Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,041
- 38,942
Wewe hata kwenye 9000 hustahili kuwemo hivyo kaa kimya upike kisamvu. Wewe na kundi lako lini mmesema hiki haijafanya vizuri? Si kila siku ni kukariri mazuri tu kama kasuku? Aliibuka Mwakyembe akasema anayetaka kufunga ndoa lazima awe na cheti cha kuzaliwa, kwenye busara wakapinga humu jf lakini mkaibuka mawakili tumbo mkatetea eti itahamasisha watanzania kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Baada ya siku 2 Bosi wake akapiga chini tamko ka Mwakyembe, mkarudi tena na mapambio mapya, " hongera sana Rais kwa kuwajali wanyonge". Mmesimama hatujui; Mmechuchumaa hatuelewi; Yaani hamna mnachosimamia ili mradi mpate bk 7 zenu mkono uende kinywani. Juzi alupotoa tamko ka TCU kuacha wanafunzi wajichagulie vyuo wenyewe tulimuunga mkono na kumpongeza. Hatuna ujinga wa kusifu upuuzi, lakini pia sio ujanja kudharau mazuri. Badilikeni nyie mliosetiwa kusifia kila kitu utafikiri batani ya kukosoa imenyofolewa.Wenye tabia hizo wengi wao hawataacha, kwasababu awamu hii ya 5 wanaisoma namba na kusaga meno. Subiri wale 9,000 wakiguswa nao watajiunga kufanya hayo na wengineo wengi tu.