Onyo: Mnaonunua samaki wa kukaanga Ubungo, nunueni vibua tu

Utakuwa umefungua genge la kukaanga vibua hapo Ubungo wewe sio bure
Hahaaa vibuaa wengi wanawaleta fresh NA unaona wanawekwa KWA moto Mpwa hao unakuta wamekaangwa kabisaa NA ukichukuanwengi wanajifanya kufurahia kumbe wanakucheka
 
Picha ingekuw
Wapo wapenzi wanaopenda sana hizi Samaki za hawa wamama kwenye kona,binafsi hupenda kuchukua vibua sababu wanakuwa wametoka kwenye moto.

Hawa sangara vipande msirogwe mkachukua. Wifi/shemeji yenu katoka kununua wa elfu 15, hapa kila kipande ndani kinatoa funza wa haja. Hakuna kilicho salama hata kimoja, na hii ni baada ya kuniambia nikamwambia zipasue kwanza, vipi wale mnaopika moja kwa moja.

Naona paka wangu walifanya maombi vilivyo leo, ngoja niwasongee na ugali kabisaa loh.

Wale wenye panya nao ni vipande vizuri kwa mitegoo, panya wengi hufa kwa kula hawa samaki.

Picha ingekuwa kielelezo kizuri sana kwa akina Tomaso
 
Kwa nini msinunue fresh kutoka katika maduka yanayouza??
Madukani sio fresh afadhali umwambie weekend aende feri au bagamoyo anunue fresh atengeneze mwenyewe na kuwaifadhi kwa kitoweo.Kumbuka pia siku hizi kuna sato na kibua wakutoka nje samaki haramu nje nje kwa solo hata muzaji aonji sembuse kkula.
 
Wapo wapenzi wanaopenda sana hizi Samaki za hawa wamama kwenye kona,binafsi hupenda kuchukua vibua sababu wanakuwa wametoka kwenye moto.

Hawa sangara vipande msirogwe mkachukua. Wifi/shemeji yenu katoka kununua wa elfu 15, hapa kila kipande ndani kinatoa funza wa haja. Hakuna kilicho salama hata kimoja, na hii ni baada ya kuniambia nikamwambia zipasue kwanza, vipi wale mnaopika moja kwa moja.

Naona paka wangu walifanya maombi vilivyo leo, ngoja niwasongee na ugali kabisaa loh.

Wale wenye panya nao ni vipande vizuri kwa mitegoo, panya wengi hufa kwa kula hawa samaki.
Pole nasikia wanaweka vikolimbwezo kama limau ndimu kitunguu swaumu mdalasini na tende then wanachovya huko ndio wanaweka kwenye mafuta,wakitoka wanakuwa na mvuto balaa jioni ukitoka kazini wanakuuzia wewe ukijua in fresh kumbe niyale yalioza wameuziwa bei rahisi wakayaboresha.
 
Ilishanikumba hiyo wakati nasoma dar, nilikuwa nawashikaji geto nilivyoingia tu ndani na hao samaki ubungo washikaji wakaanza kunilaumu nimejamba tulibishana nilipofungua kuwaandaa ndio ikabainika. Sio wote huwa wamechina lakini
 
Ustaarabu hatuna unauzaje kitu kilichooza? Hata pale nangurukulu njian km unaenda lindi samaki wao wameoza
 
Hakika shibe mwanamalevya kuna wenzenu walishasahau habari ya samaki na nyama ni mwendo wa dagaa na mboga za majani. Nyie mnawachunguza hadi ndani kama wana funza!!!
 
mimi hayo hayanigusi nakula samaki wa kuchemsha mnoooo sijui nimekula wa kukaanga lini? kuna member huku alinishauri nile sato wa kuchemsha wanaongeza makalio sasa imekuwa dozi huu ni mwezi wa sita sasa kiukweli naona kama kuna kachanges ha ha haha
 
Back
Top Bottom