Nimekupenda kutoka moyoni...

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,874
3,306
Asalaam nawasalim katka bwana...
Leo katika pitapita zangu nimekutana na jamaa ang siku nyingi tumepotezana.
Basi tukaongea mawili matatu badae akatoa simu akanionesha picha ya mwanamke basi bwana akasema hivi "kaka huyu ndo shemeji ako yaani kk huyu mwanamke nmependa kutoka moyoni nampenda sana cku akiniacha Moyo wangu utaniuma sana"...
Nikamwambia muuombe mungu akusimamie katika maombi yako kwani wanawake wengi cku hizi ni pasua vichwa..
badae tukaagana nmefika nyumbani,nikawa nawaza hivi kazi ya MOYO nikusukuma damu je kwenye kumpenda mtu moyo unahusika? Maana kama tunakosea kusema nmekupenda kutoka moyoni au moyo wangu umeumia je kwel moyo huumia?
Je jukumu la kupenda ni la kiungo gani mwilini?
Je nini maana ya ROHO?kunautofauti gani Kati ya roho na moyo? Mimi na npo njia panda maana maswali haya nimekoswa majibu yake karibuni kwa mchango
 
kinachopenda Ni Moyo ama roho?
Hisia ndio inayosukuma upendo sio moyo wala roho bila ya hisia huwezi kupenda ndio mara nyingi watu husema umeniumiza hisia zangu. Unaweza kumuona mwanamke mzuri lakini utasema hata hajanivutia. Hapo ukimaanisha hajagusa hisia za matamanio ya upendo. Nikijibu suala lako kirahisi Hisia na matamanio ndio upendo. Moyo kazi yake kusukuma damu Roho kazi yake kuendesha maisha tu, bila ya roho hakuna maisha.
 
Nimekupata vyema mkuu je kumbe watu huwa wanakosea wanaposema umeniumiza Moyo wangu ulishawahi kukwazika ukasikia kama mapgo ya moyo yanabadirika na mood in change? Je moyo huumia ama?
 
Roho n nn?
 
Hahahaaa kabla hata sijamaliza kusoma nimecheka hapa " wan awake wa siku hizi ni pasua kichwa". Hapa umemaanisha nini
 
Najaribu kupima ulichofikiria. Naona ulifikiria kwa undani sana. Ila tunaposema moyo wangu umekupenda Sijui kama huwa tunamaanisha moyo wa kiumbile.
 
Kuna moyo upi na moyo upi mkuu ulishawahi kumwambia mtu umempenda kutoka moyoni je Ni kweli ulimpenda kutoka moyoni au rohoni mwingne anasema ubongo ndo unaopenda ...
 
Moyo ni kiungo ktk mwl
Moyo ni nafsi pia moyo ni roho,yan moyo unaweza kuleta matokeo ktk mwli
 
Dr. adams faida,kupenda ni jambo la hisia na katika mwili kiungo kinachouhusika na kvafsiri hisia kama vile kupenda,uchungu,maumivu unapotendwa ama kufiwa ni UBONGO si moyo wala roho ambayo hipo kiimani zaidi.

In biological point of view,kupenda kunasababishwa na kumwaga au kuzalishwa kwa homoni kadhaa kutoka hatua ya kwanza ya mapenzi mpaka ya tatu.

Katika hatua ya kwanza ya kuelekea kupenda, hatua ya matamanio(lust stage)

mwili huzalisha homoni ya testosterone hormone kwa mwanamme na oestrogen hormone kwa mwanamke, ambazo uchangia kumfanya mtu kuwa na matamanio ya wanawake.

Hatua ya pili ya kupenda ni attraction stage,ambayo mwili huzalisha kwa wingi homoni za adrenaline(epinephrine),dopamine na noradrenaline(norepinephrine).

adrenaline inapozalishwa kwa wingi ndani ya damu inasababisha mapigo ya moyo kupiga kwa kasi na nguvu,na hivyo kvmfanya mtu pressure ya damu kupanda na hatimaye majasho ukutoka hii hali ukutana nayo mtu anapokutana na mtu anayehisi kuvutiwa nae.

Nitaendelea.
 
Naona umejibu kiANATOMY zaidi mkuu lakin bado cjapata jibu tusemeje tunapopenda mkuu?
 
Akili,macho na masikio ndiyo vyanzo vikubwa katika swala zima la kupenda baada ya viungo hivyo kusikia ama kuona vinapeleka signal kwenye akili na akili inatuma signal kwenye moyo...Ndiyo maana ukimuona msichana uliekuwa unampenda sana ama unamuwaza sana ghafla lazima mapigo ya moyo yabadilike yapaige kwa kasi sasa hapo ni akili imetuma signal kwenye moyo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…