Nini kinasababisha mtu akiwa ndani ya gari anatapika?

KING 360

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
3,002
5,191
Salaam wakuu,

Kuna kitu huwa sikielewi, pale mtu anapopanda gari baadhi huwa wanatapika. Hiki kitu nimekishuhudia mara kadhaa. Mara ya kwanza nilishuhudia nilipokuwa shule kwenye safari ya kwenda insta Conference ambapo kuna mwanafunzi mwenzetu ilimkuta hii hali ilibidi gari lisimame wakaokota jiwe la changarawe wakamwambia aliweke mdomoni ili ile hali isiendelee.

Hivi nini hasa kinatokea hapo?

Nawasilisha.
 

Hiyo ni motion sickness. Hii ni tatizo wanapata baadhi ya watu ndani ya vyombo vya usafiri kama gari, meli na ndege. Hawa watu wanahidi kutapika, kuumwa kichwa na pia kutoka jasho. Motion Sickness inatokana wakati balance system (system ya usawa) ndani ya mwili inahisi unasogea. Kwa mfano: kama upo ndani ya meli, masikio yanahisi mawimbi lakini macho yako hayaoni mawimbi. Mgongano kama hizo za hisia ndiyo huleta tatizo hili. Na ndiyo maana watu wengi wanajiskia vizuri baada yakufungua viyoo.

Watu hawa wanaweza kutumia "scopolamine patch" ni kama plaster ndogo yenye dawa ya scopolamine huwa inabandikwa nyuma ya masikio na inasaidia kwenye tatizo hili. Au pia wanaweza kutumia dawa kwenye kundi la "Antihistamines" yanayo punguza matapishi na kuleta usingizi.

Asante.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…