Nimemrudisha mke na mtoto ukweni baada ya kukosa kazi kwa miezi 3

Maisha ni safari,yana changamoto nyingi,njia si kuzikimbia bali kizikabili. Huo mwili wako unaoona kuwa hauwezi kipambana na vibarua vya zege ndio utakaohimili rapsha za kujitoa uhai? Don't do that.
Mkumbuke mkeo
Mkumbuke mwanao

They all need you in their life brother.

Endelea kufight iko siku mola atakukumbuka.

Waangalie ndege angani

Wadudu ardhini

Hawalimi wala kufanya kazi lakini wanaishi.

Riziki yako iko mahala fulani mola kakuandikia,fight with patience to reach it....

Smile more....

Worry less...

God is always good.
 
una kila sababu ya kutabasamu , una kila sababu ya kumshukuru MUNGU, ila HUNA SABABU HATA MOJA ya kujiua au kukata tamaa.miezi mitatu huna kazi wakati wenzio wapo ambao kazi walishastaafu, ni wagonjwa kitandani, nyumba zimekwenda na bomoa bomoa na wana familia inawategemea. je hawa wafanyeje?
cha kufanya ni hiki, kesho asubuhi nenda chombo chochote cha habari na vyeti vyako , waambie unaomba kujitolea. pita kwenye makampuni na waambie unataka kujitolea. trust me utapata connection za kazi humo humo ndani ya mda mfupi.
 
Uhiii umenikumbusha rafiki yangu naye hana kazi na ana mtoto na kaz imeota nyasi. Inauma sana. Bt usiache kumtegemea Mungu. Hilo ni jaribu yakupasa kulishinda. Ukiwa unaomba kwa Mungu usiwe kama habakuki anayeomba kwa kulalamika. Baadaye akaamua kuchange jinsi anavyo omba. Mungu akamjibu. Ukienda kwa Mungu usilalamike uombapo. Yesu wangu akupatie kazi na mlango wa kaz ufunguke kwaajil yako
 
Pole sana kaka maisha ni challenge ndugu ila amini Mungu yu Hai Milele,Kwanza jiulize umemtendea nini mpaka leo hii kwa uhai ulionao huo Sio ajabu malaika wanashangaa hivi huyu/yule atendewe nini ili kuamini kwamba Mungu yupo? Kaza mwendo ndugu ni bora kukosa ya dunia ila kurithi ufalme wa mbinguni. nenda kanisani omba ushauri kwani wapo wengi wanaweza kukupatia uelekeo.
 
Mwanaume hautakiwi kukata tamaa namna hiyo, hizo ni changamoto za maisha ambazo kila mtu anaweza kukutana nazo, ( ushauri )
Usichoke kutembelea office ambazo wana deal na fani yako jipendekeze kwao ata mara 3 kw mwezi
Ni sumu kukaa nyumbani ukidhani utaitwa kwenye intervew kwenye office ulizo apply,
Jichanganye na watu wote ucjitenge kwa vile huna kazi kw sasa
Fikiria ni nini plan B yako baada iyo plan A yako kufeli,
usione aibu kufanya kazi yoyote kwa sasa angalau upate mkate wa watoto wa kila cku angali unajipanga upya na plan A life yako,
(mfano)
Mimi hapa ni muongoza utalii mbugani, lkn nimekosa kaz 2 years now,
sasa ivi nimerudia plan B yangu, naendesha tax mjini na maisha yanasonga, japokuwa kuna wavimba macho wananinyooshea kidole lkn cjali ninachofurahi ni kuona watoto wangu wanaenda chooni kma kawa na wanacheza ligi ya mchangani
 
Rafiki yangu kwanza pole, matatizo uliyonayo umejitakia mwenyewe, kuna msemo unasema safari moja huanzisha nyingine. Kitu ambacho ulikifanya ambacho kinawaumiza wengi ni pale unafanya kazi kana kwamba kazi ni ya kwako fanya kazi kwa ueledi lakini usifanye kazi kana kwamba ni ya kwako.

Nikimaanisha kuwa unapofanya kazi ambayo siyo ya kwako kumbuka kilichokuweka pale ni elimu yako tu hivyo lazima ujue kuwa unafanya kazi za watu hapo najua utanielewa.

Kosa lingine ni baada ya kuachishwa kazi hukukubali kujiachisha kazi na wewe nina maana uliendelea na maisha yaleyale ukijua utapata kazi kwa urahisi matokeo yake ukala akiba yote baada ya akiba kuisha ndipo ukashtuka wakati huo hauna namna.

Maisha ni mlima kuna kupanda na kushuka hivyo nenda na maisha kama yalivyo, kubali kushuka nayo using'ang'anie kuishi kama mwanzo hapo dunia utaiona chungu kama ulizoea kula Serena hau sea cliff yaambie maisha kuwa hayo hayapo tena.

Kuna rafiki yangu aliwahi kufukuzwa akahitaji ushauri make yeye nae alikta tamaa sana nikamwambia tulia nitakusaidia kutafta kazi wakati huo kaa hapa kwangu wakati huo kulikua na mafundi wanajenga uzio wa nyumba yangu, basi nikamwambia hawe anawasaidia mafundi katika hiyo kazi sasa nilikua nikirudi ninapowalipa mafundi naye namlipa basi wakamaliza ile kazi, wale mafundi wakawa marafiki wakawa wakiwasiliana nikaona jamaa anaamka asubuhi anarudi jioni kumbe anasaidiana na mfundi.

Kwa kifupi nikipoona anaambatata na mafundi nikamshauri ajifunze kupiga plasta na kujenga matofali ingawa ilikua ngumu kwake kwa sababu ya aibu. siku moja akaniambia bro endelea kunisaidia kutafta kazi ukisikia wametangaza kazi sehemu usisite kuniambia, kwa taarifa yako jamaa alikua mhasibu wa shirika flani binafsi lakini sasa hivi ataki tena kazi za kuajiriwa na amekua fundi mzuri sasa hivi hashiki tena tofali bali ni amekua fundi mkuu tenda anapata wanaojenga ni wengine yeye sasa ni msimamizi tu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA HAKI ELIMU.
 
tatizo umekalili maisha ya kuchomekea suti na tai kisha unakaa kwnye kiyoyoz, jaribu na maisha ya upande wa pili uone je, kuna nn?, labda nikuulize swali dogo tu, je kama ungekua hujasoma na huna hyo fani yako, usingeoa? na kama ungeoa ungeishije na hyo familia yako?
 
kwanini ujiue? mbona mimi sina ajira ila napambana mkuu? nina masters ila natembeza biashara mitaani napata faida buku Tatu kwa siku maisha yanaenda.kwanini usibebe hata zege? wanaobeba wananini mkuu na wewe kwanini ushindwe? please acha mawazo ya kujiua.halafu Mungu hua anabariki kazi za mikono sasa wewe atakubariki na nini wakati upo selective na kazi.please anza kwa uaminifu na vibarua vigumu na ikifiwa wakati wake atakuinua mpaka utashangaa
 
kwanini ujiue? mbona mimi sina ajira ila napambana mkuu? nina masters ila natembeza biashara mitaani napata faida buku Tatu kwa siku maisha yanaenda.kwanini usibebe hata zege? wanaobeba wananini mkuu na wewe kwanini ushindwe? please acha mawazo ya kujiua.halafu Mungu hua anabariki kazi za mikono sasa wewe atakubariki na nini wakati upo selective na kazi.please anza kwa uaminifu na vibarua vigumu na ikifiwa wakati wake atakuinua mpaka utashangaa

Mkuu kama ni kweli ushauri wako utamsaidia .Kweli inauma jitahidi kutafuta kazi usikate tamaa
 
Wakuu,
Habari za kushinda! Naandika nikiwa na uchungu sana baada ya Breakdown ninayoipitia. Career yangu ni kwenye Media industry, tangu niache ajira yangu ya kwanza mkoani ambayo nilistawi kiasi cha kuoa na kuwa na kwangu, nikahamia Dar ambapo nilifanikiwa kupata kazi na kuendesha maisha lakini kwa mahangaiko makubwa kiasi cha mwaka mzima wa 2015 kuwa ni mwaka wa dipression kwangu.

Bahati mbaya, mwishoni mwaka jana nikapoteza ajira yangu, licha ya kutafuta huku na huko kwa njia zote na kuhudhuria interview nyingi, sijapata kazi hadi muda huu. Hivyo nikaona nisije kuadhirika ndani, nikaamua kumrudisha mke na mwanangu mchanga ukweni wanisubiri niendelee kupambana.

Nilibakiwa na Laptop na Smartphone yangu ambavyo nilivitangaza mnada hapa jamvini kwa bei ya hasara ili nisukume siku, sikupata mteja, mwisho wa siku vikaja kuibiwa vyote sebuleni kwangu na majirani wamekana kutofahamu chochote. Angalau freelancing ilikuwa inaniokoa na hicho kilaptop, pia kilikuwa na Data zote za kujiajiri kwa kufungua kampuni ya Web Design.

Nina elimu ya chuo, vyeti safi, uzoefu wa miaka 3 na Portfolio nzuri kabisa kwenye Print Media, TV Broadcasting & Advertising, lakini nimetumia kila senti niliyonayo bila mafanikio. Wakuu nimekata tamaa na nina uchungu bila kuwa na wa kumlaumu kwasababu sioni nilipokosea au sababu ya changamoto mfulilizo kiasi hiki.

Nilianza kuhoji uwepo wa Mungu na kwanini hajibu maombi yangu, kwakweli nikamezwa na hoja za kipagani na kuanza kuukana Ukristo wangu, kwamba kama kweli kungekuwa na Mungu, kwanini aruhusu hadi familia isambaratike kwa kukosa chakula na kushindwa kujiendesha? ila baadae nikawaza kuwa unapokuwa kwenye shida sio kipindi kizuri cha kuanza kuquestion uwepo wa Mungu!

Siku za hivi karibuni nimeanza kugoogle njia za kujitoa uhai na nikaambulia ufahamu wa kwamba njia rahisi ni Drug Overdose, kwa jinsi ambavyo sitaki kuwapa watu shida, nafikiria kwenda kujioverdose msituni hata maiti yangu isiwape watu gharama za mazishi.

Nimechoka sana ndani, nimekuwa nikiwapigia simu watu mbalimbali hadi wale wa utotoni, angalau nimekuwa nikihisi faraja flani lakni mwisho wa siku bado nakuwa peke yangu. Nilikuwa ninasaza chakula, nilikuwa nina kila kitu, na kazi ndio ilikuwa kitu kikubwa...sasa sipati hata kazi, kwamba nijijenge tena, afya yangu vibarua vya zege haivimudu, ndio maana nilikimbilia shule. Pole hazinisaidii, kwenda kanisani naona hiyo nauli bora iwe lunch, sijui nifanye nini.

Hapa mfukoni imebaki elfu 10 tu, nawaza sijui wiki ijayo itakuwaje. Nilikuwa nabrowse JF kwenye Smartphone, sasahivi nipo Internet Cafe...niko down sana washkaji.
"Kila ukipiga mishe michongo inabuma? sasa ya nini uhangaike na ziko hela za ndumba?"
 
It's during darkest moments that we focus to see the light.
Brother be grateful una kitu kwenye kichwa chako hata kama sasa ivi hakikupi matokeo chanya ila Mungu alikupa kwa makusudi ipo siku utaifurahia taaluma yako kama zamani,hauna sababu ya kujiua utakua kati ya watu wa binafsi kuliko wote kumbuka pamoja na yote mke na mtoto wanakuangalia wewe unataka kesho waseme nini kumbuka VITA INAVYOKUA NGUMU NDIVYO USHINDI UTAKAVYOKUA MTAMU dont give up keep ya' head up hapa JF wote tunapitia challenges mbalimbali ila siku zinaenda.
Nikupongeze kwa ujasiri wakuongea na kuieleza jamii ni mwanzo nzuri angalau utajua jinsi wote tumepitia shuruba na mateso na wengine bado wako kwenye boti ambayo unasafiria wewe kipindi muhimu sema asante kwa pumzi na nafasi nyingine ya kupambana kaka.
Naamini unaweza kufanya kazi popote kama itakua sawa kuna kazi Songea sio ya kipato kikubwa ila itakusogeza ukiridhia nicheki PM nikuelekeze jinsi ya ku-apply na mawasiliano ili tufanye jambo,tafadhali juu ya yote tunategemea kukuona hapa tena ili utupe amani kua bado uko nasi hakuna kitu kibaya kama kushindwa kumsaidia mtu alafu usikie kachukua maamuzi mabaya,stay strong hommie hopin' to hear from u very soon.
 
pole sana ndg nami siwezi sema ni.mkasa mkubwa nooo nimesamishwa kazi kampuni.moja.hiviii kisa nimewasema ukweli.jinsi ya kuikuza kampuni.wamenisimamisha eti najifanya mjuaji heee...ngoja ajira yangu ya serikalini ije tuuu hawa watu mmmh
 
pole sana ndg nami siwezi sema ni.mkasa mkubwa nooo nimesamishwa kazi kampuni.moja.hiviii kisa nimewasema ukweli.jinsi ya kuikuza kampuni.wamenisimamisha eti najifanya mjuaji heee...ngoja ajira yangu ya serikalini ije tuuu hawa watu mmmh
Dunia imejaa tabu tupu jamani, kwenye furaha muda wote Na amshukuru Mola
 
Mkuu, pole sana na naomba uelewe si wewe peke yako uliyejaaliwa matatizo kila mtu hupitia majaribu mengi tena mengine makubwa hata bora ya kwako, nakuomba ujaribu na kujitahidi kwa kadri ya uwezo kuyazingatia yale yote wana jf member wanakupea japo si wote tutaweza kutoa background ya maisha yetu tunayopitia.
Kujiua ni kumkufuru Muumba wako.
 
Kwanza nikupe pole sana Mkuu kwa hali unayopitia.
Kimsingi hauko pekee katika hali hiyo.
Binafsi niliwahi pata hisia kama zako, nikaanza ku-question the truth of religions lakini pia the fairness of Almighty God.
Lakini ilikuwa kila nitembeapo barabarani na kuona some folks having an affluence ride their dream cars while they smile, dwell in beautiful houses, nikawa najiuliza INAMAANA HAWA JAMAA WANAPENDWA SANA NA MUNGU MPAKA WANAPATA WAYATAKAYO KULIKO MIMI AMBAYE KILA NIFANYACHO HAKIFANIKIWI.
LAKINI, MBONA MIMI SINYWI POMBE wao wanakunywa, MBONA MIMI SITEMBEI NA WAKE ZA WATU, wao wanafanya, MBONA MIMI SIFANYI DHULMA lakini wao wanafanya n.k (Na yote haya MUNGU hapendi) ?????? Ni kweli kwamba MUNGU hanipendi ila anawapenda wao tu !!!!???
Kimantiki ikawa haingii akilini. Hivyo nikajua kwa vyovyote MUNGU ana namna yake kwangu.
Wewe kama muumini wa dini najua unatambua kuwa watumishi wa MUNGU wa zama hizo zilizopita walipitia magumu saaana, refer kisa cha Yakobo, refer maisha ya Prophet Muhammad n.k. Lakini hawa walipendwa sana na MUNGU na ni wateule, iweje wapate shida katika maisha yao???? MUNGU yuko na namna juu yako.
Mkuu kitu cha kwanza kukushauri ni kwamba; clear all doubts ambazo zimeshajipandikiza kwa kichwa yako juu ya MUNGU, jenga upendo na MUNGU wako, hatimaye utapata faraja.
Ukitaka kujua kwamba MUNGU amekupa neema zake, hebu waangalie walio chini yako, afadhali yako wewe leo una hata hiyo taaluma na vyeti. Kuna watu dunia hii miaka na miaka wapo vitandani tu,
Kuna mdau mmoja ameshauri u-pay visit to the hospitals ili uwaone wale uliowazidi neema ya afya uone wanavyougulia, niko na imani that visit is goin to help you.
Na kimsingi ukishapata MIND PEACE tu basi automatically utapata PASSION, na DETERMINATION, kisha utajiona ni mtu mpya mwenye nafasi na uwezo wa kuleta mabadiliko katika maisha yako.
 
Daaah kuna brother wangu mtoto wa bamkubwa alijiua hivi hivi asyee mkui dont kill ur self pambna mpaka mwisho. By the way umenikumbushaa mbali
 
Hapa ndo nnamkumbua Robert kiyosaki na kibabu chake cha poor dad rich dad. Pole sana Mkuu ila utakapo inuka tena kimaisha tafuta hki ktabu ukisome
 
Back
Top Bottom