Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,697
- 239,262
Nimekuona ukifanya kazi nzuri kila ulikopita, japo wahusika kwenye ofisi yako hujawagusa, lakini kwa hatua angalau ya kuwarejeshea mali zao waliodhulumiwa si haba
Bali, wako wale waliodhulumiwa maeneo yao na Chama chako cha CCM, hawa wako wengi mno, na wengi walikisaidia tu Chama chako kujenga ile misingi ya Mashina ya Wakereketwa, kwenye maeneo yao, kukubali kwa watu hawa kujengwa kwa mashina ya Wakereketwa imegeuka kuwa laana, ccm ikapora viwanja hivyo vya watu na kujenga ofisi zao na maeneo mengine wakaweka na majengo ya Biashara za kupangisha.
Kwa vile serikali ni ya ccm hakuna mahali popote ambapo Wahanga hawa walienda kulalamika na kusikilizwa, ofisi zote zimewapuuza, Walioenda Mahakamani nao wanapigwa danadana kila siku ili wakate tamaa, Hawana pa kukimbilia wamebaki wakilalamika huku wengine wakifa kwa kisukari kupanda na shinikizo la damu.
Sasa kwa vile wewe ni Waziri na kwa vile umeonyesha uwezo angalau kwa kuwadaka Matapeli wa Ardhi, Akiwemo Alex Msama ambaye ni Tapeli papa namba 3, basi tunaamini hata hili dogo la ccm utaliweza.
Naomba Kuwasilisha