Nimeponea kuumbuka leo

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,981
45,902
Wakuu habari zenu.

Leo chupi chupi nimeponea kudhalilika.

Kwa kweli kwa sasa napitia kipindi cha changamoto kidogo ukizingatia kwamba shemeji yenu yeye ana support Russia na mimi nipo upande wa Ukraine

Pia amegeuka feminist wa hatari kisa tu awamu ya sita ni ya mwenzao.

Basi kila nikiamka tu ananiambia maza anaupiga mwingi ili mradi tu , nashukuru juzi wamepigwa mkwara basi leo hajasema hivyo tena.

Ukijumuisha mambo yote hapo juu, swala la Chai asubuhi imekua ngumu lazima niende mgahawani.

Sasa kama mnavyojua sisi wakulima hatuna mshahara na tunategemea mvua inyeshe. Sijapanda maharage msimu huu. Mbolea ipo juu na huko mjini nako wanasema hawana hela.

Basi kwakua jiko limenuna nikapitia mgahawa mmoja nipate chai.

Nikaona meza za karibu wanaagiza supu na mimi si nikajitutumua bwana nikaagiza supu ya mbuzi na chapati na juice juu bila hata kuulizia bei


Kumbe mfukoni nina buku tano aisee. Nikapiga vitu vyangu.

Ile namaliza namuuliza mhudumu bili yangu ananiambia supu elfu nane chapati mbili elfu mbili na juice elfu tatu.

Kajasho kakaanza kunitoka. Nikikumbuka mfukoni nina buku tano.

Looh, nikasema hapa mzee mzima naumbuka.

Ila nikakumbuka kuwa kwenye line yangu ya simu huwa nakuwa na akiba nikafanya malipo pale na kuondoka zangu.

Kwakweeli bila akiba ya kwenye simu mambo yangekua mengine.
 
Back
Top Bottom