Ni nani aliyewapa vibali vya Business permit badala ya work permit Huawei-tiGO?

TCRA ,TRA NA WIZARA YA KAZI

Katika kipindi hiki ambacho kila mtu mwenye mapenzi na nchi hii anahangaika ili tutoke hii sehemu na tusonge mbele, ni jukumu la kila mwenye nafasi kuitumia vizuri kufanya majukumu yenye tija kwa Tanzania.

Neno outsorcing (uhamishaji wa majukumu ya kampuni kwenda kampuni nyingine)limejitokeza sana Tanzania katika sekta ya mawasiliano katika kipindi cha miaka 3 au 4 iliopita likihusisha kampuni kongwe na kubwa ambazo ni Airtel , Vodacom na tasisi za kifedha (mabenki)

Kwa sasa vitengo vyote vya watalaam wanaowezesha simu zetu kupiga na kupokea simu kwa hizi kampuni kubwa za Vodacom na Airtel vilishahamishiwa India muda mlefu.

Hii imewaacha watalaam wa kitanzania kubaki wamebung’aa kazi waliobaki nayo ni kuuza na kukwangua vocha maana hata voucher printing ni kazi ya m-South Africa

Zipo aina kuu mbili za outsorcing:

1. Outsourcing within the country(uhamishaji wa majukumu ya kikazi kwenda kampuni inayofanya kazi nchini)

2. Outsourcing outside the country (uhamishaji wa majukumu kwenda kampuni inayofanya hayo majukumu nje ya nchi.

Tanzania na watanzania kwa ujumla wetu hili neno sio zuri sana ingawa linaweza kutetewa kwa nguvu zote na wafanya biashara hasa wawekezaji.

Kwa aina ya kwanza ya outsorcing sio mbaya maana kampuni inahitaji kupunguza baadhi ya majukumu yake ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kupata faida.Hii huleta ufanisi na mbinu mpya katika kampuni na kuondoa desturi ya kufanya kazi kwa mazoea.

Madhara ya outsorcing yamejitokeza katika aina ya pili :

1. Watanzania kukosa ajira na kuleta madhara kwa mtu mmoja mmoja.

i. Mfano katika miaka ya hivi karibuni vyuo vingi hapa nchini vilianzisha fani za mawasiliano na uhamasishaji ukawa mkubwa ili kuleta mafanikio katika hii sekta ya mawasiliano. Kama sikosei ndo sekta inayozalisha watembea na bahasha wengi kwa sasa.

ii. Hawa ni vijana ambao tafiti zinasema ndio wanaoongoza katika matumizi ya simu na internet, hela zao ndo ambazo zinaenda kuwalipa mishahara vijana wenzao walioko India na Uchina.

2. Nchi kupoteza mapato

i. Fanya tathimini ya wafanyakazi wa Vodacom na Airtel mchango wao kama Pay As You Earn, ilikuwa kiasi gani na kwa sasa hilo pengo limezibwaje.

ii. Bora hayo mapato yaongezwe kwenye kodi yao ili nchi isipate hasara kwa maamzi ya mwekezaji.

3. Usalama (mambo ya udukuzi wa mawasiliano ya simu)

i. Hizi nchi zetu ambazo ni changa katika sekta ya mawasiliano kuna mengi yanaweza kujitokeza unaporuhusu mifumo yote ya kimawasiliano kwenda nje.Huwapa shida wawekezaji wanapokuwa na waajiriwa wazawa katika mifumo ya kampuni maana hujui uliemwajiri ni nani au ni mzalendo kiasi gani.

ii. Kazi hii huwa rahisi sana wanapokuwa na watendaji wote wa nje, ni bora kama TTCL yetu ingekuwa imara ingetusaidia baadhi ya number za viongozi wetu kutumia mfumo wa kwetu.

Ni ushauri kwa wenye mamlaka kama TCRA, WIZARA YA KAZI NA AJIRA,TRAkuliangalia hili suara kwa mapana, naamini tuna viongozi wa juu wazuri wenye mapenzi mema na nchi hii chini ya uongozi uliotukuka wa dr. J.P.MAGUFULI
 
Haya malalamiko yametulia na nina imani yamefika mahali pake. subiri tu JPM atafanya yake kama hao wahusika hawatuchukua hatua
 
Wapo Watanzania wengi nje ya nchi ambao ni wahamiaji haramu. Jana usiku tu nilikuwa nasikiliza katika news kwamba wabunge wanataka ku double check uwezo wa Rais kuwakingia kifua illegal immigrant workers,kwa sababu wapo wengi sana,na kule Marekani wanahesabika in the millions more than ten million- Obama anazuia wasifukuzwe.Kwa kifupi,nasema sheria hii ya uhamiaji serikali inapokuomba msaada wako kuwakamata hawa jamaa,na,in fact,sheria yoyote,lazima ikuguse wewe,usiifuate kibudu. Jirani yako ambaye umekaa nae kwa amani miaka mingi,halafu unamripoti yeye mhamiaji haramu? Hiyo haina maana. Jirani mwenye maringo ambaye ni mhamiaji haramu,huyo ndie wa kubishana nae.
Nimetafuta point katika haya maelezo inayoweza kuweka positive input katika uzi huu hakika sijafanikiwa kuiona......Tafadhali mkuu Andrew Nyerere unaweza saidia nijue point yako ni nini hapo?
 
Huyu Norman aliulizwa unapafahamu Namanga au ulishafika Kenya akasema hapana lakini passport yake inaonyesha alitokea Kenya. Hili nalo ni jipu.

Tunatumahini utalifanyia kazi hili JIPU.

Watu wananeemeka na ofisi za Umma! Anyway Miezi imeenda basi rudisheni mrejesho tuone kama JP anatimiza ndoto yake ya Hapa Kazi tu!
 
LHUAWEI TIGO PROJECT:

Je, ni nani aliyewapa wachina na wahindi hawa vibali vya "BUSINESS VISA" badala ya "WORK PERMIT"?

Tangu tarehe 04-01-2016 wageni wakiokuwa wakifanya kazi hapa Huawei Tigo project kwa vibali vya CTA tangu vipigwe marufuku na waziri wa kazi na baada ya ukaguzi wa kina wa uhamiaji walianza kukimbia ofisi nakutokuja ofisini huku wakifanyia kazi majumbani kwa kutumia njia ya VPN(virtual private network). Lakini majira ya jion na usiku huonekana ofisini wakiendelea kufanya kazi zao kama kawaida. Rais JPM, Je Serikali yako ikifika usiku nayo inaenda kulala?

Kama ujuavyo any foreigner is a boss pia wakiendelea kutupa majukumu kama boss kama kawaida. Sasa basi haya yote tuliyaripoti uhamiaji kwa zile ermegency contact zao na baadhi akiwemo mkuu wa idara ya ufuatiliaji hapa kinondoni. Lakini bila mafanikio.

Ikionekana kabisa kuwa kunaendekea figisu figisu ndani ya uhamiaji kinyume na utendaji wa Rais wetu mpendwa Mhe. Magufuli.

Hii hali imeendelea mpaka jana, sasa cha ajabu leo wachina, wahindi wa hapa Huawei-Tigo project (kijitonyama -Derm house 1st floor) wameingia wengi na kufurahia kuwa wamerudi kazini kama kawaida tukiwauliza kuwa mmepata work permit wamekiri kuwa work permit ni kazi kuzipata lakini kampuni ya Huawei imetutafutia BUSINESS VISA ambayo hutolewa na immigration kwa ajili ya kufanya kazi kama business trip.

Sasa wafanyakazi wazawa tumeshangazwa na hatua na mpango madhubuti wa serikali ya away ya tano na kasi ya HAPA KAZI TU ikifanyiwa mzaha na baadhi ya watendaji wa uhamiaji either kwa maslahi binafsi au kutokuwa na mlengo wa uzalendo wa nchi au kutaka kwenda kinyume na kasi ya raisi wetu mpendwa.

Hii business visa zimetolewa kidanganyifu maana hawa foreigners ni boss wetu na wanafanya kazi hapa wengine wana mwaka mmoja na zaid kama Boss Zhang Dong, Fu shiyou , Fen Gui, n.k

Pia na GNOC boss Arul Doss, Pia wengine maboss wamekuwa wakija kazini lakini tuna utata na work permit zao walizokuwa nazo haziendani na kazi wanayoifanya kama HR wetu ni mchina Chen Xuli ambaye akifuatiliwa ana work permit ya kitu kingine kabisa ambacho sicho ambacho anachokifanyia kazi maana nitashangaa serikali yetu makini impatie mgeni work permit ya HR ambayo mtanzania anaweza kufanya,

Pia bado tukiwa na HR consultant Fan Xiliang ambaye yeye ni sawa lakini si huyu Chen Xuli aliyesomea English leo ni HR wetu katika hii project wakamleta HR assistant Andrew Ikangula (Mtanzania) ambaye hathaminiki kabisa.

Pia kuna binti mmoja aitwaye Guan Shanmei (Mchina) ambaye ana work permit ambayo pia hatuna uhakika ni ya nini maana kiuhalisia anafanya kazi ya receipt checkup for retirement ambayo mtanzania anaweza kufanya ambaye akionyesha uwezo wake hafifu alishawahi kutuma mishahara ya staffs kwa bahati mbaya kwenye email ya staffs ambapo mishahara ni siri kubwa,

Pia walipokuja kukaguliwa na immigration alionyesha uwezo mdogo sana mpaka akampiga picha immigration officer akachukuliwa kwenda ofisi za uhamiaji figisu figisu zikafanyika akatolewa kwa muda mfupi sana.

Tuna mengi ya kulalamika lakini kwa ofisi stahiki za kushughulikia haya mambo tunaomba yashughulikiwe maana hatutachoka kufanya further escalation ili tuenende na kumuunga mkono Raisi wetu Dr Magufuli.

Pale uhamiaji kuna majipu mengi tu ya kutumbuliwa pia kuna wageni wengi ambao pia passport zao zilionekana zimegongewa mhuri wa namanga boarder of Kenya na passport ya Norman (mZimbwabwe) ikachukuliwa kwa ufuafiliaji lakin kesho yake alirudishiwa na kila kitu kikabaki kimya figisu. Huyu Norman aliulizwa unapafahamu Namanga au ulishafika Kenya akasema hapana lakini passport yake inaonyesha alitokea Kenya. Hili nalo ni jipu.

Tunatumahini utalifanyia kazi hili JIPU.
Mkuu hapo umemaliza kila kitu, sasa ni kazi ya Serikali kufanya yanayostahiri
 
procedure za uhamiaji nazo ni jipu tu maana hili suala linaongelewa sana hata mipakani na rwanda huko, watu wanaingia kama cheap labour wanapiga kazi kimya kimya maana kupata documents milolongoaf helakubwa...tujipange turekebishe kwanza uhamiaji wakati huo tunawakaba vilivyo hawa wageni wasannii(kuingia kwa magumashi)
 
Poleni sana kwa yaliyotokea hapo Tigo Huawei Project. Wakati ikiwa sina ni na dhamira ya kupinga ulichoandika, naomba nikupatie elimu na ufahamu juu ya mambo ya uhamiaji na vibali vya kufanya kazi.

1. Idara ya uhamiaji - kwenye mipaka au ofisi zao - hawatoi business visa. Hizi zilikuwa replaced na CTAs kulingana na Sheria ya Uhamiaji ya 1995 na regulations zake.

2. Kulingana na Sheria ya Uhamiaji ya 1995, Mkurugenzi wa Uhamiaji alikuwa ana mamlaka ya kutoa vibali vya kufanya kazi kwa muda mfupi (CTAs). Hizi ni kazi za ushauri, miradi nk. Uhai wa vibali hivi ni miezi 3 au siku 90.

3. Kutungwa kwa Sheria ya kusimamia mambo ya ajira ya mwaka 2015 na kanuni zake iliyoanza kutumika 15.09. 2015 ilibadilisha baadhi ya vipengele vya sharia ya uhamiaji ya mwaka 1995 na hivyo kumpa mamlaka Kamishna wa kazi kusimamia na kutoa vibali vyote vya ajira.

4. Kwa kuwa kulikuwa na harakaharaka ta kutekeleza sheria na pia kukidhi matakwa ya kisiasa (mambo ya ajira za wageni yalikuwa sehemu ya agenda za Magufuli wakati wa Kampeni) na kutokana na sharia mpya kunyang'anya mamlaka yeyote ya utoaji wa vibali vya ajira kwa Uhamiaji, Kamishna wa Kazi alikuwa na changamoto kubwa ya kusimamia utoaji vibali vya muda (zamani CTA).

5. Sasa ni sharti kila mtu anayekuja nchini kwa kazi ya pungufu kwa miezi 6, aombe - in advance - kibali cha muda mfupi (short term permit) kwa kamishna wa kazi kwa ada ya USD 500.

6. Uhamiaji hawana mamlaka ya kutoa kibali chochote cha kazi, bali sharia hii mpya inawapa majukumu ya kumsaidia Kamishna wa Kazi kufanya Ukaguzi sehemu za kazi na kuhoji, kukagua na kukamata yeyote ambaye hana kibali cha kazi (mamlaka haya wamepewa pia Polisi na Maafisa Kazi).

7. Uhamiaji kulingana na Sheria ya 1995 wanalo jukumu bado kusimamia "ukazi" wa watu. Kwamba ukipata kibali cha ajira cha muda mrefu kutoka Labour (Wizara ya Kazi na Ajira...) kwa ada ya dola 500, 1000 au 0, bado Uhamiaji wana mamlaka ya kutoa kibali cha ukazi (Residence Permit) kwa dola 2050 (labda kama imebadilika).

8. Kwa sasa, ukitoka airport, visa pekee wanayokugongea Uhamiaji ni "tourist".

9. Hata hivyo kutokana na heka heka hizi za mambo ya vibali vya wageni, kuna habari zisizo rasmi kuwa serikali inalegeza masharti na hivyo itarudisha utaratibu wa Business Visa (uliokuwa replaced na CTA) na hivyo kwenye entry points mtu unaingia nazo na kufanyia kazi zisizo na kipato (mkutano, semina, warsha etc).

10. Hadi leo jioni, hayo hapo juu 1-10 ndiyo yaliyokuwa yanafanywa na mamlaka zetu mbili ambazo ziko wizara mbili tofauti ndani serikali moja (Mambo ya ndani na Kazi, Ajira, Sera.....)

Kama una maswali bado tunaweza kusemezana "inbox"


lakini kumbuka,kinacho fanyika tigo huawei project ni ujanja ujanja,unacho ongelea wewe ni by books..
 
Back
Top Bottom