Nimekutana na Jini?

1. ... "Kuangalia nyuma kwa kutumia vioo sikumuona yule paka!"

Mida ya SAA 10 usiku, sidhani kama inawezekana uone kitu kilichopo nyuma eti kwa kutumia site-mirror or driver-mirror, it is never easy kwenye barabara ya giza! Unless barabara ina mataa au kuna gari lingine nyuma yako linakufuata.

2. Majini ni viumbe. Kama unaamini kuwa SHETANI yupo, basi amini pia kwamba majini yapo.

Haijawahi kunitokea, ila binafsi naamini mambo hayo yapo.

Mkuu nadhania ungekuwa ushapiga 'vyombo' + akili za usiku, walahi huyo blonde ungempa lift. Teh teh

-Kaveli-
Sasa Kaveli kwani nilikwambia nilikuwa napita barabara isio na taa?!! Ningewatajia barabara au mtaa kama kawaida yenu great thinker humu mngesema lengo la thread ni lingine. Ni hivi hio barabara ina taa mwanzo mwisho left and right. Na sikulewa ndio maana akili yangu ikaweza kujiuliza:
1.Saa kumi alfajiri mwanamke wa kizungu kasimama barabarani peke yake
2.Dress code,black long dress, kama angekuwa muuzaji angekuwa na dress code tofauti
3.Location, sio yale maeneo ambayo ningetegemea kukuta wauzaji.

Nina uzoefu na mabinti wa usiku kwa hio ninajua ninachoongea....na kweli ningekuwa na konyagi kubwa mbili kichwani ningembeba bila kujiuliza.
 
Dah... ajabu sana, eti mtu hadi unajua kuendesha gari lakini paka mweupe na mwanamke blonde aliyevaa nguo nyeusi hujawahi kuwaona live. Hii nchi ya ajabu sana
Kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti. Kuna mahali nimesema sijawahi kuona paka mweupe au mwanamke blonde?! Issue hapa ni muda,location sio case ya kuona blonde.
 
Dah... sasa tofauti iko wapi chief?
Saa kumi alfajiri, mwanamke kavaa gauni refu jeusi kasimama barabarani peke yake. Kama angekuwa anajiuza angevaa nguo fulani hivi za kuonyesha biashara halafu sio mitaa ile niliomkuta angekuwa maeneo fulani ya biashara.
 
Ndugu zangu mimi sio muumini wa haya mambo, sijui majini wanga siamini kama yapo. Ila leo kuna kitu kimenitokea kinaweza kubadili maoni yangu juu ya hivi viumbe.

Kama mjuavyo mwisho wa wiki huu unapilika nyingi za usiku na mimi leo nilikuwa kwenye misele ya usiku. Sasa wakati narudi mida ya saa kumi na robo hivi alfajiri hii nimeona vitu naona si vya kawaida.

Wakati narudi nyumbani niko peke yangu kwenye gari na barabarani ghafla akatokea paka mweupe anakatiza barabara . Kwa kawaida usiku huwa nakimbiza gari kidogo na ninaendesha katikati ya barabara, basi yule paka katokea upande wa kushoto anakatiza kueleke kulia.

Kwa instict za udereva nikanyunyiza breki kidooogo, nikahamia kushoto alipotoka nikamkwepa bila kashkashi. Kuangalia nyuma kwa kutumia vioo sikumuona yule paka! Kwenda mbele kama mita kumi nikamuona mwanamke wa kizungu 'blonde' kavaa gauni jeusi refu limefunika hadi viatu kasimama upande wa kulia wa barabara!

Nikamwangalia na yeye akaniangalia wakati napta macho yalipogongana mwili wote ukanisisimka! Kwa mazingira yale niliomkuta na muda huu si kawaida kukuta mwanamke kasimama peke yake awe wa kizungu au mswahili, ndugu zanguni huyu ni jini? Nimeandika hii habari kabla sijalala mkiona nipo kimya sana mjue ni athari za huyo 'jini'.

cc: mshana jr
hahahahahahahaπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚acha uwaga ww atakuwa dada poa tu huyo
 
hahahahahahahaπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚acha uwaga ww atakuwa dada poa tu huyo
Duh umefukua kaburi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom