tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,539
- 21,566
Ukipita katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na katika miji mingine mikubwa, aghalabu utawakuta vijana na baadhi ya watu wazima wamekaa katika makundi wakivuta bangi na kutumia dawa nyingine za kulevya bila wasiwasi wowote. Hili hutokea zaidi nyakati za jioni na usiku lakini pia sio ajabu kuyakuta makundi ya namna hii yamechanua nyakati za asubuhi au mchana. Ifikapo jioni hewa ya vichochoro na vijiwe vya wavuta bangi hujaa harufu ya bangi. Watoto wanaocheza mitaani pamoja na wapita njia wengine hujikuta wakivutishwa bangi kwa lazima bila ridhaa yao kwani hewa inakuwa imejaa moshi na harufu kali itokanayo na moshi wa bangi, hivyo kujikuta wakivuta hewa ya bangi bila ridhaa yao!
Genge la vijana wakivuta bangi kwenye kijiwe chao maarufu cha kuvutia bangi
Chanzo: mtandao
Tatizo la uvutaji bangi kwa vijana wa rika mbalimbali limekuwa kama fasheni. Vijana wa kada zote—waliopo shuleni na mitaani—wamejikuta wakitumbukia kwenye ulevi huu wenye madhara makubwa kiafya. Na kibaya zaidi, jamii nayo imeacha vitendo hivi viendelee huku madhara yake yakiwa yanafahamika hata kwa viongozi wa mitaa wanakoketi wahalifu hawa.
Matumizi ya bangi na dawa za kulevya hupunguza nguvukazi, kuchochea uhalifu na kupunguza uzalishaji mali. Jeshi letu la polisi, kwa kushirikiana na wananchi, wameendelea kuwasaka walimaji wa bangi na kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria za nchi. Hata hivyo, jitihada zaidi zinahitajika kuwakoa vijana wetu kutoka kwenye dimbwi la uraibu na uwendawazimu utokanao na uvutaji wa bangi.
Jeshi la polisi wakishirikiana na wananchi kuteketeza mimea ya bangi
Chanzo: mtandao
Idadi ya walemavu wa akili watokanao na utumiaji wa dawa za kulevya inazidi kuongezeka kila siku. Sio rahisi kukatiza mitaa miwili bila kukutana na muokota makopo. Hali sio nzuri kusema kweli.
Bila kujali ukubwa wa tatizo la uvutaji bangi na matumizi ya dawa za kulevya nchini, zipo njia maridhawa zinazoweza kutumiwa kutatua tatizo hili kwa mafanikio makubwa kama ifuatavyo:
1. Kuanzisha makambi ya kukarabati tabia na mienendo
Kadri tatizo la matumizi ya bangi na unga linavyozidi kuongezeka, lazima njia za kulikabili nazo ziongezeke. Hivyo, serikali ina wajibu wa kujenga vituo vya kurekebisha tabia kwa waathirika katika maeneo mbali mbali nchini.
Natahadhalisha vituo hivi visiwe kama magereza bali viwe kama makambi ambako wavuta bangi wataangaliwa kwa umakini na kusaidiwa kwa hali na mali kuondokana na uraibu na kurejea kwenye utu wema.
Kwa kusema hivi simaanishi kwamba serikali yetu tukufu haijafanya chochote. La hasha! Serikali nayo imepambana kwa namna mbalimbali ikiwemo kuanzisha hospitali ya vichaa, Mirembe. Aidha, vipo vituo mbalimbali (sober houses) vinavyohusika kurekebisha miendendo ya watumiaji wa dawa za kulevya, hasa katika maeneo yale yaliyoathirika zaidi.
Kituo cha kukarabati tabia na mienendo ya waathirika wa dawa za kulevya, Kigamboni
Chanzo: mtandao
Kwa kushirikiana na vituo vichache vilivyopo, makambi yatakayoanzishwa yatasaidia kuwahudumia waathirika wengi zaidi na itapendeza ikiwa yatajengwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa, kanda na taifa kutegemea idadi ya waathirika katika eneo husika. Kwa maana hiyo, inatarajiwa makambi mengi yajengwe maeneo ya mijini ambako tatizo ni kubwa zaidi ukilinganisha na vijijini. Wale waathirika ambao hawajazama sana kwenye utumiaji wa dawa wawekwe chini ya uangalizi kwenye kambi za wilaya na ambao wametopea zaidi kwenye tatizo, wapelekwe kwenye kambi za mkoa ambako wanaweza kupata huduma za matibabu kwenye hospitali za mikoa au kanda.
Lakini kuwaweka tu waathirika kwenye kambi haitoshi. Serikali ihakikishe kuwa waathirika hawa wanapokuwa kwenye kambi hizi wafundishwe njia mbalimbali za uzalishaji mali kama vile ukulima na ufugaji, ufundi, biashara na stadi nyingine za maisha ili watakapohitimu na kurudi uraiani wawe na shughuli maalumu ya kufanya badala ya kujikalia tu kwenye vijiwe ambako wanaweza kujikuta wanarudia maisha yao ya zamani.
2. Kuwapigia kura walimaji na wauzaji wa bangi
Ni vigumu kuzuia uvutaji wa bangi bila kuzuia chanzo cha bangi. Walimaji wa bangi na wauzaji wa dawa za kulevya wanaweza kubainishwa kwa kupigiwa kura za siri na wananchi. Kule kijjini kwetu siku za nyuma kulikuwa na tatizo la wizi wa mifugo hadi wananchi walipoamua kuitisha mikutano ya hadhara na kupiga kura za siri kuwataja wezi.
Njia hii inaweza kutumika kwa ufanisi kabisa kubaini wakulima na wauzaji wa bangi na dawa nyingine za kulevya. Ni dhahiri kuwa wakulima wa bangi na wauzaji wa dawa za kulevya ni ndugu zetu tunaoishi nao katika familia zetu. Hivyo, tunaoneana aibu pale tunapotakiwa kuwataja ili wachukuliwe hatua za kisheria. Njia sahihi ya kuvuka kizingiti hiki ni kuwapiga kura za siri kwenye mikutano ya vijiji, vitongoji na mitaa.
Baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika na msimamizi wa uchaguzi kuhesabu kura, wananchi watakaopata kura nyingi wanayo kesi ya kujibu. Kwa kuhofia baadhi ya wananchi kuwapigia wenzao kura za chuki, baada ya upigaji kura, wale watakaopata kura nyingi kwanza wachunguzwe mienendo yao na vyombo vya upelelezi na endapo itabainika pasipo shaka kwamba wanajihusisha na uhalifu, sheria ichukue mkondo wake.
3. Kuongeza umri wa kuanza shule
Kumekuwa na tatizo la wanafunzi kumaliza shule wakiwa na umri mdogo kwa sababu ya kuanza masomo mapema. Hivyo, serikali inashauriwa iongeze umri wa watoto kuanza shule ili wanapohitimu shule za msingi na sekondari na kukosa nafasi za kuendelea na masomo ya juu, wawe wamefikisha umri wa kujitambua na kuchanganua mambo, hivyo kuepuka kujiingiza kwenye makundi ya uvutaji bangi na utumiaji wa dawa za kulevya.
Uchunguzi wangu umeonesha watoto wengi huanza darasa la kwanza wakiwa na wastani wa miaka 5 na kuhitimu darasa la saba wakiwa na umri wa miaka 12. Kuna baadhi ya wazazi huenda mbali zaidi kwa kuwaandikisha watoto wao shule ya msingi wakiwa na umri mdogo wa miaka 4 hivyo mtoto huhitimu shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 10! Katika umri huu, endapo mtoto atakosa kuendelea na masomo ya sekondari na badala yake kuning’inia tu mtaani, inakuwa rahisi kwake kujiingiza kwenye vijiwe vya wavuta bangi kwani akili zake bado zinakuwa changa. Huu ni umri wa balehe ambao mtoto hupenda kujaribu vitu vingi wanavyofanya wakubwa pasipo kuzingatia madhara yake hapo baadaye.
Aidha, kitendo cha kuchelewa kumwandikisha mtoto shule humpa muda wa kufurahia utoto wake badala ya kumkatisha usingizi asubuhi ili awahi shule. Mtoto anayo haki ya kupewa nafasi ya kuutumia vizuri utoto wake na kukua kiakili kabla ya kuanzishwa shule. Watoto wetu tunawapunja sana haki yao hii ya msingi tunapowaharakisha kuanza masomo katika umri mdogo.
Zamani watoto walikuwa wakianza darasa la kwanza wakiwa na umri kati ya miaka 8 na 13. Mimi nimeanza shule ya msingi
nikiwa na umri wa miaka 12 na kuhitimu darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 19. Mtoto akihitimu shule katika umri wa miaka 19 au zaidi tayari anakuwa na upeo mkubwa kutambua mema na mabaya kwani tayari akili zake zimepevuka.
4. Kuanzisha vyuo vya ufundi stadi
Wanafunzi wanaopata nafasi za kujiunga vyuo vya ufundi baada ya kuhitimu masomo ya msingi na sekondari ni chache sana. Hivyo, serikali inashauriwa iongeze juhudi zaidi kuanzisha vyuo vipya vya ufundi kuliko kung’ang’ania kujenga shule za Kata wakati wanafunzi wengi hawapati nafasi za kuendelea na masomo ya juu hivyo kujiingiza kwenye mambo ya ovyo, ikiwemo uvutaji wa bangi, wanapokosa shughuli ya kufanya.
Wanafunzi waliohitimu masomo kwenye sekondari za Kata wakikaa nyumbani mwaka mmoja tu hufanana na wanafunzi wasiokwenda shule. Sio rahisi kutambua tofauti kati ya mwanafunzi aliyehitimu shule ya sekondari ya Kata na mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi au ambaye hajawahi kwenda shule kabisa. Kwa mantiki hiyo, ipo haja kwa serikali yetu kuongeza bidii kujenga vyuo vya ufundi, hata ikiwezekana kila Kata, kwa ajili ya kuwapa ujuzi vijana waweze kujiajiri na kujitegemea kiuchumi badala ya kushinda kwenye vijiwe na kujikuta wanatumbukia kwenye uvutaji wa bangi na ubwiaji wa dawa za kulevya.
5. Kubuni ajira mbadala kwa vijana
Kuna tatizo kubwa la wanafunzi waliohitimu masomo katika fani mbalimbali kukaa muda mrefu bila kuajiriwa. Ili kutatua tatizo hili, serikali ibuni ajira mbadala kwa vijana; iache kuwasubirisha kuajiriwa. Inawezekana kabisa vijana wanaohitimu vyuoni kutumia vyeti vyao kama dhamana (collateral) kupata mikopo ya biashara benki iwapo zoezi hili litasimamiwa kwa weledi na serikali.
Kuwaambia vijana wajiajiri baada ya kuhitimu masomo huku wakiwa hawana mitaji ya kufanyia biashara au kuendeshea shughuli nyingine za kiuchumi, ni zaidi ya kumpigia mbuzi gitaa. Umuhimu wa ajira kwa vijana ulionekana wazi mwaka 2020 pale vijana wengi walipojitosa kuchukua fomu kugombea ubunge kama njia pekee wanayoweza kupita ili wajinasue kiuchumi.
Ni mafuriko ubunge CCM
Kama ilivyo kwa wahitimu wa shule za msingi na sekondari, ni rahisi pia kwa wahitimu wa vyuo kutumbukia kwenye lindi la uvutaji bangi au kubwia unga iwapo mhitimu atakaa mtaani kwa muda mrefu akisubiri ajira hadi akajiingiza kwenye magenge ya uvutaji bangi. Na kibaya zaidi, msomi akishajiingiza kwenye uvutaji bangi hata anapofanikiwa kuajiriwa, kwa mfano, kama mhadhiri wa chuo kikuu hawezi kamwe kuacha kuvuta bangi. Ataendelea kuvuta bangi mpaka atakuwa Profesa bado anavuta tu!
Ushahidi kwa wasomi kujihusisha na vitendo vya uvutaji bangi
Chanzo: Youtube
Sio kwamba wasomi wanapenda kuvuta bangi ila ni kwa sababu ya kukosa shughuli za kufanya ndiko huwafanya kujiingiza kwenye kadhia ya uvutaji bangi wanapotafuta kujiliwaza ili kusahau matatizo ya kukosa ajira.
6. Kuwasaka wauzaji kwa mnyororo
Ni rahisi sana kuwapata wauzaji wakubwa wa bangi na dawa za kulevya kwa kuwakamata na kuwahoji watumiaji. Haiwezekani wauzaji na waagizaji wa wakosekane wakati wavutaji na mateja tunawaona mtaani kila siku. Njia nzuri ni kufuata mnyororo kuanzia kwa mateja, wauzaji wadogo, wauzaji wa kati, wauzaji wakubwa hadi waagizaji wakubwa. Hakuna muuzaji atakayekubali kumuuzia teja bangi huku akijua fika kuwa teja akikamatwa tu naye atapatikana. Kwa njia hii, biashara hii itajifia kifo cha mende.
Ikiwa njia hizo nilizozitaja hapo juu zitafanyiwa kazi kwa vitendo na kikamilifu, tatizo la uvutaji bangi na ubwiaji wa unga katika jamii litabaki historia. Ifike wakati kila raia achukizwe na vitendo vya uvuaji bangi kwani madhara yake ni makubwa sana sio tu kwa mtumiaji, bali jamii kwa ujumla. Hakuna tatizo lisilotatulika ikiwa njia mujarabu za utatuzi zitafuatwa.
Asanteni sana.