1. Wananchi waelimishwe tena wazi wazi kwamba askari kama hana kitambulisho asiruhusiwe kuondoka na mtu au kumkamata (isipokuwa kama amevaa mavazi ya kiaskari). Tunapoelekea hao wajulikanao kama magaidi wataweza kuingia na kwa jinsi wanavyoendesha matukio huko kibiti, ni dhahiri watanzania wote hatuko salama. Dalili zinaonyesha kwamba wakibanwa mistuni watahamia mijini, hii inahitaji kujipanga.
2. Polisi wajisafishe na kiwe chombo huru. Waachane na siasa na waingie kazini kwa weredi. Kuna kila Dalili kuwa matukio ya huko Pwani yana mikono ya baadhi ya askari ambao sio waaminifu kwa kazi zao. Hapa namaanisha hao wanaotekeleza uhalifu wana taarifa za ndani kutoka kwa majeshi yetu. Hata operation inapobadilishwa na kuweka chombo kingine chenye nguvu kama Jeshi na Makomando kwa kutumia kivuli cha Polisi taarifa huvujishwa na waarifu kutake action. Maana yake kuna usaliti ndani ya Majeshi yetu hasa jeshi la Polisi.
3. Ufanyike mpango wa kuwatambua askari waliofukuzwa hasa mahali walipo na kazi wanazozifanya. Intelijensia iingie ndani zaidi kuchunguza hili. Mbinu wanazozitumia waharifu ni dhahiri zimeenda shule kiasi cha kuyatetemesha majeshi (sio Polisi tu).
4. Jeshi la Polisi liache mzaha na Wananchi wote waheshimiwe equally before the law. Ni aibu kuona nguvu kubwa inatumiwa kudhibiti vyama vya siasa badala ya kuwalinda Wananchi na mali zao. Hivi sisi Wananchi tulieleweje jeshi letu siku 5 baada ya maneno ya faraja kutoka kwa IGP watu zaidi ya 5 wameuawa tena eneo lile lile? Kwa silaha zile zile? Jeshi lijitafakari, kimsingi hawa jamaa "they are not Localize" wanahama pale wanapobanwa sehemu moja. Ni vyema jeshi liunganishe nguvu moja, Hata mawazo ya wafuasi wa vyama vya upinzani yanahitajika kwenye ulinzi na usalama wa nchi. Ni aibu kwa RPC kutoa tamko la kushindana na CHASO tena wa chuo fulani (mbeya), wakati mwingine busara zibgeweza kutumika. Na kazi hii kwa vijana wa chuo kimsingi Mkuu wa kituo cha Polisi angeweza kulishughulikia badala ya matamko kutoka kwa RPC na OCD ambao kimsingi wanakuwa tayari wamepokea maagizo kutoka juu.
5. Majeshi yote specifically yale yanayohusika na operation maalum kama za Kibiti na Tanga, familia zao zihamishiwe makambini (mahali salama). Kuna Dalili za visasi kwenye matukio yanayoendelea tangu yalipotokea yale ya Tanga na uvamizi wa vituo vya Polisi. Hawa jamaa wanaweza kuzigeuzia kibano familia za maaskari Maana Hata ya kibiti yalianza na viongozi wa serikali.
Ni hayo tu kwa leo, maana haya mengine Ni aibu.
Cc
mwigulu nchemba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers