Neema Mrindoko atakiwa ajieleze kiwanja cha TBC kuwa na jina lake

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534

Naibu waziri wa Wizara ya Habari, Anastazia Wambura, ametoa siku saba kwa Menwja Rasilimaliwatu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Neema Mrindoko kujieleza ni kwanini ameandika jina lake katika kiwanja kilichopo Kisarawe mkoani Pwani.

Wambura alisema hayo jana akionesha kukasirishwa na kitendo hicho alipotembelea kiwanja hicho kilichopo eneo la Kimani ambacho mpaka sasa hakijakamilisha usajili wake na kupewa hati wakati kilinunuliwa na Shirika hilo mwaka 2012.

Kiwanja hicho kilichojaa nyasi nyingi kuonesha kilishatelekezwa, kimejengwa nyumba za watumishi ambao wangekuwa wakifanya kazi katika kituo cha Kisarawe lakini hazijakamilika.

"Natoa siku saba mtu huyu awe anipa Maelezo ya kutosha kwanini hati hiyo imesainiwa na mtu mmoja ambaye ni yeye na ameandika jina lake badala ya jina la Shirika, inamaana alikua hajui? Hii ni makusudi," alisema Wambura.

Wambura alisema mtu huyo amefanya makusudi kwa nafasi yake kushindwa kutambua kukaa miaka yote hiyo bila kupewa hati na kutelekezwa bila kuendelezwa ni ufisadi ambao hauwezi kuvumiliwa.

Awali Wambura alipokuwa akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Mwanamvua Mrindoko, alisema kiwanja hicho chenye mita za mraba 9,567 kilipimwa na kusajiliwa kwa namba 68480 mwaka huo huo TBC iliomba kuandaliwa hati.

Mrindoko alisema utaratibu za ukamilishaji hati zilifanyika na walilipia na kujaza fomu ya maombi ya hati hata hivyo baada ya TBC kuisaini na kuirudisha Ardhi ilionekana kuwa na mapungufu ikarudishwa TBC.

Aliyataja mapungufu hayo kuwa ni hakukua na nalala halisi ya kuanzishwa shirika na pia fomu hiyo ilisainiwa na mtu mmoja badala ya wahusika wawili wa Shirika hilo na hivyo kukwamisha mchakato wa kupata hati.

Naibu Waziri huyo alipomuhoji Afisa miradi wa Wizara hiyo, Macksselin Chota ambaye alikuepo hapo, alisema Maelezo hayo ni sahihi kwamba mapungufu hayo wanayafanyia kazi.

Chota alisema viwanja vingi vya TBC havijapata hati ambapo kati ya viwanja 55 ni 19 pekee ndivyo vyenye hati na pia viwanja vingi viko katika migogoro mbalimbali kama vile uvamizi na pia uporaji.

Naibu Waziri Wambura aliagiza ndani ya siku hizo saba hati ya kiwanja hicho cha Kisarawe Iwe imepatikana, na pia TBC itoe Maelezo ni namna gani watafanya kuendelea majengo ambayo yameanza kujengwa hapo.

"Hii inatia mashaka kabisa, mnachelewesha kupata hati na baadae viwanja vinaingia kwenye migogoro, unafanya hivyo ili baadae nyie wenyewe mzunguke, tutashindwaje kuamini hivyo?" Alihoji Naibu Waziri.

Naibu Waziri huyo aliagiza TBC kuangalia namna ya kuanzia kuendeleza viwanja vya Shirika hilo kwa ubia ili kulipatia Shirika mapato na pia nyumba za watumishi wake.

Chanzo: Habari Leo
 
... Neema Mrindoko ni Meneja Rasilimaliwatu TBC; anatuhumiwa kiwanja cha TBC kilichoko Kisarawe kusajiliwa kwa jina lake ...

... Mwanamvua Mrindoko; ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kisarawe

Sometimes mambo mengine "yashinda fahamu zetu" kuyaelewa - twahitaji usaidizi wake Muumba.
 

Kutoka kwa Vijazi hadi kwa Mirindoko (LOL).
 
Mpaka dakika hii ninapotuma posti hii sijasikia ukawa hata mmoja aliyetumbuliwa kwa ufisadi, rushwa au kukwepa kodi hii maana yake ni kwamba wezi ni ccm, haihitaji utafiti kujua hili
Usikate tamaa kusubiri
 
Na hiyo ndo sababu watumishi wengi wa serikali hasa ngazi za juu wana kadi za ccm ili kulinda maslahi yao ila kwa sasa wataisoma namba
 
Unganisha dots .......
 
Mpaka dakika hii ninapotuma posti hii sijasikia ukawa hata mmoja aliyetumbuliwa kwa ufisadi, rushwa au kukwepa kodi hii maana yake ni kwamba wezi ni ccm, haihitaji utafiti kujua hili

Subiri haya mambo yanaweza kutushangaza. Ukawa sio malaika lakini pia wananafasi chache za kupiga. Kuna wengine by association au wanaukawa kamili watanasa-issue je wakinaswa ukawa itawalinda style ya CCM au itawachukulia hatua gani? Kwa kiasi kikubwa CCM imewalinda hadi amekuja JPM, nae watu wanawasiwasi kama atayaweza hayo majipu kongwe.
 


Nakuabaliana na uchambuzi wako
 

Unataka kunieleza kuna mahusiano kwa vile wanafanana majina ya ukoo, je wanahusishwaje mmoja mmoja na hiii kashfa mungu anatuona kweli hakyamungu bee ne ndisogwe kuboma beee, ne ndimgaya sida nene loo
 
khaaa hii kali yaani kiwanja cha ITV kiwe na jina la Joyce Mhavile loh patachimbika..
 
Nakumbuka huko nyuma aliwahi kweli katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini anaitwa Mrindoko je ni ndugu?
 
Uyu angeenda na mama Kilango leo leo anataka jifanya JMT kwa kujimilikisha kiwanja
 
Jamani kwa nini mnamuacha fisadi kuu lowasa liko nje linakula tu chakula

Hili fisadi lowasa lipelekwe gerezani mara moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…