Ofisi ya Mbunge Muleba Kusini wajichukulia fedha za mikopo ya halmashauri ya vijana kwa njia zisizo halali

Mchumba

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
280
262
Vijana wa jumuiya ya CCM wilaya ya Muleba tuliungana kwa pamoja na kusajili kikundi cha Umoja wa Vijana wa CCM Muleba kikiwa chini ya viongozi wa chama ambapo ni katibu wa vijana na Mkiti wa vijana Jumuiya ya CCM Muleba. Kikundi hicho kilipata leseni yake mnamo tarehe 23/07/2022. Leseni hiyo ilitolewa na Halmashauri kwa ajili ya kutambua kikundi hicho kuwa kinajihusisha na ufyatuaji wa matofali.

Ndugu Adelius Apolinary ambaye ndio Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini lililopo chini ya Mh Dr Oscar Kikoyo CCM. Vijana wa umoja wa CCM kwa ujumla tulimuomba kama katibuwa mbunge na msomi wa taaluma ya Sheria atusaidie namna ya kufuata utaratibu mzuri wa kuomba mikopo inayotolewa na Halmashauri isiyo kuwa na riba. Mbunge alitoa kibali hicho kwa msaidizi wake ili aweze kusaidiana na sisi tupate mkopo kiurahisi kwa kufuata sheria zote zinazokidhi hadi kupewa mkopo huo.

Ndugu Adelius alienda kinyume na makubaliano ya kikundi akatumia mwanya huo wa kuaminiwa kutokana na kuhudumu kwenye ofisi ya Mbunge kama katibu wake. Alishawishi baadhi ya watumishi wa serikali wakamsaidia kwa uharaka. Kile kikundi tulikuwa tayari tumeishaandaa na signatories yeye akaenda benki akafoji saini zao na kubadilisha namba za simu ili aweze kuchukua mkopo pasipo sisi kujua. Hata documents zote zipo benki ya CRDB na signatories wote wanaonekana.

Huyu Adelius Katibu wa Mbunge akaamua kubadilisha jina la kikundi lakini kwa kutumia mikataba ile ile ya kikundi chetu cha vijana na huku akiweka signatories wa kwake ambao hata akitoa hela hawatauliza zinaenda wapi. Adelius akafanikisha kujichukulia mkopo wa Tshs 60,000,000.00/= (milioni 60) kwa njia za udanganyifu na kisha kuanza kutumia hela hizo kujinunulia gari la kutembelea pamoja na gari chakavu aina ya Canter kwa ajili ya kufanya shughuli za ufyatuaji matofali. Huu ndio mradi ambao tuliuasisi sisi vijana yeye akatumia ofisi ya mbunge kutugeuka.

Baada ya kuchukua hela hizo za mkopo alianza kututishia baadhi ya vijana kwamba hatuhusiki na hizo hela na kijana atakayejifanya kufuatilia hizo hela atafungwa kwa sababu ni mpango wa mbunge. Sis Vijana baada ya vile vitisho na kuogopa usalama wetu tukaanza kuwaambia baadhi ya watu ambao wakasaidia kupiga kelele mtaani na sehemu nyingine.

Baada ya suala hili kuanza kusambaa sana. Ofisi ya vijana wa CCM Mkoa waliingilia kati na kumuita mhusika Adelius katibu wa Mbunge kujitetea juu ya suala la kufanya dhuluma. Adelius alikubali kurudisha hela lakini ameendelea kujinasibu kwamba yeye ni mwanasheria na bosi wake ni mwanasheria ambaye ni mbunge anasema hicho kikundi ni mali zao na hakuna hata hela ambayo itarudi.
Tayari ofisi ya vijana wa CCM Mkoa nao wameishatishwa kufuatilia hilo suala kutokana na kuogopa huyo Kigogo ambaye yuko nyuma ya sakata hili.

Tunaomba Katibu Mkuu wa Chama Mh Daniel Chongolo atusaidie vijana wapate haki yao. Wakati Katibu Mkuu alipokuja kwenye ziara wilayani Muleba alifurahishwa na namna vijana wa CCM ambavyo tulijitolea kuweka kambi za matofali na matofali hayo yalisaidia kujenga shule na zahanati nyingi ndani ya Muleba. Kwa kauli yake aliomba vijana tushikwe mkono na serikali ili tupatiwe mkopo ambao utatusaidia kuendesga maisha yetu maana vijana wengi hatuna ajira ambazo ni rasmi. Ofisi ya Mbunge imefanya kitendo cha kutuumiza vijana, vijana wanakosa imani na Mbunge wao pia Chama ambacho wanakipigania usiku na mchana wanatokea watu kwa ulafi wao na tamaa zao wanatudhulumu haki yetu. Katibu Mkuu tusaidie Muleba vijana tunanyanganywa haki yetu. Ushahidi wote upo mje mtushike mkono sisi ni vijana wenu

Tunaomba Serikali ituhakikishie vijana usalama wetu ambao tunatetea haki ya kupata stahiki ya mkopo wetu ambao tuliomba au wapewe onyo haraka waache kututishia. Maana katibu wa mbunge anatutisha vijana ambao tumekua mstari wa mbele kudai haki yetu.

Tunaomba chama chetu mtusaidie viongozi wetu wa huku ngazi ya wilaya wamekalia kimya na wao wanashindwa kuingilia kati kwa kuogopa ofisi ya mbunge.

Tunaomba msaada wenu tunateseka kwenye nchi yetu. Tuna imani sana na Rais wetu Mh Samia Suluhu Hassan na tuko naye bega kwa bega kwenye kuchapa kazi lakini kuna watendaji wachache ambao ndio wanaenda kinyume na matakwa ya Rais wetu. Kidumu chama tawala.

Asante sana.
 
Acha Mvua inyeshe ili tuone panapovuja.

Mama alisema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Poleni sana vijana.

Muleba naijua vizuri na namjua vizuri hiyo mbunge anamiliki shule ya sekondari kama unaenda nshamba siyo!?

Sasa basi

Niko hapa Muleba kwenye kagorofa hapa wanapoziba pancha, Nina Toyota Hilux nyeusi kama utaweza njoo na vielelezo haraka nitakusaidia.

Wahi mm nitampigia Moja kwa Moja huyo mbunge na mtapata Haki yenu.
 
Vijana jasho lao watapata lakini mambo mengine umeongeza chumvi.
Huyu katibu anaitwa Delly inabidi awajibishwe kwa kosa lake.
 
Kwa taarifa zilivyo...
Katibu wa Mbunge aliwaondoa watia Saini wote halali akamuweka mke wake. Akadraw Hela yote na akamfungulia duka la nguo. Alinunua Gari aina ya Fuso na gari husika kumbe lilikua na deni baada ya kubanwa akaliuza akaamua kununua gari la kutembelea.
Mbunge wa Muleba Kusini alipiga sana sana simu akiwatisha Vijana a wasidai haki Yao
Kila mtu Muleba kuanzia DED Afisa Maendeleo wote wanajua hii issue.
Huyu Deli inaonekana ana watu wengi nyuma yake ndio maana ana huo ujasiri
 
Tupe namba ya kijana mmoja kati yao
 
Vijana wa jumuiya ya CCM wilaya ya Muleba tuliungana kwa pamoja na kusajili kikundi cha Umoja wa Vijana wa CCM Muleba kikiwa chini ya viongozi wa chama ambapo ni katibu wa vijana na Mkiti wa vijana Jumuiya ya CCM Muleba. Kikundi hicho kilipata leseni yake mnamo tarehe 23/07/2022. Leseni hiyo ilitolewa na Halmashauri kwa ajili ya kutambua kikundi hicho kuwa kinajihusisha na ufyatuaji wa matofali.

Ndugu Adelius Apolinary ambaye ndio Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini lililopo chini ya Mh Dr Oscar Kikoyo CCM. Vijana wa umoja wa CCM kwa ujumla tulimuomba kama katibuwa mbunge na msomi wa taaluma ya Sheria atusaidie namna ya kufuata utaratibu mzuri wa kuomba mikopo inayotolewa na Halmashauri isiyo kuwa na riba. Mbunge alitoa kibali hicho kwa msaidizi wake ili aweze kusaidiana na sisi tupate mkopo kiurahisi kwa kufuata sheria zote zinazokidhi hadi kupewa mkopo huo.

Ndugu Adelius alienda kinyume na makubaliano ya kikundi akatumia mwanya huo wa kuaminiwa kutokana na kuhudumu kwenye ofisi ya Mbunge kama katibu wake. Alishawishi baadhi ya watumishi wa serikali wakamsaidia kwa uharaka. Kile kikundi tulikuwa tayari tumeishaandaa na signatories yeye akaenda benki akafoji saini zao na kubadilisha namba za simu ili aweze kuchukua mkopo pasipo sisi kujua. Hata documents zote zipo benki ya CRDB na signatories wote wanaonekana.

Huyu Adelius Katibu wa Mbunge akaamua kubadilisha jina la kikundi lakini kwa kutumia mikataba ile ile ya kikundi chetu cha vijana na huku akiweka signatories wa kwake ambao hata akitoa hela hawatauliza zinaenda wapi. Adelius akafanikisha kujichukulia mkopo wa Tshs 60,000,000.00/= (milioni 60) kwa njia za udanganyifu na kisha kuanza kutumia hela hizo kujinunulia gari la kutembelea pamoja na gari chakavu aina ya Canter kwa ajili ya kufanya shughuli za ufyatuaji matofali. Huu ndio mradi ambao tuliuasisi sisi vijana yeye akatumia ofisi ya mbunge kutugeuka.

Baada ya kuchukua hela hizo za mkopo alianza kututishia baadhi ya vijana kwamba hatuhusiki na hizo hela na kijana atakayejifanya kufuatilia hizo hela atafungwa kwa sababu ni mpango wa mbunge. Sis Vijana baada ya vile vitisho na kuogopa usalama wetu tukaanza kuwaambia baadhi ya watu ambao wakasaidia kupiga kelele mtaani na sehemu nyingine.

Baada ya suala hili kuanza kusambaa sana. Ofisi ya vijana wa CCM Mkoa waliingilia kati na kumuita mhusika Adelius katibu wa Mbunge kujitetea juu ya suala la kufanya dhuluma. Adelius alikubali kurudisha hela lakini ameendelea kujinasibu kwamba yeye ni mwanasheria na bosi wake ni mwanasheria ambaye ni mbunge anasema hicho kikundi ni mali zao na hakuna hata hela ambayo itarudi.
Tayari ofisi ya vijana wa CCM Mkoa nao wameishatishwa kufuatilia hilo suala kutokana na kuogopa huyo Kigogo ambaye yuko nyuma ya sakata hili.

Tunaomba Katibu Mkuu wa Chama Mh Daniel Chongolo atusaidie vijana wapate haki yao. Wakati Katibu Mkuu alipokuja kwenye ziara wilayani Muleba alifurahishwa na namna vijana wa CCM ambavyo tulijitolea kuweka kambi za matofali na matofali hayo yalisaidia kujenga shule na zahanati nyingi ndani ya Muleba. Kwa kauli yake aliomba vijana tushikwe mkono na serikali ili tupatiwe mkopo ambao utatusaidia kuendesga maisha yetu maana vijana wengi hatuna ajira ambazo ni rasmi. Ofisi ya Mbunge imefanya kitendo cha kutuumiza vijana, vijana wanakosa imani na Mbunge wao pia Chama ambacho wanakipigania usiku na mchana wanatokea watu kwa ulafi wao na tamaa zao wanatudhulumu haki yetu. Katibu Mkuu tusaidie Muleba vijana tunanyanganywa haki yetu. Ushahidi wote upo mje mtushike mkono sisi ni vijana wenu

Tunaomba Serikali ituhakikishie vijana usalama wetu ambao tunatetea haki ya kupata stahiki ya mkopo wetu ambao tuliomba au wapewe onyo haraka waache kututishia. Maana katibu wa mbunge anatutisha vijana ambao tumekua mstari wa mbele kudai haki yetu.

Tunaomba chama chetu mtusaidie viongozi wetu wa huku ngazi ya wilaya wamekalia kimya na wao wanashindwa kuingilia kati kwa kuogopa ofisi ya mbunge.

Tunaomba msaada wenu tunateseka kwenye nchi yetu. Tuna imani sana na Rais wetu Mh Samia Suluhu Hassan na tuko naye bega kwa bega kwenye kuchapa kazi lakini kuna watendaji wachache ambao ndio wanaenda kinyume na matakwa ya Rais wetu. Kidumu chama tawala.

Asante sana.
Hiyo ndio kazi ya ccm pia na nyiyi watu wa mreba tangu mfumo wa viama vingi uludi 1994 alikataa upinzani hiyo ndio dawa yenu na bado mtakomeshwa sana safina mbunge komesha wajinga hao
 
Poleni sana vijana.

Muleba naijua vizuri na namjua vizuri hiyo mbunge anamiliki shule ya sekondari kama unaenda nshamba siyo!?

Sasa basi

Niko hapa Muleba kwenye kagorofa hapa wanapoziba pancha, Nina Toyota Hilux nyeusi kama utaweza njoo na vielelezo haraka nitakusaidia.

Wahi mm nitampigia Moja kwa Moja huyo mbunge na mtapata Haki yenu.
Sio kweli
 
Kwahiyo jamaaa kawapiga milioo 60,sema nchi hii bwana na ww ukipata wajinga wako wapige tu,utajieleza mbele,katibu wa mbunge siyo ajira rasmi uchawa tu!!anyway tutapiga kelel
 
KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA YA MULEBA, MKOANI KAGERA
Leo tarehe 3/10/2023 katika Mahakama ya Wilaya Muleba mbele ya Mh Lilian Mwambeleko, imeamriwa kesi ya Jinai namba 91/2023 Jamhuri dhidi ya Adilelius Vedasto Apolinary mwenyekiti wa kikundi cha ujasiliamali cha Umoja wa Vijana Youth Fund cha Muleba pia ni Katibu wa Mbunge, ambapo alishitakiwa kwa kosa la kutoa taarifa za uwongo kwa Mkurugenzi kuhusu matumizi ya fedha za uwezeshaji vijana Milioni sitini, zilizotolewa na Halmashauri ya Muleba mwaka 2022. Kinyume na kif cha 122 cha Kanuni za Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2022, Kesi iliongozwa na Wakili Kelvin Murusuri

Mtuhumiwa ametiwa Hatiani na kuamriwa alipe faini ya Tsh. Laki tano 500,000/- au jela miezi sita
Pia kufuatia maombi ya Wakili Murusuri mtuhumiwa ameamriwa arejeshe fedha zote Milioni Sitini ndani ya miezi mitatu na tayari amelipa Milioni Tisa katika akaunti ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Muleba, na amelipa faini na kuachiwa.
 
Back
Top Bottom