Nywele zawaponza walimu

Livejr

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
2,070
2,794
Nywele zawaponza walimu wa shule ya Msingi…!

Kuna jambo limetokea la kishirikina kijiji cha Mongomongo, kata ya Navanga, Wilaya ya Lindi mkoani Lindi. Jambo hili limehusisha wanafunzi wa shule ya msingi Mongomongo walimu wao watatu wa kiume pamoja na wazazi wa hao watoto.

Ilikuwa siku ya Jumatatu ambayo mwanzo wa wiki na mara nyingi watoto wanakuwa smart kuliko siku zote za wiki na ndio siku ambayo ukaguzi wa mazingira na usafi wa wanafunzi unaangaliwa zaidi kuliko siku zingine tena huku vijijini inawezekana ndo siku ambayo vipindi vinachelewa kuanza kutokana na kufanyika kwa shughuli nyingi.

Kwa bahati mzuri ulifanyika ukaguzi wa usafi kwa wanafunzi wote ukihusisha walimu watatu wa kiume kati ya watano waliopo shuleni hapo. Baada ya kufanyika kwa ukaguzi huo kuna baadhi ya wanafunzi kama tisa (9) hivi walikuwa na nywele ndefu, chafu na hawakuchana ndipo walipopewa onyo wakazinyoe wakisharudi nyumbani jioni.

Jambo la kushangaza siku ya pili yake walirudi wakiwa hawajanyoa zile nywele ndipo walimu wakiongozwa na mwalimu ONGO walipowatoa mstarini na kuwauliza kwa nini hawajakata nywele wakajibu wazazi wao hawana pesa, ndipo walimu hao walipoamua kupitisha mkasi vichwani mwao ili wakirudi wakanyoe na hali hii inatokea sana mashuleni huku vijijini.

Hapo ndipo lilipoanza zogo kwani wazazi wa watoto wale nane walikuja shuleni siku iliyofuata na kudai wapewe “Nywele” za watoto na kutoa siku tatu kwa walimu hao warudishe nywele wasiporudisha watakiona cha moto (watawaroga). Ila wale walimu walipuuzia baada ya siku tatu kupita wale wazazi walirudi tena shuleni kuchukua nywele za watoto wao lakini hawakupewa.

Siku ya Jumapili ilipofika ya wiki ile ile ndipo mwalimu ONGO alipoamka na kukuta kichwani mwake amewekwa mashilingi (amenyolewa) kama muundo wa mapunye sijajua huko kwenu inaitwaje. Wiki ya pili sasa hiv Yule mwalimu hajaota nywele kwenye sehemu alizonyolewa baada ya wiki moja akahamishiwa Rondo na wale waliobakiwa wawili wakiwa bado wanaendelea na majukumu yao mmoja alisafiri kikazi akabaki mmoja ndipo na yeye alijikuta yupo juu ya mti maeneo ya shuleni asubuhi akiwa uchi wa mnyama Yule mwingine ambaye amesafiri kikazi mpaka leo hajarudi shuleni kuendelea na majukumu yake.
 

What is so special with ONGO naona ndiye pekee katajwa kwa jina na ameandikwa kwa herufi kubwa tupu japo kuna wenzake wengine kadhaa hawajatajwa au wao ni nameless
 
Hao wazazi ni wajanja sana maana sasa baada ya walimu hao kuondoka watoto wao watakuwa wasafi na watafaulu sana masomo yao.
 
What is so special with ONGO naona ndiye pekee katajwa kwa jina na ameandikwa kwa herufi kubwa tupu japo kuna wenzake wengine kadhaa hawajatajwa au wao ni nameless
Hao wengine nimewasahau tu ndg na huyo jamaa nlishawahi kufanya nae kazi ndo aliniambia hilo suala pia niiwasiliana na MEK wao Mr. Yasini alinithibitishia hilo tukio.
 
nilisha soma shule moja ya sekondari wilayani mpanda yaani shule ilikuwa na wanafunzi washirikina kibao,kunajamaa mmoja yeye ikikaribia mitihani ana omba ruhusa akirudi full chale na hilizi,kwenye mtihani anapiga chabo za live na hakamatwi lakini sasa matokeo yake utacheka,sikuwahi kumuona amepata walau c paper nayo ikumbuka alio fanya vimbwanga ili kuwa la history lakini aliambulia 32%
 
Alafu kesho wataenda kwa magufuli ooh Rais tunaomba msaada.. N..y..c..c..c..c ! Watabaki maskini hao wazazi kufa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…