Oparesheni za Kijasusi zilizofanikiwa zaidi katika Historia

Members: Kumradhi kwa kuwakatisha uhondo wa Makala ya Kifo cha JF Kennedy, nitaendelea nayo siku si nyingi. Mniwie radhi.


OPARESHENI 5 ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI KATIKA HISTORIA


Katika mfululizo wa Makala hii mpya, tutachambua Oparesheni kubwa tano za kijasusi (na kijeshi lakini kushirikiana na idara za ujasui) ambazo zilitekelezwa kwa kutumia weledi uliotukuka na umaridadi wa hali ya juu sana.

Kama wewe binafsi au ndugu au jamaa au rafiki, umepitia mafunzo ya weledi wa kijeshi (special Force, au "ukomando" kama tulivyozoea kuita) au labda mafunzo maalumu ya Ujasusi basi ni imani yangu umewahi kusoma kwa kina japo 'darasani' kwenye makaratasi juu ya mojawapo (au zote) kati ya oparesheni hizi ambazo nitazichambua kwenye makala hii. ninaposema kuzisoma kwa kina, namnaanisha kufundishwa juu ya weledi, teknikaliti, sacrifise na uzalendo uliotukuka ambo umedhihirika katika opereseheni hizi.

Tuanze na hii ya kwanza...



OPERATION ENTEBBE


Jina mbadala: Operation Thunderstorm/Operation Yonatan



Watekelezaji:
-MOSSAD
- IDF (ISRAEL DEFENCE FORCE)



Kitengo cha Weledi:
Sayeret Matkal


Mwaka wa utekelezaji
: July, 1976

Nchi: Israel/Uganda


Silaha za kukumbukwa:
Lockheed C-130 Hurcules


Wahusika wa kukumbukwa:
- Yonatan Netanyahu (kaka wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu)
-Ehud Barak (alikuja kuwa Waziri Mkuu miaka ya karibuni)

View attachment 524078



MOSAD & IDF: OPERATION ENTEBBE



Siku ya tarehe 27 June mwaka 1976 ilianza kama siku nyingine yioyote ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa nchi ya Israel Tel Aviv, uwanja ujulikanao kama Ben Gurion International Airport. Moja kati ya ndege ambayo ilikuwa inafanya safari yake katika siku ya elo ilikuwa ni ndege ya kampuni ya Air Frace ambao walikuwa na ndege yao ya Air France Flight 139 ambayo ni ndege aina ya Airbus A300B4-203 yenye namba ya usajili mkiani F-BVGG (c/n 019).

Ndege hii ilikuwa inafanya safari yake katika siku ya leo kutoka Tel Aviv na ilikuwa inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Charles DE Gaulle International Airport jijini Paris, Ufaransa. Baada ya taratibu na protokali zote za uwanja wa ndege kukamilika na abiria wote kukwea kwenye ndege, ndege iliruka kutoka kiwanjani ikiwa na abiria 190 ndani yake pamoja na ‘crew’ ya watu 12 (Marubani na wahudumu) ambamo asilimia kubwa ya abiria walikuwa ni raia wa Israel pamoja na watu wenye asili ya kiyahudi. Ndege iliruka kutoka Tel Aviv mpaka jijini Anthens, Ugiriki ambapo ilichukua abiria wengine wapatao 58. Baada ya hapo ndege iliruka pasipo kujua kwamba kati aya abiria hao 58 waliowachukua Ugiriki ndani yao kulikuwa na abiria wanne ambao walikuwa ni wanachama wawili wa kikundi cha Popular Front For The Liberation of Palestine – External Operations (PFLP-EO) kutoka Plaestina na wanachama wawili wa kikundi cha Revolutionary Cells kutoka nchini Ujerumani.

Baada ya abiria wote kukamilisha utaratibu na kupanda ndani ya ndege, ndege iliondoka uwanjani Athens mnamo amjira ya saa 6 na dakika 30 mchana kuelekea Paris, Ufaransa.
Dakika chache baada ya ndege kuruka rubani mkuu wa ndege ambaye ndiye alikuwa ameshikili ‘usukani’ Bw. Michel Bacos akasikia kelele nyuma ya ndege wanakokaa abiria (cabin). Ili kujiridhisha kwamba kila kitu kiko sawa, rubani Michel Bacos akamuagiza msaidizi wake mmoja wapo ambaye ndiye alikuwa injinia wa ndege aende kuangalia nini kilikuwa kinaendelea.
Mara tu baada ya msaidizi huyo kufungua mlango wa mbele wa chumba cha marubani, alikutana uso kwa uso na bastola usoni mwake iliyoshikiliwa na mtu ambaye mkononi alikuwa amebeba bomu la kurusha kwa mkono. Huku msaidizi huyo akiwa bado ameshikwa na bumbuwazi, mtu huyu mwenye bomu mkononi na bastola (jina lake anaitwa Wilfred Bose raia wa Ujerumani) alimsukuma yule injinia nakumrudisha tena ndani ya chumba cha marubani na kisha yeye mwenyewe pia kuingia.

Mara tu baada ya kufika ndani ya chumba cha marubani, akawaweka chini ya ulinzi marubani ambao bado walikuwa kwenye mshituko wa mshangao na kisha kumnyanyua rubani msaidizi kutoka kwenye siti yake na kukaa yeye. Baada ya kukaa kwenye siti ya rubani msaidizi kitu cha kwanza alichokifanya haramia huyu Wilfre Bose ni kuchukua microphone ambayo marubani huwa wanatumia kutoa matangazo kwa abria, na baada ya kuiweka microphone akatoa tangazo lake la kwanza, kwa sauti ya utulivu iliyojaa lafudhi nzito ya kijerumani, akawasema; *“..kuanzia sasa ndege hii inaitwa HAIFA 1, badala ya Flight 139..”*

Haifa ni eneo (mji) maarufu ulipo kaskazini mwa nchi ambayo abiria wengi waliopanda kwenye ndege hiyo walitambua kama Israel lakini watekaji hawa na watu wengine duniani wakitambua kama Palestina.

Mara tu baada ya tangazo hili kusikika kwenye vipaza sauti vya ndege, abiria wote licha ya kuwa kwenye mshituko mkubwa wa ghafla lakini moja kwa moja waling’amua ni nini kilikuwa kinaendelea. Flight 139 au Haifa 1 kama alivyoibatiza aliyetoa tangazo, ilikuwa imetekwa na maharamia.

Baada ya Tangazo hili, haramaia Wilfred Bose akamuamuru rubani Michel Bacos kuendesha ndege kuelekea mji wa Bengazhi, nchini Libya.
Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Bengazhi nchini Libya, ndege ilitumia karbia masaa saba uwanjani hapo kwa ajili ya kujaza ndege mafuta. Katika masaa hayo saba kuna mwanamama Patricia Martel mwenye asili ya Uingereza lakini akiwa ameolewa nchin Israel miaka michache iliyopita alifanya ‘kituko’ ambacho kilikuja kuwa na manufaa sana baadae. Wakati ambao ndege inaendelea kujaza mafuta kwa masaa yote hayo, huyu mama ambaye ni nesi kwa taaluma, alianza kulalamika juu ya maumivu ya tumbo yaliyopitiliza. Aliwaeleza watekaji kwamba ana ujauzito. Maharamia haya yakaruhusu wahudumu wa ndege wamuhudumie mwananmke mwenzao kwa vile ambavyo wataweza kwa kuzingatia kwamba ana mimba. Baada ya kuhudumiwa kwa karibia saa nzima, Patricia akatumua ujuzi wake wa unesi akafanya alicho kifanya na ghafla akaanza kutoka damu kiduchu sehemu za siri. Baada ya damu hizi kidogo kuanza kumtoka na kulalamika kuwa maumivu yamemzidia ndipo hapa ambapo wahudumu wa ndege wakaripoti kwa maharamia kuwa mimba ilikuwa imetoka.

Kwa huruma na ili kuepusha taharuki ndani ya ndege maharamia hawa wakamuachia huru mwanamama Patricia Martel hapo uwanja wa ndege mjini Bengazhi ili aweze kupata uangalizi mzuri zaidi wa kidaktari.

Lakini ukweli ni kwamba Patricia hakuwa na mimba wala hakuwa na maumivu yoyote tumboni, alichokifanya ilikuwa ni uigizaji pamoja na kuchanganya utaalamu wake wa fani ya unesi na kuweza kuwahadaa maharamia hao.

Baada ya kuachiwa Patricia alikuwa ni mtu wa kwanza muhimu kutumiwa na Mossad kujua taarifa sahihi zaidi kuhusu nini hasa kilikuwa kinaendelea ndani ya ndege, kulikuwa na watekaji wangapi, jinsia zao, silaha zao na vingine vyote ambavyo alifanikiwa kuviona.
Baada ya hapa Bose akamuamuru tena rubani Michel Bacos kurusha tena ndege angani pasipo kumueleza kuwa wanaeelekea wapi.

Wakiwa angani ndipo alianza kumpa maagizo wapi hasa anataka waelekee. Upande wa abiria kwenye cabin ambao nao walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi na maharamia wengine waliosalia, wao hawaku wanafahamu hata ni wapi walikuwa wanaeleke. Ndege ilikuwa inaruka angani kwa karibia masaa 24. Abiria wengi walianza kuhisi labda ndege ilikuwa inaruka kuelekea China au labda Siberia, na vichwani mwao walikuwa wanajiuliza kwa nini walikuwa wanapelekwa huko.

Lakini laiti kama wangelijua mahali ambako walikuwa wanapelekwa basi wangetamani ndege hiyo ielekee kweli china.

Baada ya ya takribani masaa 24 ndege kuwa angani tangu iruke kutoka Bengazhi nchini Libya, hatimaye abiria walisikia ndege ikitua na kugusa Runway ya kiwanja cha ndege mahali fulani dunia walipowasili lakini wakiwa hawafahamu ni mwapi hasa walikuwa.

Baada ya matairi ya ndege tu kukanyaga lami za runaway na abiria kufungua ‘pazia’ (shutters) kwenye vioo vilivyopo pemnbeni mwa siti zao na kuangalia nje, mara moja wakaelewa wako wapi. Nje uwanjani kwenye lami, kulikuwa kumesimama lijitu la miraba minne lenye ngozi nyeusi tiiii likiwa na walinzi wa kijeshi na wengine waliovalia nguo za kiraia likiwa limezungukwa pande zote na walinzi hao. Mtu huyu mwenye umbo la kutisha kwa kipindi hiki alikuwa anajulikana ulimwenguni kote kutokana na matendo yake na ukatili wake. Kwa kutupa jicho mara moja tu haukuweza kukosea kujua kuwa pale kwenye lami uwanjani, alikuwa amesimama Generali Nduli Idd Amin Dadaa, ‘Field Marshal’. Swali lilokuwepo vichwani mwao lilikuwa limejibiwa tayari, wamepelekwa kwenye ardhi ya moja ya watawala ‘watemi’ na katili kuwahi kutokea juu ya uso wa dunia. Walikuwa nchini Uganda.

Baada ya ndege kusimama abria wote 248 ambao wengi wao walikuwa ni raia wa Israel na wayahudi, walishushwa kutoka kwenye ndege na moja kwa moja kupelekwa ‘terminal’ ambayo kwa wakati huo ilikuwa haitumiki. Mpaka muda huu wakang’amua kwamba hawakuwa ‘abiria’ tena kama ambavyo waliondoka Tel Aviv, bali sasa walikuwa ni mateka wa maharamia haya ya kijerumani, palestina na jeshi la Uganda.

View attachment 524095
Uwanja wa ndege wa Entebbe siku ya utekaji

Wakati huo huo…

Nchini Israel katika jamii ya masuala ya usalama walikuwa wako kwenye bumbuwazi kuu, matukio ya dizaini hii huwa ni ya kushtukiza na yanatokea kipindi ambacho ‘haujajiandaa’. Pia kwa kipindi hiki bado Idara ya Ujasusi ya Mossad hawakuwa na Intelejensia ya kutosha za nchi nyingi za kiafrika, akili yao na nguvu yao yote ilikuwa kwenyekudhibiti juhudi za nchi za kiarabu kufuta Israel kutoka kwenye eneo hilo walilopo. Kwa hiyo kitendo cha raia wao wengi kiasi hiki kutekwa na kupelekwa Africa kilikuwa si tu na changamoto ya namana gani wanawaokoa bali pia kulikuwa na changamoto ya uwepo wa Intelijensia ya kutosha kuhusu eneo la Entebbe, Uganda kuweza kufanya oparesheni yoyote ya kijeshi.

Ndipo hapa ambapo waziri mkuu wa kipindi hicho wa Israel Yitzhak Rabin akaitisha kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa jeshi na Mossad na kuwauliza swali moja tu, *“…tunafanayeje?”*







Itaendelea…





THE BOLD




SEHEMU YA PILI



Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao.

Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii.

Baada ya kuwatenganisha raia wote wa Israel na kuwaweka kwenye chumba kingine peke yao hapo hapo kwenye terminal, kuna mwanadada raia wa Ufaransa aliyeitwa Jocelyne Monier yeye jina lake halikuitwa kwenye ile list ya wanaotakiwa kutengwa kwenye chumba kingine (Waisrael na Wayahudi). Lakini ‘boyfriend’ wake alikuwa ni Muisrael na aliitwa jina na kutengwa na wengine katika kile chumba kingine. Mwanadada huyu ili kuonyesha kumtia moyo mpenzi wake na kupinga huu ubaguzi uliokuwa unafanywa na hawa magaidi, kwa hiari yake alijipeleka kwenye chumba cha mateka wa Kiisrael. Si mwanadada huyu pekee ambaye alifanya kitendo hiki cha ushujaa, lakini pia kulikuwa na mwanamama mwingine aliitwa Janet Almog (rai wa Marekani) na mateka mwingine aliyeitwa Jean-Jacques Mimouni (raia wa Ufaransa) nao kwenye kuonyesha hali ya kuwaunga mkono wenzao waliotengwa kwenye chumba kingine na kupinga ubaguzi uliokuwa unafanywa na maharamia hawa, nao walijipeleka kwa hiari yao kwenye chumba ambacho mateka hao walikibatiza jina “Chumba cha Waisrael”, ambacho mateka wote walijua fika kwamba kuna jambo baya maharamia hao walikuwa wamepanga kulifanya.

Licha ya maharamia kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kufanya uchambuzi huu wa kina kuhusu uraia wa kila mateka waliye naye, lakini walifanya kosa kubwa sana ambalo lilkuja kuwagharimu sana hapo baadae. Kwenye uchambuzi wao wote huu walioufanya walishindwa kumng’amua mateka mmoja mwanajeshi wa Israel ambaye alikuwa ana uraia pacha na siku hiyo alikuwa anatumia passport ambayo sio ya Israel. Mateka huyu alikuja kuwa muhimu sana huko mbeleni kuwapatia Mossad Intelijensia mujarabu kabisa kuhusu watekaji, jengo wanaloshikilia mateka, na namana wanavyoshirikiana na jeshi la Uganda.

Siku iliyofuata yaani June 30, maharamia haya wakawaachia mkupuo wa kwanza wa mateka wasio raia wa Israel au wayahudi. Katika mkupuo huu wa kwanza waliachia mateka 48 ambao walikuwa ni wazee, watoto na akina mama wenye watoto wadogo.

Baada ya mkupuo huu wa kwanza wa kuwaachia mateka hawa wachache, maharamia wakaweka wazi matakwa yao ili waweze kuachia mateka wengine. Kwanza kabisa walitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5. Na pili walitakakuachiwa kwa wafungwa 53 wenye asili ya kipalestina wanaotuhumiwa kwa ugaidi, ambao kati yao 40 walikuwa kwenye jela za Israel na 13 katika nchi nyingine za Ulaya. Watekaji hawa wakatoa ‘ultimutum’ kwamba kama matakwa yao hayatatekelezwa ndani ya masaa ishirini na nne yajayo (mpaka tarehe 1 July saa 8 mchana) basi wataanza kuua raia wa Israel mmoja baada ya mwingine.

Dunia nzima ni kama ilisimama kwa masaa kadhaa kutokana na sintofahamu iliyogubika kila mahali. Sintofahamu hii ililetwa na ukweli kwamba, ilikuwa inajulikana wazi kwa miaka yote kwamba Israel wana sera ya kutofanya mazungumzo au makubaliano na Magaidi. Kwahiyo kila mtu alikuwa nafahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa ndani ya masaa 24 yajayo ulimwengu ukashuhidia watu zaidi ya 200 wakichinjwa kama kuku.

View attachment 524097
Rais Idd Amin akiwa uwanja wa ndege "kuwasalimu" mateka



NCHINI ISRAEL: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI


Nchini Israel kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeitishwa na waziri Mkuu Yitzhak Rabin kujadili kuhusu hatua za kuchukua kuokoa raia wake ambao wameshikiliwa mateka huko uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda.

Hali ya kikao ilikuwa tete sana kutokana na kila dakika waliyokuwa wanaitumia kujadili ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia saa 8 mchana ya tarehe 1 July. Walipowasilana na Ujerumani na Ufaransa ambao nao walikuwa na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina ambao watekaji walitaka waachiwe… walipowaomba ushirikiano wao kuhusu kukabali kuachia hao wafungwa, Ujerumani na Ufaransa walikataa katakata kuachia hata mfungwa mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa kwenye magereza zao.

Sintofahamu ilizidi kuongezeka. Masaa yalizidi kuyoyoma. Saa 8 mchana ya tarehe 1 July ilizidi kukaribia. Harufu ya damu ilikuwa inabisha hodi mlangoni kwao. Licha ya weledi wao wote walionao lakini mbele yao waliona giza.

Inapaswa kukumbukwa kwamba Idd Amin aliwahi kupatiwa mafunzo ya weledi wa kijeshi nchini Isarel (Special Force Training). Kwa hiyo baraza la mawaziri likamuagiza Baruch Bar-Lev, kamanda mstaafu wa IDF ambaye alihusika kumpatia mafunzo ya kijeshi Amin kipindi yuko Israel na kufanikiwa kujenga naye ukaribu. Baraza la Mawaziri likamuagiza Baruck (marafiki zake humuita “Burka”) kufanya mawasiliano na Rais huyo wa Uganda ili kujaribu kumuomba awashawishi magaidi wanaoshikilia mateka kwenye uwanja wake wa ndege wa Entebbe wawaachie mateka hao bila masharti magumu.

Kupitia kwa Burka, Israel ilifikia mpaka hatua ya kumuahidi Idd Amin kuwa kama atafanikisha kuachiwa kwa mateka hao basi watatumia ushawishi walionao kuhakikisha kuwa Amin anatunukiwa tuzo ya amani ya Nobel.

Lakini Amin hakulegeza msimamo, akaendelea kuwasisitiza kuwa hakuna namna nyingine yeyote ambayo mateka hao wataachiwa bila masharti yaliyotolewa na watekaji kutimizwa.
Baada ya juhudi hii ya kumuhonga ‘tuzo’ kugonga mwamba, Waziri Mkuu wa Israel akawasiliana na serikali ya Marekani na kuwaomba wamshawishi Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alikuwa anaheshimiana sana na Amin ili amshawishi kuwaamuru magaidi yaliyoko uwanjani kwake Entebbe waachiemateka bila masharti magumu.

Amin bado akashikilia msimamo kwamba hakuna mateka atakayeachiwa pasipo masharti yaliyotolewa kutimizwa.
Juhudi hizi za kumshawishi Amin zilikula muda mwingi sana na hatimaye wakajikuta tayari kulikuwa kumekucha asubuhi. Mbele yao kulikuwa kumebakia masaa chini ya manane kabla ya damu ya zaidi ya watu 200 kumwagika.

Baraza la mawaziri la Israel likamuomba Amin aongee na watekaji wakubali kusogeza siku mbele ili kuipa serikali ya Israel muda wakutosha kushughulikia lojistiki na kushawishi Ujerumani na Ufaransa ili waweze kutimiza sharti la kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wanaotuhumiwa kwa ugaidi.

Rais Idd Amin baada ya kushawishiwa sana akakubali ombi hili na akaieleza serikali ya Israel kwamba ni siku tatu tu pekee zinaongezwa, yaani ikimaanisha kwamba siku zitaongezwa mpaka tarehe 4 July, saa 8 mchana. Serikali ya Israel ikakubliana na hili.

Mchana wa siku hiyo, serikali ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari wakilaani vitendo vya kigaidi na hususani matukio ya utekeji wa raia wasio na hatia, na pia ikaendelea kusisitiza kuhusu sera yake ya kutojadili na magaidi. Lakini taarifa hii ikamalizia kwa kueleza kuwa kwa kujali zaidi uhai wa zaidi ya raia 200 ambao bado wanashikiliwa na magaidi hayo, na kujali maumivu ambayo familia zao na taifa zima linapitia, wamekubali kutimiza sharti la magaidi hao la kuwalipa fedha za kimarekani dola milioni tano pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wenye tuhuma za ugaidi.

Ilikuwa ni moja ya matukio machache ambayo yaliishangaza dunia kwa Israel kukubali kushindwa hadharani. Kwa upande wa maadui wa Israel hii ilikuwa ni sherehe kubwa kwao. Na kwa upande wa Isarel na maswahiba zake hii iikuwa ni maombolezo makubwa.
Amin na wenzake kule Uganda walikuwa wanasherehekea baada ya taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari. Walihsi kabisa harufu ya ushindi inanukia kwenye pua zao.

Kitu ambacho walikuwa hawafahamu ilikuwa ni kwamba, Israel walikuwa wanawafanyia ‘mchezo’ wa kisaikolojia ili Amin, jeshi lake na watekaji wajiamini kwa kuona kuwa ushindi umeegemea upande wao na hatimaye wajisahau kutokana na kujiamini huku.


NYUMA YA PAZIA

Huko Tel aviv, makamanda wa IDF na maafisa wa Mossad walikuwa wamekusanyika katika conference room ya mako makuu ya wizara ya ulinzi kuweka mkakati wa oparesheni ya uokozi (rescue mission) wa mateka wanaoshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda.
Kati ya watu muhimu ambao walikuwepo kwenye kikao hiki alikuwa ni Waziri Mkuu Rabin na Ehud Barak ambaye kipindi hicho alikuwa kamanda wa ngazi za juu kwenye jeshi anayeongoza kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence).

Moja kati ya vitu muhimu ambavyo viliwasaidia ilikuwa ni taarifa ya intelijensia iliyoletwa na Mossad kwamba uwanja wa ndege wa Entebbe ulijengwa na kampuni ya Kiisrael inayoitwa Solel Boneh.

Kwahiyo muwakilishi kutoka katika kampuni hii ya ujenzi naye akaitwa kikaoni kwa ajili ya kuwasilisha michoro kuhusu jengo lote na uwanja wa ndege wa Entebbe ulivyo.
Lakini pia wakati huo huo kulikuwa na maafisa wa Mossad ambao walikuwa ufaransa kuwahoji wale mateka ambao walikuwa wameachiwa awali. Mtu muhimu zaidi ambaye alitoa taarifa nzuri kwa Mossad alikuwa ni yule afisa wa jeshi niliyemuelezea awali kwamba alikuwa na uraia wan chi mbili (Israel na Ufaransa) na siku hii alikuwa ametumia passport ya nchi ya ufaransa hivyo watekaji walimuachia pamoja na wenzake wa kundi la kwanza lile la watu 48.

Bwana huyu alitoa taarifa muhimu zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Entebbe, kwa kuwa yeye tofauti na wenzake kutokana na uzoefu wake wa jeshi alikuwa aliweza kuwaeleza Mossad kuhusu ni salaha za namna gani watekaji walikuwa nazo, kulikuwa na ndege za aina gani za kijeshi pale uwanjani (Idd Amin aliamuru Air Force ya Uganda kulinda uwanja huo masaa 24), pia aliweza kuwaeleza kuhusu ‘rotation’ ya ulinzi ya jeshi la Uganda pamoja na taarifa nyingine muhimu ambazo abiria wengine wasingeweza kuzitilia maanani au kkuzieleza kwa ufasaha.

Baada ya kupata intelijensia ya kutosha, mkakati wa awali ambao ulipendekezwa na jeshi ulikuwa ni kutumia ndege ya kijeshi na kisha kudondosha makomando kwenye ziwa Viktoria na kutoka hapo watatumia boti za mpira kuvuka mpaka nchi kavu na hatimaye kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali sana na ziwa Viktoria.

Mkakati huu ulikuwa ni mzuri lakini ulihairishwa baada ya kupewa taarifa kuwa ziwa Viktoria lilikuwa na mamba wengi na ingeweza kuhatarisha uhai wa hawa makomando kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa ndege. Kwahiyo ilikuwa dhahiri kwamba mkakati wowote ambao utawekwa ni lazima uwe wa kuvamia kutokea nchi kavu na ikiwezekana kutoka nchi jirani.

Changamoto kubwa zaidi ilikuwa ni usafiri. Yaani kwamba oparesheni hii ilikuwa si tu kwamba makomando wanaotumwa kutekeleza wanaenda kupambana na magaidi wanne tu walioteka ndege, bali ilikuwa ni kana kwamba wanaenda kupambana na jeshi zima la Uganda. Kwa hiyo kikosi cha makomando ambacho kitatumwa kwenda huko lazima kiwe na watu wengi wa kutosha na pia lazima wachukue silaha nzito za kutosha. Ili kufaniskisha safari yenye makomando wengi hivi na vifaa vizito ilikuwa ni lazima kutumia ndege kubwa za kijeshi zenye uwezo mkubwa pia na hakukuwa na chaguo zuri zaid ya kutumia ndege za kijeshi za LOCKHEED C-130 HERCULES. Sasa changamoto ilikuwa inakuja kwamba huwezi kurusha dege kubwa kama hii kwenda na kurudi kutoka Israel mpaka Uganda bila kujaza mafuta tena japo mara moja.

Katika kipindi hiki bado Israel walikuwa hawajawa na uwezo wa kufanya ‘Aerial Refuel’, yaani ndege kujazwa mafuta kwa kutumia ndege nyingine ikiwa angani. Lakini pia ilikuwa ni lazima madege hayo yakikaribia Uganda yaruke chini chini ili kukwepa kudunguliwa na kuikwepa rada ya kijeshi. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kupata nchi ndani ya afrika Mashariki ambao watakubali madege hayo ya kijeshi ya Israel kutua kwenye uwanja wake wa ndege na kujaza mafuta lakini pia kujiandaa na kuanzisha operation kutokea hapo na pia anga lao kutumika kuanzisha shambulizi la kijeshi kuelekea Uganda.

Sasa japokuwa nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa hazikubaliana na kitendo cha Rais wa Uganda kushirikiana na watekaji, lakini hakukuwa na hata nchi moja ambayo ilikuwa iko tayari kuingia kwenye mzozo na Idd Amin kwa kuruhusu viwanja vya vya ndege kutumika na ndege za jeshi la Israel au wanajeshi kujiandaa kuvamia Entebbe au pia kuruhusu anga lao kutumia na jeshi la Israel.

Ndipo hapa ambapo kwa haraka sana siku hiyo hiyo Waziri Mkuu Rabin akamtuma Ehud Barak na maafisa wachache wa Mossad kwenda Kenya kushawishi serikali ya Mzee Jomo Kenyatta iruhusu ndege za jeshi la Isarel kutumia kiwanja chao cha ndege. Ehud barak na wenzake hawakwenda tu moja kwa moja kwa Mzee Kenyatta, bali kwanza walienda kwa Waziri wa kilimo wa kipindi hicho Bw. Bruce McKenzie ambaye huyu aliwahi kuwa afisa wa Idara ya ujasusi ya Uingereza, MI6 na pia alikuwa swahiba mkubwa wa Ehud Barak.

View attachment 524098
Ehud Barak enzi za utumishi jeshini

Kwa hiyo Israel ikamtumia Bruce McKenzie kumshawishi Mzee Jomo Kenyatta kuruhusu anga la Kenya na viwanjavya ndege kutumiwa na makomando wa Israel na ndege zao.
Ehud Barak na maafisa wa Mossad hawakuishia hapa tu, bali pia walifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya wenye asili ya Israel na wale ambao walikuwa na ‘marafiki’ wa Israel kuwaomba watumie ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wasaidie kumshawishi Kenyatta kukubali ombi la seriakli ya Israael viwanja vyao kutumika na ndege za kijeshi za Israel na makondo wake.
Baada ya mashinikizo haya kutoka kila upande, Mzee Kenyatta hakuwa na chaguo linguine zaidi ya kukubali ombi lao.

Bwana huyu McKenzie pia alikuwa na ndege yakebinafsi, na Ehud Barak akaona fursa. Walitumia ndege hii ya kiraia kuruka mpaka Uganda mijini Entebbe na kukatiza juu ya anga la uwanja wa ndege wa Entebbe na walipokuwa wanapita juu ya anga la uwanja wa ndege, Ehud Barak akatumia fursa hii kupiga picha kila eneo la uwanja. Kwa kuwa hii ilikuwa ni ndege ya kiraia, jeshi la Uganda hawakushughulika nayo.
Picha hizi zilizopigwa na Ehud Barak zilikuja kuwa na umuhimumkubwa katika maandalizi ya mwisho ya oparesheni ya makomando wa Isarel Kuvamia uwanja huu.

Mpaka kufikia hapa maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika.


WAKATI HUO HUO


Upande wa watekaji kule Uganda walikuwa wanasubria mifwedha yao dola milioni 5 za kimarekani.
Rais Idd Amin naye baada ya kufikia makubaliano na Israel kuwa masharti ya fedha na wafungwa wa kipalestina kuachiwa tarehe 4 July, naye ‘akarelax’ na akaona huo ndio muda wa kutekeleza majukumu Mengine akisubiria tarehe 4 July ifike.

Katika kipindi hiki Idd amin ndiye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa uenyekiti kuzunguka kwa kila nchi kwa mwaka mmoja mmoja na wiki hii alikuwa anatakiwa kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kilichokuwa kinafanyika Mauritius. Kwa hiyo Amin akafunga safari kuelekea Mauritius kwenda kukabidhi kijiti cha Uenyekiti.

Ehud Barak aliposikia taarifa hii, kwa kutumia akili yake kubwa ya kuzaliwa aliyojaliwa na uzoefu wake wa ujasusi, aliona fursa adhimu kabisa hapa. Akawasiliana na walioko kikaoni huko Tel Aviv na kuwaeleza taarifa ambazo awali wote hawakuielewa.

Ehud Barak: “Idd Amin akiwa ndani ya Uganda huwa anatumia Mercedes Limousine katika msafara wake”

Waziri Mkuu Rabin: “Ok! Limefanyaje?’

Ehud Barak: “Nataka mtafute gari kama hiyo… Mercedes Limousine”

Waziri Mkuu Rabin: “la kazi gani?”

Ehud Barak: “siku ambayo kikosi cha makomando wakipanda kwenye ndege kutoka huko Israel kwenda Uganda, gari hilo nataka pia lipakiwe ndani ya ndge!”

Kwa dakika kadhaa wote ambao walikuwa wanamsikiliza pale kikaoni kupitia simu hakuna ambaye alielewa nini hasa Ehud Barak alikuwa anapendekeza.
Yalikuwa yamebaki masaa machache tu ambapo, weledi, ushujaa na uzalendo uliotukuka ulikuwa unaedna kudhihirika.



BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA TATU


THE BOLD - 0718 096 811 (WhatsApp tu...tafadhali usipige) hii namba maalumu kwa wale wanaotaka kujiunga na group la WhatsApp (kuna Ada)... Kwa hiyo nicheki WhatsApp tu... Usipige tafadhali
Hasa mkuu unatuachaje njiani ungemalizia tu story
 
The bold nataka kufahamu...pale waisrael walipotua ndege yao ina maana wale watekaji hawakusikia sauti ya ndege wakati inatua au?
Nimesoma mahali.. uwanja ulikua unatumika na ilikua taa zote zinazimwa na kuwashwa tu pale inapotokea ndege iliyopewa ruhusa kutua hapo. Taa zinawashwa then ndege husika ikishapita kwenye 'run way'' taa zile zinazimwa tena. Sasa hawa mabwana wa Israel walicheza na ratiba ya ndege fulani ivi nadhani ni British Airways ilikua inatua muda fulani hapo Entebe so walipowashiwa taa tu nao wa Israel wakaunga 'tela' wakatumia mwanya huo huo wa mwanga. Kwa maelezo haya nadhani hata swala la sauti ya ndege za kijeshi kusikika limejibika.
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush[/USER
Mbona mimi simo
 
OMBI: Wakuu, huu utaratibu wa kutag nafanya kazi kubwa sana lakini wengi wanalalamika kuwa sijawatag... Ishu ni kwamba notification zinasumbua kufika na ni tatizo ambalo uongozi wa JF wanashughulikia... Pia nilianza utaratibu wa kuanza na neno "The Bold: ................." Ili ukiwa unaperuzi na kukutana nao ujue kuwa ni Uzi mpya nimeweka...

Tumeshauriana na mods na kubaini kuwa utaratibu huu wa kuweka username yangu kwenye kichwa cha habari inaleta mkanganyiko wa kimantiki hasa hasa kwa watumiaji wapya wa JF.

Sasa basi, nawashauri kufanya moja ya yafiatayo ili kupata notification zangu kwa urahisi zaidi.

1. Hakikisha umenifollow

2. Subscribe kwenye uzi

Hii nadhani itakuwa rahisi zadi kuliko hii kazi kubwa ya kutag watu alafu hawapati notification.


Shukrani.







OPERATION ENTEBBE







Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini…



Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U.



Tuendelee…







SEHEMU TA NNE





Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio.



Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini.



Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi.



Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’.



Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal.



Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo.



Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake).



Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka.

Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa.



Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka.

Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”.


Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi.



Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi.



Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni.

Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo.



Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”).



Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege.



Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale.



Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia.



Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi.

Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo.



Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka.



Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja.

Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari.



Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda.



Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi).



Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.!



Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’.





Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”!



Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya.



Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa.





Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi.

McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake.



Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya.
[6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake.



Je kuna uhusiano wowote wa matukio haya mawili?? Operation Entebbe na Vita ya Kagera?? Jibu la haraka ambalo wengi watalitoa ni kwamba hakuna uhusiano wowote ule…

Lakini nashauri uhifadhi jibu lako kwa sasa, tukijaaliwa siku moja tutachambua kwa umaridadi kabisa, hatua kwa hatua, vita ya Kagera na yaliyo nyuma ya pazia kwa miaka mingi bila kusemwa.







Muwe na usiku mwema wakuu,




Tumemaliza kuchambua Oparesheni hii ya kwanza. Bado nyingine nne.

Siku ya Alhamisi nitaweka Oparesheni ya Pili.





THE BOLD - 0 718 096 811 (Namba hii ni kwa wale ambao wanataka kujiunga na group la WhatsApp ambalo naweka makala na simulizi kila siku... Usipige tafadhali
 
Back
Top Bottom