Umetumia msemo tata ambao sijui kama wewe mwenyewe unauelewa, "kubadili fikra". kubadili fikra sio tu kufanya kile wewe unachokiwaza bali nadhani ni mtu kutafuta fikra za ziada kuongezea kwenye zile alizokuwa nazo.
sasa mfano wewe unasema "tupo Katika wakati mgumu Sana kiuchumi. Uwezo wa watu wengi kufanya manunuzi umekuwa ukipungua kila uchwao, mzunguko wa pesa umekuwa ukipungua kila siku" alafu baada ya kutoa tathmini hiyo ya kiuchumi umetoa hitimisho au ushauri "Kwa wale ndugu zetu wenye vipato vya uhakika ni muda muafaka wa kuinuka. Ni vizuri wakajielekeza kwenye kupunguza matumizi au kwa lugha lahisi, "wakaokoka". Kiasi watakachookoa basi wakielekeze kwenye uwekezaji"
yaani ni sawa na kusema chakula hiki kina sumu alafu unamalizia kwa kuwashauri watu watu kuwa waanze kula.
uwekezaji unaendana na soko, biashara zinapokuwa zinashamiri ndio wakati wa watu kuwekeza mitaji ili kuzalisha bidhaa au huduma za kuwapatia wanunuzi wanaoongezeka lakini wanunuzi wanapoanza kupungua, uwezo wa watu kununua unapopungua maana yake ni mitaji iliyoko sokoni inaanza kuwa mikubwa kuliko wateja na matokeo yake biashara zinakufa.
si wakati muafaka wa watu wengine kubana matumizi eti nao waache kununua na wawekeze maana yake ni kufanya hali ngumu zaidi. kipindi hicho ni cha kutafuta mbinu za kuchochea wanunuzi wanunue zaidi.