Inasikitisha na kuleta mkanganyiko katika jamii. Nachelea kusema kwamba nchi hii inahitaji ushauri wakisomi wakizalendo na unoatoa haki kwa wananchi. Hapana wananchi hawatendewi haki na uongozi wa awamu hii.
Ni mshauri gani anaishauri serikali kusitisha utoaji ajira za serikali kwenye nchi masikini kama hii ambayo ajira za serikali ndio moyo wa ajira na uchumi? Mwenzetu huyu alisoma vitabu gani?
Ni msahauri gani anaishauri serikali kubuni aina mbalimbali za kodi zisizowiana na gawio la ongezeko la uzalishaji? Sekta ya huduma binafsi katika nchi masikini ni dhahifu mno na inastahili jitihada za serikali kuikuza! kadhalika sekta binafsi, ni changa mno kwetu. Kwa hali hii kodi stahiki ni kodi zinazotokana na ongezeko la uzalishaji au mwendelezo wa uzalishaji. Sasa leo hii mfanyabiashara mdogo anayelipa wafanyakazi wake kwa m-pesa au anayeweka kiasi chake bank na kukitumia kwa matumizi ya kila siku anabuniwa kodi; kwa uzalishaji gani anaoufanya?
Sasa ajabu wapo wanaotutaka tusilalamikie uwingi wa kodi. Wanasahau kwamba malalamiko yetu ni matokeo ya lundikano la sera zinazoumiza. Sio kodi tu bali kodi hizi zinapoleta madhara katika sekta ya utalii, uwekezaji, microeconomic activities, telecommunications, banking industry, transportation, etc madhara yake ni makubwa kuliko kiasi cha ela kinachokusanywa na serikali kutoka kwenye kodi hizi.
Ni Tanzanian tu, narudia Tanzania tu, ndiko uongozi wa nchi unapimwa kwa ukali wake katika kukusanya kodi. Kadhalika ni wachumi wa Tanzania wa awamu hii ndio wanaodhani nchi inaendelea kwa ukali na utitili wa kodi. Nchi zilizoendelea hazikeshi mezani kubuni aina mbalimbali za kodi, sio kwasababu wananchi wake watiifu katika kulipa bali viongozi wa nchi hizo wanajuwa madhara ya kodi katika uchumi. Kodi kama chumvi kwenye mchuzi, ukiweka sana huwezi kula na ukila kiasi hiko hiko miaka nenda rudi bila kupunguza jiandae kwenda hospitali kwa high blood pressure!
Aisha uongozi huu unakosa washauri wa kiuchuni au washauri wake bado hawana ukomavu katika fani mzima ya economic development na development economics. Uchumi wa taifa tulioujenga miaka kadhaa leo unaangamia at a supersonic speed!