Naandika Kwa uzoefu wa mashauri mawili yaliyotokea katika Mikoa miwili Kwa nyakati tofauti.
Katika tukio la kwanza Kuna mtoto alifariki akazikwa .Baada ya miaka 2 mtoto huyo alionekana mbali na Mkoa aliofia akidhurura mitaani.
Baadaye ndugu wakajitokeza kudai kuwa huyo ni mtoto wao! Walionesha ushahidi wa kimaumbile,kudhirisha kuwa ni mtoto wao! Hata ndugu majirani, watoto wenzake walimtambua kuwa ndiye yule aliyefariki na kuzikwa!
Ili kujiridhisha Serikali iliamua kupima DNA matokeo ya vipimo hivyo yalikataa kuwa wazazi hao waliojitokeza hawana Uhusiano na mtoto aliyeokotwa!
Shauri la pili linafanana na hili kwanza Mtu alikufa, akazikwa baada ya miaka kadhaa akaonekana akiwa hai hajitambui kidogo.
Watu wakamtambua, wakaitwa ndugu zake wakathibitisha kuwa huyo ni mtoto/ndugu yao wakaainisha Kwa kufanana, alama zake mwilini na mambo kadhaa! Kwa kuwa huyu alikuwa ni mtu mzima hata jina lake aliweza kulitaja na sehemu alilokuwa anaishi.
Kama kawaida Ili kujiridhisha Serikali iliamua kupima DNA Matokeo yakaonesha kuwa wazazi hao waliojitokeza hawana Uhusiano na msukule huyo!
Nawasilisha kwenu Wataalam mdadavue hii inatokeaje?
Nimeandika Kwa kifupi na kupunguza maelezo Kwa sababu Maalum!
Kama huamini uwepo wa uchawi, misukuke nk hapa Si mahali pako!