Ndalichako kila mwaka utafukuza TIE, suluhisho ni hili.....

mumburya

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
321
448
Tumesoma leo kuwa Waziri amewasimamisha Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi wa TIE kutokana na ubovu wa vitabu. Anaweza kudhani hilo ni suluhisho. Si suluhisho hata kidogo kwa sababu:

1. Hii si mara ya kwanza madudu ya TIE kuonekana. Mwaka jana yalionekana kwa mara ya
kwanza ndipo wakaletwa hawa makaimu.

2. TIE hawana mshindani, na ukikosa mshindani huwezi zingatia ubora.

3. Duniani kote hakuna nchi ambayo serikali ina publish vitabu vya shuleni ( soma tena - hakuna)
kazi hiyo imeachwa kwa sekta binafsi ambayo inawabobezi katika fani hiyo, Serikali hubakia kama mdhibiti tu.

4. llipovunjwa EMAC watu hawakujua kuwa waliokuwa wanaumda EMAC walikuwa TIE na wenzao wa taasisi zingine, yaani members wa EMAC, walitoka TIE, BAKITA na UDSM, hivyo utaona EMAC ilishiba zaidi. Tatizo la EMAC ilikuwa kutanguliza rushwa.

5. Tatizo litaisha kama sekta binafsi itaingia na kushindanishwa na kupata kitau teule kimoja.
sidhani mtu anayeshindana ataandika Dodoma is the big city of Tanzania. TIE ibaki kama
regulator.

6. Uandishi ni hobby na kipaji, ndiyo maana hata yeye Profesa Joyce, hakugundua hayo makosa
hadi vitabu vina enda printing. (sidhani kama waziri hakuomba kuona copy ya kitabu kinacho
printiwa kwa Tsh. bil. 8 na kujiridhisha, kama ndivyo basi ni mzembe). Pia kwa mujibu wa
sheria Waziri ndiyo anayetoa ithibati baada ya kujiridhisha. Wakati anabebesha wenzake
mislaba na yeye abebe wa kwake.

7. Baada ya mwaka mmoja, huu uzi utarudi kuthibitisha haya, kwamba makosa yataendelea chini
ya hiyo TIE mpya mtakayoiunda. Tusubiri.
 
Hakika umenena kilicho cha kweli Mumburya. Huo ndio mwarobaini. Serikali isimamie ubora wa vitabu lakini sio wawe waandishi halafu wao wenyewe hawana mtu wa kuwakagua. Ni kudanganyana tu.
 
Wabunge walitakiwa wakomae profesa aondoke. Yaani Profesa mzima unashindwa kupitia vitabu kwa sababu una waamini TIE!!!!!!!
 
Good
 
Wabunge walitakiwa wakomae profesa aondoke. Yaani Profesa mzima unashindwa kupitia vitabu kwa sababu una waamini TIE!!!!!!!
Utamaduni huu sio wa nchi zisizoendelea.
Kwa ustaarabu kabisa ilatakiwa jina la huyu madamu liungane na hawa akina meck sadiki (honestly), majaji wawili (honestly) ila kwa yeye ingeandikwa Mrs. Ndalichaku (dishonestly)
 
Elimu ya nchi yangu bado inasafari ndefu sana-lakini tatizo moja ni nguvu za Raisi na Waziri ukilinganisha na vyombo vya utekelezeji (TIE, NECTA, NACTE, TCU etc). Raisi au waziri analotaka basi huwa bila majadiliano. Jana udahili kupitia CAS, leo direct chuoni ni mfano tu. Management zimejengwa kuwa na woga, wao wanatanguliza au wanalazimishwa kufurahisha hao wakuu wao. Tuna mfumo mbaya. Nitaandikaje kitabu halafu nitathmini kitabu hicho hicho (mgongano wa maslahi) na ikubalike?. Mabodi ya taasisi hizi inaelekea mengi yameshikwa na management ( hivyo hayaoni madudu ya wazi).
 
elimu yetu aliyeanza kuiua ni mkapa aliyekuja kuichimbia kaburi na kuizika ni kikwete,ndalichako naona anajitahidi kuifufua
 
elimu yetu aliyeanza kuiua ni mkapa aliyekuja kuichimbia kaburi na kuizika ni kikwete,ndalichako naona anajitahidi kuifufua

Hivi vitabu feki vimetoka mwaka huu dada, hivi si vya zama za Mkapa au Kikwete. Usimtetee Ndali.
 
5. Tatizo litaisha kama sekta binafsi itaingia na kushindanishwa na kupata kitau teule kimoja.
sidhani mtu anayeshindana ataandika Dodoma is the big city of Tanzania. TIE ibaki kama
regulator.


Kama wametoa vitabu bomu wataweza ku regulate?
Na kama watabaki kuwa regulators, huoni kuna chances za kuendekeza rushwa na ku favor watakaotoa dau kubwa

Mimi nadhani TIE inatakiwa kusukwa upya kwa kuwa na mchanganyiko wa watu wabobezi toka vyuo vikuu, wasioendekeza maslahi yao binafsi, ikiwezekana hata kuwashirikisha wakuu wa vyuo vya ualimu wastaafu waliofanya kazi nzuri huko nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…