Ninafuraha Kwa sababu nimezaa Wawekezaji Wawili na Nchi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,081
62,756
Habari Mkuu!

Ilikuwa ndoto yangu kubwa kuwa mwekezaji mkubwa katika taifa langu. Ndoto hiyo ya muda mrefu sasa inaenda kutimia.

Miaka miwili iliyopita nilikuwa kwenye Project moja ambayo inaendeshwa na Taifa la Marekani. Hapo ndipo nilikutana na pass ya wazi kabisa Baada ya kuonana na Skyler, Binti wa kimarekani mmojawapo kwenye hii project.
Pass adimu kama hizi ni mara chache Streka kama Mimi kushindwa ku-score.

Kwanza huyo Skyler mwenyewe sasa. Mtoto mweupe pee, toto la kizungu, nywele ndefu zimedondoka mgongoni kama jinni la kihindi. Macho ya yakuti samawi licha yalikuwa yanatisha lakini Taikon nikakaza tai shingoni kama Mlokole wa Moron.

Niliwahi ambiwa zamani mabinti za kizungu HUPENDA Sana Vijana WA kiafrika wenye pigo flani za kinyamwezi, ugumu flani hivi classic. Basi Taikon tangu nimeitwa kwenye hiyo project nikaanza kujiweka vurumai, valavala, kama chizi fresh flani hivi. Nywele sikuwa nimechana, zenyewe nazo hazikuniangusha Kutokana na asili yake ya Kipilipili nilichorithi.

Sikutakiwa kuoga mara Kwa mara wala kupaka mafuta ili niendane Ile Grade ya Vijana tunaomezewa mate na watoto Wakali wa kizungu. Basi hivyo ndivyo nilivyoanza ku- dribble Mpira nikielekea ndani ya kumi na nane Kabla sijaweka Mpira kambani.

Ilinibidi pia nibadilishe na lafudhi ili Isiwe imechakachuliwa. Sauti na lafudhi ya ki-local ilishafanana na mwonekano wangu. Yaani kama mshamba Fulani hivi, yaani kama MTU wakuja hivi. Yaani kama Mshikaji Fulani aliyeingia mjini hivi leo.

Hiyo ilinifanya niingie kwenye Boksi la penati kukabili lango la Skyler. Maskini Skyler hakujua aliyembele yake ni Simba mwendapole, ambaye Hali mifupa Bali hula minofu. Na mnofu ndiye yeye sasa.

Mwezi ukapita, kimya! Nikasema hapa kweli kila kazi ni ngumu. Nilichoka kuigiza Aiseeh! Lakini nilipokumbuka ndoto yangu ya Milenia nikajikaza zaidi na zaidi.

Utaniuliza si ungemtongoza. Thubutu! Nani atongoze! Wewe mjinga nini! Nazijua Kanuni na ibara ya kudili na ishu hizi. Wengi waliokuwa na Akili kama zako walimfuata Skyler na kujifanya mashababi Vijana chakaramu wakitaka kuchakura wajilie bila nidhamu. Waliishia wapi? Nakuuliza waliishia wapi kama sio kupigwa na kitu kizito.
Mimi Taikon Kutoka Makanya Huko Upareni nilifundwa kudili na mambo hayo. Mzungu kama Yule hatongozwi, Babu yangu akiwa niambia ukitaka umpata Mzungu basi tumia mtego wa Kicheche. Hiyo ni hadithi nyingine.

Binti akajikausha akijifanya CIA kunichunguza asijue nimembanika kwenye jiko la vigondi. Akauke nimtie mafuta, chumvi, pilipili na ndimu kisha nimle. Lakini sitamla kama Joka la mdimu. Asilani! abadani! katukatu! Kamwe nisingeweza.

Mtoto akachanganya nami nikamkanyaga. Nani anamuda! Streka gani akose Goli akiwa hatua tano tuu Kutoka Mbele ya golikipa. Kama yupo basi huyo sio Mimi. Mimi nilishazoea kufunga mabao nje ya kumi na nane. Nishazoea kufunga kwenye Kona, napiga mwenyewe na nafunga mwenyewe. Wangapi wangeweza kufanya hivyo? Ni aghalabu kukutana na wafungaji mahiri kama Mimi Taikon Master.

Kula chuma hiyo! Mzungu chalk! Skyler akamezwa na Nondo mla Watu, nikamtafuna zshwaa! Zshwa! Alafu nikammeza aam! Aam! Aam! Nikabeua kama jitu baya lenye muonekano wenye madevu yasiyo na mpangilio.

Shoo ikawa show! No ikawa Know! Ningefanya nini Mimi? Ningetenda nini Mimi? Nipo tayari kulipia lakini furaha yangu imetimia.
Baada ya kummeza kitukuu cha mkoloni.

Wiki tatu bila kuzihesabu zilifika, ujumbe ambao raha yake hauelezeki ukatua Maskini mwangu. Skyler akaniamba anajihisi Roho zikimchafua tumboni. Mara ateme teme mate, mara kichefuchefu, basi ilimradi dalili ya mimba zimtese Binti Yule.

Unajua kazi niliyoifanya nilipaswa kuitwa bungeni, Bunge gani bhana Taikon, mbona maneno mengi! Sikiliza! Unajua kumzalisha Binti WA kiranja wa Dunia sio Jambo Dogo.
Embu fikiria Baba mkwe wako ni Super power wa Dunia. Embu fikiria Mama mkwe wako ni Mmiliki wa World Bank sijui mashirika gani huko. Aaaah! Acheni masikhara ninyi na Wivu wenu. Acheni nitambe.

Mimba haijifichi, miezi Mitano tuu Skyler tumbo Mbele hahahaha! Daah! Basi nilikuwa namchombeza akawa anacheka mwenyewe ungedhani nimempa Mgodi. Raha tuu! Utamu tuu! Mahaba tuu!
Akajifungua Mapacha Wawili. Madume mawili hivi.

Nimezaa Wawekezaji wa baadaye, najua watakuja kuwekeza tuu. Sio ajabu wakapewa Migodi au Mradi wowote Mkubwa. Nami nitakuwa Baba WA wawezekaji.
Japokuwa wamerudi Marekani lakini Adhma yangu Ipo katika damu Yao. Hakuna wa kuitoa.

Nimemaliza!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Flow kama jiga, misifa kma khaleed...umeiwakilisha vema 255, ova.
 
Back
Top Bottom