Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,666
- 729,798
Tunamalizia wiki iliyokuwa na drama nyingi kuhusiana na mwajiriwa wa Msanii Masanja mkandamizaji kwa cheo cha katibu kwenye shughuli zake za usanii na kanisa aliyepoteza uhai kwa kinachosemwa kajinyonga
Asilimia 99 ya mijadala ilitawaliwa kwenye kujadili yafuatayo
.Kifo tata cha katibu
.Mahusiano ya katibu na mke wa boss wake
.Reaction ya Masanja baada ya hayo matukio
.Na mwishowe watoto wa Masanja na mkewe
Athari kwenye shughuli zake za kisanii ni kama hazikugusiwa kabisa
Athari kwenye makampuni aliyoingia nayo mikataba ya kufanya matangazo ya kibiashara pia hayakujadiliwa kabisa
Athari kwenye kituo chake cha kiimani/kanisa pia zimejadiliwa kwa uchache
Kwenye mijadala husika na wachache walijaribu kugusia athari binafsi na za kifamilia
Kwenye mada hii tutaangazia athari za kanisa la Feel free church na hatima yake
Ukiachana na Makanisa yaliyojengwa kitaasisi na mifumo kamili ya utendaji kazi, makanisa mengi hasa yaliyoibuka karne hii yenye kumilikiwa na watu binafsi, yalipotea, kufa, kupoteza mvuto, kuzorota ama kufifia kutokana na wamiliki wake kupata dhoruba mbalimbali za kimaisha
Makanisa ya Marehemu mama Rwakatare, Nabii Elijah, Mzee wa upako, Mfalme Zumaridi ni mifano michache ya hicho nilichokiandika hapo juu kwa hapa nchini.. Kwakuwa wao ndio roho ya kanisa, basi kilichowapa wao kililipata kanisa pia
Kanisa la msanii Masanja mkandamizaji, lililoanza kama utani, ni kanisa changa lililokumbwa na upepo wa dhoruba kutokana na mmiliki wake kukumbana na changamoto za kimaisha. Achana na uchanga wake yeye ndio alikuwa mkuu wa hilo kanisa na shughuli zote nyeti na muhimu zilikuwa chini yake kama makanisa mengine ya namna hiyo yalivyo
Yaani ustawi wa kanisa, kukua na kushamiri kwake vyote vilikuwa mikononi mwa mwanzilishi wake.. Maombi, mahubiri, maono, na shughuli zote za kiroho vilikuwa mateka chini ya roho moja!
Msiba wa katibu wa Masanja ulikuwa msiba wa kanisa! Kama kulikuwa na katibu ina maana basi kulikuwa na viongozi wengine wa kukaimu na kukasimu madaraka pindi wakubwa wakiwa hawapo! Kanisa la jisikie huru lilipaswa kuonekana popote kivyovyote kwenye jambo kubwa kama hilo la msiba bila kujali yatokanayo!
Kwa kutofanya hivyo kanisa limejitia doa kubwa na baya mbele ya jamii na watu wachache waliokuwa na imani nalo! Kwa kuzidi kuharibu mmiliki akashindwa kutofautisha mambo binafsi ya kifamilia na ya kanisa lake! Akaenda huko mbele ya waumini wake na kuanza kuwapa vichambo vya uhakika wote walioshiriki mijadala mitandaoni kuhusiana na sakata zima!
Taswira nzima ya kanisa ilipigwa upofu pale! Na inawezekana lile likawa ndio kusanyiko la mwisho ama la lenye waumini wengi! Jumapili hii ndio itatoa majibu na hata kama wakiwepo wengi ni kwa ajili ya kwenda kushuhudia umbea
Kashfa na tuhuma zilizomkuta Masanja zinaathiri moja kwa moja shughuli zake zote za kisanii lakini kubwa na baya zaidi kanisa lake
Kashfa na tuhuma hizi ni tofauti na zile zilizowahi kuwapata wamiliki wa yale makanisa mengine kama kina
Zumaridi kupigana maofisa wa serikali
Mzee wa upako na ulevi
Gwajima na uzinzi
Geodavie na uchawi nknk
Hili la Masanja ni tuhuma za mauaji na mazingira tata ya kifo husika na ishu za kifamilia..! Imekaa vibaya mno!
Kwa jicho la kiimani na kiroho tunaweza kusema ni changamoto na jaribu la kiimani..! Lakini kwa tafakuri nyepesi kabisa ni huduma ipi kubwa ya kiroho aliyowahi kuifanya kiasi cha kumtikisha shetani hata aamue kulipa kisasi!?
Hatima ya kanisa la jisikie huru limo mikononi mwa suluhu ya kiroho kama Masanja mkandamizaji na familia yake hawana vinasaba na damu ya mtendaji wake katibu wake! Damu ya mtu hunuka., na harufu yake hutiwa chaji na roho iliyomo ndani yake... Roho ni kitu kisichokufa hivyo huibeba damu yake kutengeneza mizania ya haki..