Ndalichako na sera mbovu za elimu

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Wizara ya Elimu ilitoa tamko kuwa wanafunzi wote wasome sayansi, mpaka hapo walimu wa masomo ya Sanaa na biashara hawana soko tunasomesha wasomi baadae tunawatelekeza sisi wenyewe, kwa miaka ya baadae kutakuja tokea ukosefu wa walimu masomo ya Sanaa na biashara kama ilivyosasa hamna walimu wa kutosha wa masomo ya sayansi.

Je serikali inaweza jenga viwanda vya kuwaajiri wanafunzi walioshinikizwa wasome sayansi? Sayansi inayofundishwa ni ya viwanda au ndio hii ordinary science? Kwa nini serikali isirudishe TECHNICAL SCHOOLS? Ndio ziwe zinafundisha industrial science (elimu ya viwanda). Hawa walimu wa biashara na sanaa walio mtaani, walioajiriwa na walio vyuoni tunawapeleka wapi? Serikali inaanda wasomi halafu inakuja kuwatelekeza

Bado serikali inasomesha wakandarasi halafu bado tenda watapewa wengine, sawa sisi wakandarasi wazawa hatuna uzoefu juu kazi Fulani na miradi mipya nchini. Serikali inatutengenezea mazingira gani ili sisi tujifunze? Nilitarajia kwenye mikataba iwe inaorodhesha kuwa wakandarasi wa nje wawe wanashirikiana na wakandarasi wazawa iwe, iwe ni sheria kwenye mikataba ili sisi wakandarasi wa ndani tuweze pata maarifa juu ya teknolojia na ufanyaji kazi wa miradi iliyo migeni hapa nchini kama fly over Dar n.k

Wizara ya elimu inabidi ibadili mifumo ya elimu hapa nchini ili sera ya viwanda iweze tekelezwa kwa uhakika, swala la kunyima mikopo kwa wanafunzi wa vyuo waliotoka diploma ni ujinga wa hali ya juu. Kwa nchi yetu ni lazima tutoe kipaumbele kwenye mikopo kwa masomo ya sayansi ili tutoe motisha na kwa kutilia maanani fani za sayansi ni gharama sana kwa familia duni za kitanzania haziwezi mudu gharama hizo.

Wizara ya elimu pia yapaswa kuandaa mtahara mmoja wa nchi nzima, sio ukienda shule za wahindi wanakuwa na mitahala yao, mbona sisi tukienda tunasoma mitahala yao? kama yetu ina mapungufu basi tushirikiane kutunga mitahala mipya inayoendana na kizazi na mahitaji ya karne ya 21.
 
We kama umesoma na huna vision na ulichokisoma njoo ulime selikari hataajili watu wrote kajifunze Nigeria watu wana PhD wapo wanauza mitumba tafuta fulsa jamaaa acha kulalama mtafute HASAN ngoma au Niki WA 2
 
Mkuu nimekuelewa sana. Sema hii ni nchi ya pekee duniani ambayo inaendeshwa kwa matamko yasiyo na tija. Shule zote kama ifunda tech, mbeya tech nk sijui kwa sasa kama hata vile vifaa vipo usikute viliuzwa screpa. Nilisoma ifunda tech for 2 yrs ila baridi liliniumiza nikahama ila niwe mkweli ile shule ilikuwa inafundisha hakika na walau nami ujuzi flani ninao kama matunda ya ile shule.

Serikali irudi na ijiuzilize nchi ya viwanda itapatikana kwa shule za kata ambazo wamekosa hata kuwekea milango watoto wanapita madirishani? Walimu wao wengi theory ndo wamebobea na sio practical kwa vile walisoma bila vitendo.

Tujiulize....... Kibonzo tym
 
Ngoja walimu wa sekondari wakafundishe primary ili tuone miujiza mingine ya dunia
 
Bashite age mkuu usitumie nguvu nyingi
 
Bashite age mkuu usitumie nguvu nyingi
Waziri wa elimu hana mpango na utafutaji wa mbinu mpya katika elimu yetu. Kwani nani kasema nchi ikiwa ya viwanda haihitaji watu wa arts? Kila baada ya miaka 10 kila kitu huwa kinaanza upya nchi hii, sijui twaenda mbele au tunarudi nyuma haieleweki.
 
serikali hii haishauriki wala haipangiwi cha kufanya.. inajua nani aajiriwe na nani asiajiriwe... tena mkishauri ndo mnaharibu kabisa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…