Fikra Nimezipenda
Ni kawaida kuona meli iko kwenye maji lakini ni hatari kuona maji kwenye meli.. kuwa wewe kwenye moyo wa dunia na wala usiiweke dunia kwenye moyo wako
Kama siku ukipata hasara ya kitu ambacho hukutarajia kukikosa, elewa kwamba Mwenyezi Mungu atakuruzuku kitu ambacho hakuna siku ulitaraji kukipata
Kuwa na matumaini pale mambo yanapokuwia magumu, kwani Mwenyezi Mungu mtukufu ameapa mara mbili: "hakika baada ya dhiki faraji, bila shaka baada ya dhiki faraji"
Hatujui baada ya rehma ya Mwenyezi Mungu ni nini kitatuingiza peponi??
je ni rakaa, au sadaka, au kunywesha maji, au kukidhi haja ya Muislamu, au dua, au dhikr !!!!
basi tenda wala usidharau
Weka hisia kidogo kwenye akili yako ili ipate kulainika,
na weka akili kidogo kwenye moyo wako ili unyooke
Napendezwa na nyoyo ambazo zinapokea maumivu kwa ukimya na zinatetea makosa ya wengine kwa nia njema
Pale unapoamini baada ya huzuni ni furaha, na baada ya machozi yako ni tabasamu, hapo utakuwa umetekeleza ibada adhimu ambayo ni dhana njema kwa Mwenyezi Mungu
Ukitaabika na machungu ya dunia usihuzunike.. huenda Mwenyezi Mungu amependa kusikia sauti yako ukimuomba... usingoje furaha ndipo utabasamu.. lakini tabasamu ili uwe mwenye kufurahi..kwa nini unarefusha kufikiri wakati ambapo Mola ndiye mtengenezaji.. na kwa nini upatwe na wasiwasi na usichokijua na kila kitu kwa Mwenyezi Mungu kinajulikana.. kwa hiyo tulia kwani wewe uko kwenye jicho la Mwenyezi Mungu mwenye kuhifadhi.. na sema moyoni mwako kabla ya ulimini mwako <<nimeyapeleka mambo yangu kwa Mwenyezi Mungu>>
Mola azifanye nzuri ziku zenu kwa kumtaja kwake
Ewe Mola tumeyapenda maisha na wewe ni mwenye kuyamaliza, na tunatamani pepo na wewe ndiye mjengaji wake, turuzuku uongofu ili tuwe wakazi wake, na ziongoze nafsi zetu, kwani tumeshindwa kuzitibu. Ewe Mola kama utaturuzuku kwa rehma zako sehemu katika pepo yako basi tupe uthabiti hadi tutakapokutana nawe, na tuongoze, kisha tuongoze, na zisafishe nyoyo zetu, na turejeshe kwako mrejesho mzuri
TUAMRISHANE
MEMA