Nina matatizo ya tumbo na kukosa choo

BRAVER

Senior Member
Jun 23, 2015
105
95
Nina matatizo ya muda mrefu (zaidi ya miaka10) ya Tumbo na kukosa choo haya siku mbili.

Nimetuma madawa mengi ya Hospitali, za asili Na tiba mbadala Lakini tatizo haliishi. Nimefanya endoscopy tatu moja Vidonda vimeoneka mbili hakuna Ila kuna iflamation.

Sasa hivi namtumia product inaitwa Shake off Phyto fiber. MK Na wadau wengine naombeni Ushauri.
 
Pole sana kwa hayo matatizo yako mimi nitakusaidia kwa Tatizo la kukos choo na kuhusu tatizo la Vidonda vya tumbo utanitafuta kwa wakati wako.

WHAT CAUSE CONSTIPATION?




UKOSEFU wa choo
ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida.

Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa.

Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?

Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?

Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo:

Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda Choo. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi.

Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvuguvug yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa Mafuta ya mnyonyo kijiko 1 muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
 
Pole sana,
Kunywa maji kwa wingi,
Mapapai,
Maparachichi,
Ndizi mbivu,
Maembe yaliyoiva.
Leta mrejesho.
 

Wasiliana nami kwa 0752 693 692 tujadiliane jambo...
 
chemsha magome na majani ya mti wa mlonge kisha jitahidi kutafuna mbegu zake japo tatu kwa siku
 

Kula Tende utakuja niambia.
 
kunywa mafuta ya olive oil (mafuta ya zaituni) yana ladha mbaya kidogo ila yanasaidia sanaa kw siku kunywa vijiko foodspoon,,ukinywa kunywa na maji ili usihisi ile harufu yake
kula vyakula vya fiber sana,, mboga mboga ,, fanya mazoezi
 
Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia kupata matatizo ya choo.

1. Angalia ni kuanzia lini ulianza kupata matatizo
2. Angalia chakula unachokula, tabia yako ya unywaji wa maji, uwezo wako wa kufikiri, aina ya mazoezi ya viungo unayofanya, choo chako unakipenda kiasi gani. Haja kubwa inatakiwa ifanyike kwenye sehemu unayoipenda, pawe mahali safi, kwani unaweza kutumia nusu saa kama unamatatizo, usiwe sehemu ambayo mwenzako anasubiri nje, inabidi uharakishe hiyo inaweza haribu system yako pia. Kuna watu wanaweka magazeti chooni wanasoma wakati wa tendo.
3. Ni muda gani kawaida unapata choo kila siku? Kubadilisha muda ghafla kunaweza leta psychological effects.
4. Umetumia dawa hivi karibuni kwa mfano, dawa za kuongeza damu mara nyingi zinasababisha ufungaji wa choo, anti acids, anti diarrhoea, inawezekana ulitakata ufunge tumbo la kuhara kumbe funguo bado inaendelea. Pia antihistamines.

Weka kumbumbu ya siku unayopata choo, ulipata kigumu na vipande vipande kama mavi ya mbuzi, ulipata kilaini na kilitoka kwa mfano wa sausage, ulipata uharo? Pamoja na rangi ikiwezekana angalia pia kama kina damu kikitoka kigumu. Hii itamsaidia daktari atakae kutibu kuelewa zaidi hali yako.
 
kunywa mafuta ya olive oil (mafuta ya zaituni) yana ladha mbaya kidogo ila yanasaidia sanaa kw siku kunywa vijiko foodspoon,,ukinywa kunywa na maji ili usihisi ile harufu yake
kula vyakula vya fiber sana,, mboga mboga ,, fanya mazoezi
Vijiko vingapi mkuu. Ni vikubwa au vidogo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…