Pakistan: Watu 72 wafariki shambulio la Islamic State katika madhabahu

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
18,716
28,622
Watu 72 wamefariki dunia kwenye shambulio katika madhabahu maarufu ya Wasufi kusini mwa Pakistan, polisi wamesema.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika katikati mwa waumini katika madhabahu ya Wasufi ya mtakatifu Lal Shahbaz Qalandar katika mji wa Sehwan, mkoa wa Sindh.

Waziri mkuu Nawaz Sharif amelaani shambulio hilo.

Wapiganaji wa Islamic State, Taliban nchini Pakistan na makundi mengine ya wanamgambo, wamekiri kuhusika.

Madhabahu hayo ni miongoni mwa yale ya kale zaidi na yanayotukuzwa sana na yalikuwa yamejaa watu Alhamisi, kwani siku hiyo huchukuliwa kuwa tukufu kwa Waislamu kufanya sala katika madhabahu hayo.

Walioshuhudia wanasema mshambuliaji alijilipua watu walipokuwa wakicheza dansi ya imani.

Vyombo vya habari zinasema alirusha guruneti nakisha akajilipua.

"Niliona miili imetapakaa kote. Niliiona miili ya wanawake na watoto," mwanamume mmoja aliwaambia wanahabari.

Chanzo: BBC Swahili
 

Babati, vipi zamu yako haijafika? Jiandae kusafirishwa. Safari ijayo ni zamu yako.
 
Nilishawahi kusema kuwa hii itikadi ya kuua mnaowaita makafiri si nzuri,wakasema wao ni raha sana kuua makafiri na wanafurahia wakiua watu hovyo,leo mmeuliwa ninyi mnaliiia hata wasio waislam wanaumia kama ninyi,nawapongeza waliotekeleza hayo mauaji ili iwe funzo kwa waislam wote duniani kuwa kuuwa watu si jambo zuri
 
Interesting! Mbona red (underlined) na blue haviendani! Mtakatifu halafu muislamu! Tangu lini ndani ya Islam kukawa na watakatifu/utakatifu? This is big joke! Hebu wataalamu nisaidieni japo mstari mmoja wa Koran unaozungumzia utakatifu.
 
Interesting! Mbona red (underlined) na blue haviendani! Mtakatifu halafu muislamu! Tangu lini ndani ya Islam kukawa na watakatifu/utakatifu? This is big joke! Hebu wataalamu nisaidieni japo mstari mmoja wa Koran unaozungumzia utakatifu.
Hii habari nimeitoa bbc
Kwahiyo kwenye islam hakuna utakatifu kuna mauti na mizigo ya dhambi tu bas au unamanisha nini ustadh
 
mi huwa nawaza kuwa watu hutumia tu mgongo wa dini ili kufikia malengo yao ya kisiasa. hakuna njia nzuri y kukusanya watu kwa lengo fulani kama kutumia dini. haya mambo yamepamba moto baada ya kuwa na power vacuum huko Afghanistan, Iraq na Syria. hiyo inaonyesha kuwa haya si mauaji ya kidini bali ya kugombania mamlaka.
 
Well said
 
Sasa mbona waislamu hawakemei na kulaani matukio pindi wakiuawa wasio waislamu,?!!!!!?
 
Pole yao hao waliofariki wahifadhiwe mahali panapostahili MWENYEZI MUNGU tuokoe na vita hivi vya kidini
 
Soma article vizuri, yawezekana hiyo madhabahu siyo ya waislam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…