Kama chama chochote cha siasa hakitakusaidia uboreke zaidi katika fikra zako na katika tabia yako, na maono yako kuhusu maisha yako, na utaifa wako, na badala yake kikakufundisha kuwa mbinafsi na mwenye choyo, kisha kuharibu tabia yako njema na kuwa mpiga porojo na mwongo, ambaye unaweza kununuliwa na kuuza utu, na kusaliti nchi yako ni bora ubaki bila chama.
Roho yako ni muhimu kuliko chama chochote cha siasa na kuliko pesa yeyote.
Nenda kwenye chama kitakachokufanya kuwa bora na kwa kiongozi atakaye kuboresha na sio kukupotosha kwenye njia sahihi. Na kukufanya kuwa mwovu.
Kama hakipo baki nyumbani fanya kazi nyingine waache wararuane wenyewe kwa wenyewe.
Kama chama hakiko for the best interest of the people usijiunge. Kama hakikufanyi uwe na tabia bora usijiunge. Nenda kwenye chama na kwa kiongozi atakayekusaidia kufikiri sawa sawa na kutenda vyema. Kiongozi ambaye atakusaidia ku improve your behaviour ndio kiongozi.
Nchi haiwezi kuendelea pasipo kuwa na watu bora ambao wamechekechwa na kuchujwa na kuchaguliwa kuwa viongozi wa watu.
Chama chochote ambacho kinafanya ukuaji wako wa kifikra udumae kutokana na maamuzi ya kijinga ya viongozi wake usikae.