Habarini wakuu!
Kama ilivyo kawaida yetu humu ndani tumezoea sana kuitana WAKUU bila kujali unayemwita ni kweli ni Mkuu au la!
Humu ndani kuna wazee na wajukuu zao, wazazi na watoto wao, watu waliotalakiana, wenye vyeti feki na halali, misukule na watu timamu: Lakini utamaduni wetu ni huu wa kuitana MKUU.
Nimegundua Kwanin tunalitumia sana neno MKUU;
Kwanza, humu ndani wengi tunatumia ID na AVATAR feki hivyo kila mmoja ana HOFU na mwenzake. Kuchati na mtu usiyemfahamu kunahitaji Busara yaweza kuwa unacomment thread ya babu yako, au mama au boss wako kazini Ndiyo maana wengi tunatumia neno MKUU.
Pili nadhani wengi wetu tunatumia MKUU ili tusitukanwe, wengi humu ukiwaquote na kucomment vibaya wanarudisha majibu ambayo yatakuharibia Siku na mood ya kufanya kazi itaisha.
Tatu, wengi wakianzisha Uzi hasa unaohitaji mchango wa mawazo, hutumia sana WAKUU ili kuvuta watu watiririke nondo za maana na kwakuwa tumeshavimbishwa bichwa kwa kuitwa wakuu, wengi tunauvaa uhusika wa UKUU ipasavyo.
Haya WAKUU, Mimi nimegundua hayo, ongeza na lako kama lipo.