Habari za usiku huu. Ni matumaini yangu mko wazima wa afya, na wale wasio wazima basi Mungu awawezeshe muwe na afya njema.
Mimi nina swali, kama nilivyouliza ktk kichwa cha habari:
NI NINI LENGO LA ADHABU YA KIFO KWA MTUHUMIWA? JE NI ADHABU KWAKE AU WAPENDWA WAKE WASIO NA HATIA?
Nimejiuliza hili swali baada ya siku za hivi karibuni kuna raia wa Bangladesh kwa jina Motiur Rahma, kanyongwa mpaka kufa kwa kosa alilolifanya miaka ya sabini.
Pia nikikumbuka, Saddam Hussein alinyongwa mpaka kufa na ilionekana ktk mitandao ya kijamii mingi tu jinsi alivyokuwa anavalishwa ile nguo ya usoni nyeusi na kusimamishwa ktk gallows kabla ya executioner kuvuta ile pulley na kisha alivyoning'inizwa.
Kwa Saddam, lilikuwa ni zoezi la sekunde si zaidi ya 8 toka wavute pulley mpaka mauti yanamkuta, hivyo kama ni maumivu ni ya muda mchache sana kwa mnyongwaji.
Natumai adhabu zote za kifo huchukua sekunde chache sana kuchukua maisha ya mtuhumiwa, hivyo SIDHANI kama alikuwa akihukumiwa na kupatikana na hatia kwa kosa la kuua au kubaka linaendana na adhabu yake ya kifo na hasa mtindo unaotumika siku hizi wa kuwatoa hao watuhumiwa maisha.
Matokeo yake, WANAOUMIA ni wale ndugu, jamaa na marafiki wa huyo aliyeuliwa ambao hawana hatia. Hawa ndio 'wanaifeel' adhabu kisaikolojia na emotions za kumpoteza mpendwa wao.
Lengo la adhabu, pamoja ya kuwa jamii inapaswa kujifunza kutokana na kosa la mtuhumiwa kwa kuwaingizia woga wa kifo endapo nao watafanya kosa linalofanana na la mtuhumiwa, ila mtuhumiwa nae inatakiwa apate maumivu na mateso ya muda mrefu ili ajue kuwa alichofanya ni kosa, sio kumuua tu ndani ya sekunde 10. KAMA INGEWEZEKANA, AULIWE KWA NJIA AMBAYO NI YA MAUMIVU MAKALI NA NI SLOW DEATH, hata mwezi mzima wa mateso makali ya mwili na akili ayapate.
Kuna maneno ya actor mmoja wa filamu USA, alisema ukitaka kumtesa mtu USIMGUSE YEYE, dili na watu anaowapenda; sasa naona na mahakama zimeamua kutumia msemo huu kuufanyia kazi.
Lengo la adhabu ya kifo lisiwe ni kutoa adhabu kali na ya muda mrefu kwa wasio wahusika, iwe ni adhabu kali kwa muhusika. Kifo cha sekunde 10 sio adhabu kali.