ojizzle
Member
- May 23, 2011
- 50
- 10
Nimeioenda hiyoUkitaka kuja kwenye biashara hasa yenye mtaji mdogo,asije na hizo theories za darasani atafeli. Huku kwenye biashara kunahitaji moyo wa mwarabu. Mimi nina jiwe la uchumi toka 2012. Nilifanya kilimo cha mahindi ekari 7,2013 kikanikata,nikauza kiwanja 2014 nikaingia bonde la mto Rukwa kuchukua mpunga,nilikuwa na milioni 10,nilipata gunia 400+ kwa sh 25,000/= mpaka 28 kulingana na mkulima,mpaka Sumbawanga mjini nauli ya gunia 1000/=,nilitia stock toka mwezi wa 6 mpaka 12,2014.
Mwezi wa 12,2014 niliuza niliuza 55,000 kila gunia. Stoo nilikodi kwa mwezi 30,000 kw mwezi. Gharama za ubebaji toka stoo mpaka mashineni kwa mteja ilikuwa ni 1000. Kupakia kwenye gari ilikuwa ni 500 per gunia na kushusha 500.
Nilipata 21 milioni na ushee,hakuna kodo nililipa tuu ushuru wa geti 1000 kila gunia wakati natoa bushi.
Hivi sasa ni hadware nauza vifaa vya ujenzi. Nina familia na ninajenga mdogo mdogo nipo kwenye batu. Vyeti vyangu juzi ndio nimevifanyia lamination.
Ushauri: Usipoteze mda,jenga mindset ya biashara,usi-regret,hiyo milioni 8 ya masters iwekeze. Jizile mimi nilitia kambi kijijini. Huko nilijifunza kula kambare,ukilala unaamka ni kawaida kukuta nyoka chumbani. Nilienda na kabegii ka kizushi,nokia yangu nyeusi,na mpunga wangu kwenye airtel money,ukiisha naenda mjini Sumbawanga mjini. Huko Rukwa kuna malaria kali inaua,ila nilienda kiume kukusanya mpunga. Jioni kama huna degree,fanya kazi kiume halafu toka mazingira ya home. Nenda mkoa au mji mwingine. Mimi nilitoka Moshi mpaka Sumbawanga kule hakuna anaenijua zaidi ya bro aliyenipa mchongo kule. Nikajizila hakuna mtu alijua nina shule. Komaa kiume
MAZAO NA KILIMO SIJAACHA
Wasaalam