Njombe: Katekista wa Kanisa Katoliki apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kubaka

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,902
19,093
Njombe, katekista wa kanisa katoliki apandishwa kizimbani kwa kumbaka binti wa miaka 17 nyuma ya jengo la kanisa.

=======

Simon Njavike (43) ambaye ni Katekista wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Mlangali Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya hiyo akituhumiwa kwa kosa la kumbaka Mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 17.

Mwendesha mashtaka Angelo Marco mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Ludewa Isaac Ayengo amesema Mshtakiwa Simon Njavike ambaye ni Mwalimu wa Watoto wa kipaimara akiwemo Binti huyo amekuwa akifanya vizuri katika mafunzo yake ya Kipaimara hivyo katekista alimpa Tsh. 10,000 kama zawadi ya kufanya vizuri kwenye mafunzo hayo.

Baada ya siku kadhaa Mshtakiwa alianza kumtaka kimapenzi lakini Binti huyo alikataa ndipo akaanza kudai kurudishiwa TSh. 10,000 yake aliyokuwa amempa lakini Binti alishindwa kuirudisha kutokana na kutokuwa nayo.

Ameeleza kuwa baada ya siku kadhaa Mtuhumiwa alimuita Binti nyuma ya kanisa majira ya mchana ambako kuna msitu na binti alipofika akamkamata kwa nguvu na kuingia nae katika msitu kisha akatimiza lengo lake na kutokomea kusiko julikana.

Polisi walifanya jitihada za kumtafuta na baada ya siku kadhaa alikamatwa na kufikishwa Mahakamani ambapo amekana shitaka hilo na kupelekea kesi hiyo kuahirishwa mpaka February 09 mwaka huu.

Millard Ayo TV
 
Mabinti waelimishwe kutomumini mtu yeyote hasa kuhusu mwili wake,miaka 17 alitakiwa awe na tahadhari kabisa hasa baada ya kujua lengo la Katekista mapema,asingekubali kuitwa msituni
 
Huyu anaruhusiwa kuowa katekista?
Katekista nineno la kilatini lenye maana ya mwalimu wa kanisa na kitabu anachotumia kufundishia kinaitwa Katekisimu maana yake kitabu Cha mafundisho ya kanisa, katekista anaruhusiwa kuoa ni mlei au muumini aliyepewa mafundisho ya Kanisa na maranyingi anakuwa kama msaidizi wa paroko parokiani kiufupi katekista ni mwalimu wa kanisa
 
Njombe, katekista wa kanisa katoliki apandishwa kizimbani kwa kumbaka binti wa miaka 17 nyuma ya jengo la kanisa.

=======

Simon Njavike (43) ambaye ni Katekista wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Mlangali Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya hiyo akituhumiwa kwa kosa la kumbaka Mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 17.

Mwendesha mashtaka Angelo Marco mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Ludewa Isaac Ayengo amesema Mshtakiwa Simon Njavike ambaye ni Mwalimu wa Watoto wa kipaimara akiwemo Binti huyo amekuwa akifanya vizuri katika mafunzo yake ya Kipaimara hivyo katekista alimpa Tsh. 10,000 kama zawadi ya kufanya vizuri kwenye mafunzo hayo.

Baada ya siku kadhaa Mshtakiwa alianza kumtaka kimapenzi lakini Binti huyo alikataa ndipo akaanza kudai kurudishiwa TSh. 10,000 yake aliyokuwa amempa lakini Binti alishindwa kuirudisha kutokana na kutokuwa nayo.

Ameeleza kuwa baada ya siku kadhaa Mtuhumiwa alimuita Binti nyuma ya kanisa majira ya mchana ambako kuna msitu na binti alipofika akamkamata kwa nguvu na kuingia nae katika msitu kisha akatimiza lengo lake na kutokomea kusiko julikana.

Polisi walifanya jitihada za kumtafuta na baada ya siku kadhaa alikamatwa na kufikishwa Mahakamani ambapo amekana shitaka hilo na kupelekea kesi hiyo kuahirishwa mpaka February 09 mwaka huu.

Millard Ayo TV
hapo afungwi mtu hiyo kesi atayayuka kama balafu chezea kania la roma wewe
 
Back
Top Bottom