Habarini wanajf.
Jana jioni nilithibitisha kuwa misemo, semi na methali za wahenga zina beba maana nzuri.
Story iko hivi, mtaani kwetu kuna kaka tunaishi naye, wao ndio wazawa wa huo mtaa wanajiita wazawa sie wengine kwa kisukuma wanatuita MAJOGOLI. Kaka huyu ni mwizi sugu tena ambaye amevuka hatua ya kibaka sasa ni jambazi.
Ni jambazi ambaye tukio lolote la wizi likitokea kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela lazima Polisi wamkamate kama mshukiwa wa kwanza. Huwa anakaa sana mahabusu hadi tunamsahau lakini baadae anarudi tena uraiani kuendelea kutusumbua, hajawahi kuhukumiwa. Watu walishahoji sababu ya yeye kutokufungwa lakini OCD akasema kuwa tatizo ni kwamba watu hawaendi mahakamani kutoa ushahidi kwahiyo kesi inakosa uzito hadi anaachiwa huru.
Oooops! ngoja sasa niwasimulie yaliyotokea jana.
Jana jioni wakati natoka kibaruani nikakutana naye barabarani tukasalimiana akaniomba nisimame tuongee kidogo kwa kuwa ana matatizo, na mie bila hiyana nikamkubalia kumsikiliza.
Ndipo hapo alipoanza kunielezea mkasa uliompata juzi usiku 7/11/2017. Alisema kuwa watu walivamia kwake usiku, wakamfungia mlango kwa nje halafu wamemubia kuku wake wa kienyeji 16. Baada ya kugundua kuwa wamemfungia, ilibidi apige simu kwa jirani zake na hapo ndio jirani walikuja wakavunja komeo la mlango.
Akazidi kuongea kwa hasira "Yaani sister nitahakikisha hawa wezi nitawasaka hadi niwapate, nitazunguka hoteli, baa, vibalu vya pombe za kienyeji na hata kwa mama lishe wote hapa Buswelu hadi nijue kuku wangu walipouzwa"
Baada ya kumsiliza kwa kina sasa ikawa zamu yangu kutoa ushauri. Nikamshauri kuwa aende Kituo cha Polisi Nyakato wakamfungulie taarifa.
Lahaula kwata! Aliniangalia jicho baya, la hasira ambalo kwa mie mtaalamu wa "non-verbal communication" nilitafsiri kama vile ananiambia:
1. Wee mwehu nini ushauri gani huo.
2. Wee naye hebu ni kome sitaki ushauri wako wa kipuuzi
3...
Leo nitajitahidi sana nimtafute jioni anipe mrejesho wa kutafuta mali yake halafu nitauweka hapa JF.
MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU.