiasa kwa wananchi ni hongo. Na inawezeshwa na ukwasi wa kufuru walionao wabunge na unaotokana na mishahara mikubwa na posho nono vinavyo idhinishwa na serikali kuwalainisha ili kupitisha miswada ya kuibeba serikali.
 
Huyu foreigner siku hizi pumba kabisa! Kwa nini mtu umzuie kutoa mchango wa maendeleo ya jimbo lake? Yaani tangu Magufuli aingie madarakani, unachojua ni kuzuia tu!

Wewe kama hutaki kuchangia maendeleo ya nchi yako, kaa huko ambako wenzio walichangia yakawa bora wewe ndio sasa unafaidi.
 
Huyu Mwanakijiji yeye mwenyewe alishawahi kusaidiwa nauli ya kuja Dar na Dr. Slaa. Binadamu wasahaulifu sana.
 
Kwa kawaida jukumu lao ni kuwakilisha wananchi, kukumbusha serikali namna bora ya kufanyia kazi hoja mbalimbali za wananchi; Nchi inao mfumo ulio mahsusi ambao ukifuatiliwa na kutenda kazi, wanasiasa hawatakuwa na muda wa kutoa hizi takrima ( I owe you).

Ukitizama wakati wanatoa hiyo wanayoiita misaada wanakuwa wametinga magwanada rasmi ya vyama, hivyo kuleta fikra kwamba wapenzi wa chama kingine, au wale wasio na vyama hawana haki katika kupokea hayo.

Serikali ipo kuanzia ngazi ya taifa, mawizara na idara mbalimbali, Mikoa na uongozi wake, wilaya, halmashauri n.k. wote utawakuta wana mpango kazi wa maendeleo kwa wananchi wote, lakini utashangaa na hawa wa kuchaguliwa na kuteuliwa; wabunge, madiwani n.k. wanaibuka na mipango yao!!

Mimi nakuhakikishia kwamba kama miundo ya kiserikali ingetenda kwa uadilifu na ufanisi, pasingekuwa na sababu ya kulipa mishahara minene na posho za vikao vingi za wabunge; kwanza ndizo zinazowapa vifua vya kutoa "misaada" na kutukuzwa.

Pia kuendelea kutatua kero za wananchi miaka yote! Inatakikana kwamba kero ziiishe ili kazi iwe kwenye kutekeleza mipango ya maendeleo kuongeza vipato na pato la taifa, kufanya mambo makubwa badala ya ku invest kwenye kero kila uchao.

Namba niongeze ka swali hapo, Je, Kingetokea au Kitatokea nini kama mifumo rasmi ya kiserikali itafanya kazi kwa ufanisi na kuondoa kero za wananchi haraka ili ku focus kwenye maendeleo?
 
Wengine huwa wanadandia misaada ya wafadhiri na kuonekana wao ndio wamewezesha.
 
Hili swala tunaweza kuliangalia kirahisi sana lakini huko tuendako litatughalimu sana. Wabunge na madiwani watajikuta wanaacha majukumu yao ya msingi ya kusimamia serikali na maendeleo badala yake wataanza kushindana kutafuta misaada huko serikali ikijifanyia yake bila usimamizi
 
  • Thanks
Reactions: KXY
Mtoa mada enzi zake alikuwa akitoa mada karibu wat wote wanamuunga mkono leo imekuwa kinyume chake.
 
Hoja au mapendekezo ya mtu aliye out of touch... Hata huko ulipo kuna viongozi wa kuchaguliwa wanatoa misaada uner their name of their charities, sasa sijui inakuaje unaleta haya wakati Tanzania unaijua

I think you are doing this simply kwasababu umeona mwamko wa wabunge wa ukawa kuchangia maendeleo ya majimbo yao... Kinakuwasha, kinakuuma, kinakukereketa na kukupwita

Wacha watanzania tuishi kitanzania, wewe kama unaipenda sana tanzania rudi nyumbani tuishi wote the "real life"
...you said it all brah....seems jamaa anaumia watu wanapofanya charity activities.....sioni kwanini watu wasitoe misaada kama wanaweza kwenye jamii iliyokithiri umaskini kama TZ.....Huko nje ya nchi kama USA watu wanatoa misaada pamoja na utajiri wa watu wao ije iwe TZ!!!....yani badala ya kushukuru watu wanatoa misaada watu wanasema wazuiwe??....amazing.....Noana mtoa hoja anataka kuharamisha misaada hii ili ionekane kama takrima or something...lakini anasahau kuwa hawa wanaotoa misaada tayari ni watumishi halali kwa watu wao baada ya kuchaguliwa(ama kuteuliwa).....hapa hamna swala la hongo...maana watu hawa tayari wanahudimia jamii kwa nafasi zao za ubunge..sasa unawazuia ili iweje???......Mtoa mada angesema serikali wa discourage michango ya harusi ili watu wachangie maendeleo yao ningeelewa ana uchungu na maisha mabovu ya watanzania...lakini kwa ku suggest kufutwa misaada ya wabunge kwa watu wao ni unafiki.....
 
Duh kweli tumeharibiwa; ndio maana mwanzoni tuliwaita "wafadhili" siku hizi tunawaita "washirika wa maendeleo"! From Donors to Development Partners! Na ombaomba wabadilishwe majina - kutoka Ombaomba hadi Wenye Kiu ya Maendeleo!
Ujumbe wako mzuri sana kaka, misamiati mingi inatumika lakini haina uhusiano wa moja kwa moja na shida za walio wengi. Wachache wanafaidika na wengi wanabaki na maisha ya shida. Nimesikiliza taarifa ya habari ya usiku wa leo kupitia Channel 10, wanasema duniani kuna watu 60 ambao ni matajiri wenye kuweza kuwalisha watu wote duniani. Ni hawa kina Bill Gates ambao wakija Afrika wanapewa majina tofauti na ambayo yanajaribu kupunguza makali ya unyonyaji wanaoufanya, ambao unawaumiza walio wengi.
 
CCM wanatoa rushwa, why? Ni kwasababu chama chao ndo kipo madarakani,.. Kwahiyo hao CCM ni haki kutoa hizo vitu kwa wananchi bila sifa bila kuleta waandshi wa habari,..

Ila Ukawa ni haki kutoa coz ni chama pinzani so hivyo vitu ilibidi serikalui itoe kwa wananchi wake bt rulling party kimeshindwa kutoa hivyo vitu,...

So tunakuja kuona CCM wanaiga hawana jipyaa zaidi wanatatapa na kuigiza igiza vitu wasivyoviweza..
 
Back
Top Bottom