Ni lini serikali itaanzisha masomo ya uchawi mashuleni?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
23,294
55,012
Afríka ínasifika sana kwa uchawi lkn hatujaitumia vema fursa hii. Nadhani sababu kubwa ni kwamba wazungu walituvuruga sana walipokuja Afrika kama wakoloni.

Kuna haja ya kuifufua taaluma yetu asilia ya uchawi kwa kuanzisha Somo la uchawi (witchcraft knowledge) mashuleni.

Halafu A level kuwe na tahasusi (combination) ya Bible Knowledge (Divinity), Islamic Knowledge & Witchcraft Knowledge. Yote haya ni masomo ya dini:- Dini ya Kikristo, Dini ya Kiislam, na Dini ya kipagani kwa mfuatano huo. Nchi nyingi zimeanza kutoa masomo ya uchawi ktk vyuo vikuu ikiwemo Marekani, South Africa, n k.

Kwa kufanya hivyo tutakuwa na wataalamu wengi wa uchawi ambao watatambuliiwa rasmi na serikali na hivyo watalipa kodi na kuongeza pato la taifa. Kama tulivyo na wachungaji, manabii na mashekhe wengi nchini wanaosajiliwa na serikali na hivyo wanatambulika.

Wateja wa uchawi wapo wengi sana barani Afrika na hasa hapa nchini. Takwimu zinabainisha kuwa 26% ya watanzania wanaamini uchawi, 23% ya wanigeria wanaamini uchawi, n.k.

Wabunge wengi sana ni wateja wa wachawi. Prof. Majimarefu (rip), aliwahi kutamka bungeni kuwa zaidi ya nusu ya wabunge wa bunge la 10 walipita mikononi mwake na akawachanja.

Somo la uchawi (witchcraft knowledge) ni fursa iliyosahaulika.
 
Afríka ínasifika sana kwa uchawi lkn hatujaitumia vema fursa hii. Nadhani sababu kubwa ni kwamba wazungu walituvuruga sana walipokuja Afrika kama wakoloni...
Anvyo husudu UCHAWI ndomana Kaandika Mahuleni Mod. wala usibadili acha lisomeke hivyo hivyo hadi akome.
 
I'm neither alcoholic, neither drug addict nor insane. So the smartphone is in the right hands
Kutokuwa mlevi haina uhusiano wa wewe kuwa mzima wa afya ya akili moja kwa moja.

Watu wenye akili tunawatambua kwa
1. Mambo wanayosema
2. Mambo wanayofanya na
3. Mambo wanayosema wanafanya
 
watu wanapambana kuwa maliza wew unawapigia promo waanzishiwe chuo umeshajiuliza zipi athar zake katika jamii maana hauna faida yoyote uchaw na maendeleo ni paka na panya
 
watu wanapambana kuwa maliza wew unawapigia promo waanzishiwe chuo umeshajiuliza zipi athar zake katika jamii maana hauna faida yoyote uchaw na maendeleo ni paka na panya
Hizo nchi zilizoanzisha yafaa tushirikiane nazo ili kujua faida za uchawi zilizowasukuma kuanzisha shahada za uchawi. Sisi waafrika huwa tuko nyuma sana ktk kung'amua fursa
 
Back
Top Bottom