Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,203
- 157,376
NITAMTAMBUAJE MKE /MUME AMBAYE MUNGU AMENIANDALIA?
Na astor:Emmanuel
Swali;
Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu
Pastor:Emmanuel
Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa ajili yenu kwa huduma mnayoitoa ambayo imekuwa msaada katika maisha yangu kama mkristo na kama mwanajamii. Mungu awabariki sana.
Pili naomba msaada wa maarifa juu ya namna ya kumtambua mke ambaye Mungu ameniandalia. Nimefanya maombi ya kumuomba Mungu mke mwema tangu septemba 2015hadi sasa lakini bado sijapokea majibu ya maombi yangu. Ninaamini ninasumbuliwa na tatizo la upokeaji wa majibu ya maombi yangu jambo ambalo linahatarisha ustawi wangu kiroho.
Ni swami ni lilokutana nalo inbox Leo, niwieradhi kwa kulijibu swali lako huku ni ili niwasaidie wengi sitakutaja jina
Naomba kwa manufaa ya wengine pia ambao wana tatizo kama hili niwape majibu hayo kwenye kipengele cha maswali na majibu.
Majibu;
Kwa mtazamo wa haraka swali ni pana sana na ‘it is more personal’ kimajibu, lakini namshukuru Roho Mtakatifu anayeweza kutupa majibu ya kutufaa .Katika swali hili nimegundua mambo mawili ya msingi ambayo natakiwa kuyatolea ufafanuzi, moja ni namna unavyoweza kumtambua mke/mume ambaye Mungu amekuandalia na pili namna bora ya kuomba yenye kuleta matokeo.
Katika kujibu maswali haya mawili nitazungumzia mambo manne yafuatayo ambayo naamini baada ya kuwa umeyasoma haya utapata ufahamu wa kukusaidia katika kufanya maamuzi hayo yanayokukabili;
Jambo la kwanza; Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kukujulisha wewe mwenzi wa maisha yako (Isaya 55:8).
Nimeona hata sasa nianze na msingi huu na hii ni kwa sababu vijana wengi hujaribu kuuliza wanandoa waliotangulia kwamba waliwapataje wenzi wao wa maisha kwa dhana ya uongozi wa Mungu? Kutokana na majibu ambayo vijana hao hupewa wengi humuomba Mungu na wanasubiri, Mungu aseme nao kwa njia ile aliyotumia kusema na mtu mwingine.
Kibiblia wazo hili siyo sahihi kwani, Mungu ana njia nyingi sana za kusema na watu wake katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nani atakuwa mwenzi wako wa maisha. Kwa mtu mmoja Mungu anaweza akasema naye kwa ndoto, mwingine kwa sauti yake, na mwingine kwa maono, mwingine kwa mafunuo, mwingine kwa amani ya Kristo, mwingine kwa kutumia watumishi/wachungaji nk
Jambo ninalojaribu kukuonyesha hapa ndugu ni kwamba ‘Mungu ana namna yake ya kukusaidia kumtambua mwenzi wako wa maisha, ambayo si lazima ifanane na ya mtu mwingine’. Na mara nyingi namna/njia hiyo haitofautiani sana na ile ambayo Mungu hutumia kusema nawe katika mambo mbalimbali. Hivyo tafuta kujua njia ambayo Mungu huwa anatumia kusema na wewe katika mambo mbalilmbali, naam kwa hiyo aweza kusema na wewe hata kuhusu mwenzi wako.Kwa kulitambua hili nimekaa kimya kwa mtu fulani ambaye amekuwa akiuliza juu ya ndoto anayoiota kuhusu mchumba anayemtaka kwani najua Mungu anaweza kutumia njia nyingi
Kwa kuwapa watu tafsiri tofauti ya mambo wanayoyaona kwenye ulimwengu wa roho tutasabisha watu wengi waishi maisha ya kuumiza wakidhani ni Mungu amesema kumbe wakati mwingine ni hisia au hata mapepo,ninamifano mingi ya watu walioambiwa na watumishi kuwa ndoa walizonazo ni sahihi lakini mwisho wa siku ndoa hizo huwa mbaya kabisa,badala yake jenga mahusiano imara na Roho mtakatifu iliakusaidie kufanya maamuzi sahihi.
Jambo la pili; Jenga na kuboresha mahusiano yako na Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu ndiye aliyepewa jukumu la kuwa Msaidizi wako hapa duniani katika kufanya maamuzi mbalimbali. Watu wengi leo wanakwama au wanajikuta wamefanya maamuzi mabaya kwa kosa la kutokumshirikisha Roho Mtakatifu awasaidie. Mwambie Roho Mtakatifu nahitaji mwenzi(Mke),mume nisaidie kumtambua yupi ni wa kwangu, naomba uongozi wako. Roho Mtakatifu kwa hakika atakuongoza katika njia sahihi (Zaburi 32:8). Jambo la msingi ni kwa wewe kuboresha mahusiano yako na yake ili kuruhusu mawasilano mazuri kati yenu. Kumbuka mawasilano hutegemea mahusiano. Na jambo la msingi katika kuboresha mahusiano ni utakatifu na kutenga muda wa kuzungumza naye kwa njia ya maombi na neno.
Jambo la tatu; Jifunze kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie kuhusu mwenzi wa maisha yako.
Hili ni jambo lingine la msingi kuzingatia. Endapo umeamua kufuata au kutafuta kumjua mwenzi wako kutoka kwa Bwana, basi ni vema ukaruhusu mapenzi yake juu yako yatimie. Wengi huenda mbele za Bwana wakimuuliza jambo hili lakini anapoleta wazo/jibu lake juu ya nani anafaa, wengi wakishamtazama huyo muhusika kimwili na kwa vigezo vyao humkataa na kusema si Mungu. Ni vizuri ukafahamu kwamba, kama Mungu ndiye aliyemleta mtu wa kwanza kwako na wewe kwa sababu zako binafsi ukasema huyu si wa kutoka kwa Bwana, maana yake umemzuia Mungu asikusaidie kwenye hilo eneo, na hivyo usitegemee kusikia tena kutoka kwake, labda mpaka ujue kosa lako na kuomba toba.
Kumbuka usimuombe Mungu akujulishe mwenzi wako wa maisha wakati moyoni mwako tayari kuna mtu au watu ambao umeshadhamiria kutaka mmoja wao awe mwenzi wako, Mungu hawezi kusema hapo. Ikiwa unataka Mungu ahusike mpe asilimia mia moja hatafanya makosa kama Mwandamu.
Jambo la nne; Jifunze kuomba kimaswali
Najiribu kufikiri kwa nini umeomba tangu Septemba 2015hadi sasa Mungu asijibu? Kwa ufahamu nilionao katika Kristo nina hakika yeye alisha-kujibu ila wewe ndiyo hukuelewa kwamba alijibu. Nina uhakika huo kwa sababu mtu amwendeaye Mungu kutaka kujua jambo, Mungu humjibu mtu huyo ili kumsaidia asipotee katika jambo hilo.
Naamini shida ipo kwako, huenda jibu ulilokuwa unataka wewe ni kuambiwa fulani ndiye mwenzi wako, kumbe kwa Mungu huenda alikuwa anasema huu si muda wake endelea kuomba maana kwa kila jambo kuna majira yake. Zaidi huenda shida iko kwenye namna unavyoomba na namna unavyopokea, au kuelewa Mungu anapoleta jibu.
Ili kuweza kupata ufumbuzi juu ya jambo hili jifunze kutumia mfumo wa maswali katika maombi yako, naamini utaona matokeo yake. Jifunze kuyatengeneza maombi yako kimaswali, omba huku ukitaka kujua/ukitafuta ufumbuzi wa lile unaloliombea kwa Mungu.
Jambo la msingi katika maombi haya ni kuwa na muda wa utulivu wa kuhojiana na kusemezana na Mungu wako. Kama vile ambavyo unaweza kuongea kwa simu na rafiki yako na mkasikilizana na kujibizana, ndivyo Mungu anavyotaka tujifunze kuwasilama naye. Unaeleza haja yako kwa swali na unampa muda na yeye akujibu. Najua kama hukuwa na mazoea ya kutumia mfumo huu, unapoanza itakusumbua, lakini endelea kufanya hivyo utona matokeo yake.
Ingawa swali lilikuwa ni pana, naamini Roho Mtakatifu ameniongoza kujibu kwa namna ambayo kwako na hata mwingine mwenye changamoto kama hii, mtakuwa mmepata ufahamu wa kusaidia. Kama umefuatilia kwa makini katika majibu yangu sijeleza moja kwa moja ni kwa namna gani utamjua mwenza wako, ila nimeelezea mazingira mbalimbali ambayo ukiyazingatia itakuwa ni rahisi kwako kumjua mwenzi wako wa maisha.
Mungu akub we'dariki, tuzidi kuombeana
Pastor:Emmanuel
Na