Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,669
- 8,265
Na Thadei Ole Mushi.
Inahitaji utulivu na kufikiri nje ya Box...
Jana nimehoji hapa inakuwaje nchi ndogo kama Burundi yenye KM za mraba ambazo hazifiki hata nusu ya KM za mraba za Tabora na nchi yenye watu wachache hivyo kutuuzia experts kwenye eneo la Makocha wanaokuja kutufundishia timu zetu.
Watu wachache akiwemo Mfadhili wa Coastal Union Maestro Nassor Binslum waliingia mkenge na kusema mbona China na India hawana makocha pamoja na ukubwa wa Eneo na population yao kuwa kubwa? Hivi ndivyo walivyojustify hoja zao. Wengine waliishia kutukana tu bila kujibu kwa hoja.
Ndugu zangu tukubaliane si sawa kwa population yetu kubwa namna hii kuuziwa utaalamu na nchi kama Burundi. Kwa ukubwa wetu tunatakiwa tuwe na uwezo wa Kuzalisha wataalamu wenye ubora kila eneo. Population yetu inaruhusu kufanya hivyo na sisi ndio tulipaswa kuwa wauzaji wa wataalamu kwa ndugu zetu wanaotuzunguka. Katika hili kuna mahali tumekosea tunapaswa kupa rekebisha mapema sana.
Si sawa kusema tuna tatizo la Ajira huku tukiachia fursa kama hizi zikichukuliwa na Wageni. Ninachokiona kwenye Football ndicho hicho hicho ninakiona kwenye maeneo mengine. Mfano pitieni kwenye mashamba ya makubwa ya Kahawa ukanda wa Kaskazini mikoa ya KLM, Manyara, Arusha na Tanga. Mameneja wa mashamba hayo wanatoka Kenya karibia asilimia 95 huku maprofesa wetu pale SUA wakikimbizana na Panya wa APOPO. Huku Graduate wetu wa Pale SUA wakigombania abiria wa Boda boda na wa Std Seven vijiweni na maeneo mengine hali ni hiyo hiyo fursa bado zinachukuliwa na wageni.
Narudia population yetu inaruhusu kuuza madaktari, Mainjinia, Makocha, Na wataalamu wa fani nyingine nje ya nchi. Tukifanya hivi ndivyo tutakavyopunguza tatizo la Ajira na kupata wazawa kurudi ku invest nchini mwetu na kundi kubwa sana kuendelea kufaidi.
Kusema mbona China na India hawana makocha ni kufikiri kwenye uoni wa Pua. Yaani wao wakikosea basi inajustfy na sisi tukosee. Tukilinganisha vitu hivi hatutakaa tusogee. Lazima hili eneo tulirekebishe kama tunataka nchi isonge mbele kwa kila nyanja. Makosa ya wengine hayatumiki kuhalalisha kufanya makosa.
Kwa nn nilimtolea Matola mfano?
Ukiniambia katika vijana walimu wa mpira nchini wenye uwezo na Uzoefu mkubwa basi mimi kwa mtizamo wangu kwa sasa nitamtaja Matola. Jamaa anajua na lazima tukubali kuwa anajua ndio maana makocha pale Simba wanakuja na kumuacha na pindi anapoachwa mwenyewe pale Simba Timu inafanya vizuri sana.
Kuna watu hawajui kuwa pamoja na uwezo wake huo hana leseni inayomfanya akubaliwe kufundisha timu ya Ligi kuu. Kitendo hiki kinamnyima fursa ya kuwa kocha mkuu wa club. Huenda angekuwa na Leseni na kuifundisha timu kama Simba kama Kocha mkuu huenda alishachukuliwa nje ya nchi S.A au hata Misri na Moroco.
Tunavyozungumza sasa hivi hakuna Kocha hata mmoja wa Tanzania anayefundisha nje ya nchi. Kinachoendelea kwa sasa wanapukutika tu kwenye ligi ya ndani na hakuna Generation inayokuja kuwarithi. Kwa jinsi mambo yanavyokwenda ipo siku makocha wote wa Ligi kuu watakuwa wanatokea nje ya nchi. Huu ni udhaifu mkubwa lazima usemwe tusiogope kuusema ili wenye mamlaka waliangalie kwa jicho la kipekee.
Kwa Uwezo wa Matola hatuna hata haja ya kutafuta kocha mkuu wa Taifa Stars huyu anajua watanzania na kacheza soka la Tanzania na Africa tungesogea sana.... Ukisema hivi utasikia wewe baki kwenye siasa bila kujua kwenye Mpira ndiko kwenye Siasa kubwa zaidi. Nimeandika na nitaandika tena kuhusu soka njooni mniue
I stand to be corrected.
CC. Mh Mohammed Mchengerwa Mbunge