Nimeenda supermarkets kadhaa wanasema hawana sukari

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
426
684
Nilinunua sukari nyingi ya kunitosha mwaka mzima (Kwa kuwa naishi mwenyewe ni rahisi). Baada ya kuja suala la kudhibiti bei ya sukari, nadhani wafanyabiashara wako katika mgomo fulani. Jana nimeenda supermarket wamenambia hawana sukari.

Nadhani badala ya kudhibiti bei kuna namna sahihi zaidi ya kudeal na suala hili. Bei za vitu zitajipanga zenyewe, wala hakuna haja ya kupanga bei. Badala yake ni muhimu kuruhusu sukari iingie nchini na kama bei inaonekana kuwa kubwa basi inawezekana kuondoa baadhi ya tozo na kodi ili bei zishuke zenyewe.

Haya masuala ya kuweka bei tunarudi zama za ujamaa ambao ulishafeli kitambo.
 
hizo zote kelele ndio ununue sukari ya kukutosha mwaka mzima? tuseme ni kiasi gani?? ila jf nyie
Kwa miezi minne natumia kilo moja, kwa mwaka ni kilo nne zinanitoshwa mwaka mzima, mimi nilinunua tu kilo 10. Je, karibu home, sijaoa
 
Ukiwa na wafanyabiashara wajinga wajinga kama wa kwetu hapa ni tatizo maana wanakula na wakubwa haiingii akili wafanyabiashara 5 au 6 wanaamua wanachotaka na nchi haiwafsnyi chochote..

Kama sukari hatuzalishi ya kutosha tutoe vibali vya kuingiza sukari kutoka nje. Vibali vitolewe kwa viwanda vinavyozalisha ili kuvibust pia kiuchumi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…