Nchi Nzima Hakuna Mvua, Serikali Ina Mkakati Gani na Tatizo La njaa?

Hapo umesema Ukweli ndugu yangu. Naomba Serikali ichukue Tahadhari kabisaa kabla mambo hayajawa Makubwa. Maana ukweli usiopingika Mvua mwaka huu ni haba sana. Nafikiri Serikali itaangalia kwa upana wake huu Uzi wako. Hongera sana ndugu yetu kwa kuliona hili. Naomba UKAWA na CCM tushirikiane kwa pamoja ili kuona ni vipi tunaweza kuwaokoa wananchi wetu katika baa la njaa. Tofauti zetu tuweke kando na Serikali itenge Fedha kwaajili ya dharula.
 
Huu ndio ujinga unaolikabili taifa. Suala la ukame mtu unaleta siasa, unadhani njaa ikiikabili nchi kuna uchama hapo? Au unadhani kuwa ukivaa shati la kijani utapewa mgawo wa mahindi?
Njaa ikitokea ni janga la kitaifa na nchi kupitia serikali ndio inaratibu upatikanaji wa chakula toka nje au kutoka eneo moja hadi jingine. Unadhani wale wajomba zako kule kijijini wanaweza kujiagizia chakula toka Zambia? Kama sio serikali kuratibu mpango wa chakula kutoka sehemu nyingine?
Ni kweli kuwa kuna maeneo mvua zinanyesha, lakini sio yale yenye uzalishaji mkubwa wa chakula na kuwa tegemeo kwa taifa hivyo kuchukulia jambo hili kwa utani ni ujinga wa kitoto kabisa. Yapo mataifa makubwa na tajiri yaliyumba kwa ukosefu wa chakula sembuse sisi hohehahe? Serikali ikiendekeza siasa katika swala hili itaondolewa madarakani kabla hata ya wakati wake na tena hao hao wana ccm ndio watakuwa wa kwanza kutaka iondoke kwa hiari au nguvu
Dhambi za CCM kumtumia Lipumba kudhoofisha ukawa ndiyo inaleta Ukame,Mungu hapendi Taibia za umamluki,unafiki na kula pesa za Umma kwa kazi ya kudhoofisha upinzani,
 
Dhambi za CCM ndizo zimezuia mvua
Hebu tuache hizo sababu tunazo dhani zimeleta ukame bali tujikite na swali jee serikali imewaandaaje wananchi kukabiliana na viashiria hivi vya njaa?
Tusifikiri sana kwa maisha ya mjini ambayo watu watapata tuu vyakula madukani, supermarket nk bali tuwafikirie zaidi mamilioni ya wananchi vijijini ambao wanategemea chakula kutoka mashambani
 
Mkuu ni vigumu kwa mda huu kufikiria Ukame kwa sababu Akili zote zipo kwenye ununuzi wa ndege na ujenzi wa uwanja wa ndege chato.
 
Jamani hali ya mvua ni tata nchi nzima kwa hiyo ni ishara kuwa lazima njaa itakuwa kali nchini mwaka ujao. Lakini mbona serikali haionyeshi kuwa inao mpango mkakati wa kukabiliana na baa hilo linalo tunyemelea?
Au bado tunasubiri mpaka hali itakapo kuwa mbaya ndio tuanze kukimbizana kutafuta utatuzi? Mipango ya zima moto itaisha lini nchi hii hasa katika maswala ya hatari kama hayo?
Hujasikia ujumbe wa kulima mazao ya muda mfupi na yanayostahili ukame?
 
Hujasikia ujumbe wa kulima mazao ya muda mfupi na yanayostahili ukame?
Mkuu tusi generalise mambo namna hiyo, elimu ya wakulima wengi wanaolisha nchi hii ni ya chini hivyo bila msisitizo wa serikali ( na serikali ni kuanzia serikali kuu hadi za vijiji) hakuna kitakachofanyika na njaa haina mchezo, inaweza kusambaratisha familia hadi taifa
 
Kila mfalme anapotawala nchi anakuja na yake.
Mungu akiamua kuonyesha uovu flani analeta njaa,mafuriko ama mahonjwa,mwenye akili kishaelewa
 
Jamani hali ya mvua ni tata nchi nzima kwa hiyo ni ishara kuwa lazima njaa itakuwa kali nchini mwaka ujao. Lakini mbona serikali haionyeshi kuwa inao mpango mkakati wa kukabiliana na baa hilo linalo tunyemelea?
Au bado tunasubiri mpaka hali itakapo kuwa mbaya ndio tuanze kukimbizana kutafuta utatuzi? Mipango ya zima moto itaisha lini nchi hii hasa katika maswala ya hatari kama hayo?

wanasafisha nchi zilikuwa mvua za deals hahahahahhahahahahahah
 
Mvua hakuna nchi nzima mkakati wamuombe lowasa alete ya kutengeneza kama alivoahidi wakati wake itatuondolea ukame
 
Jamani hali ya mvua ni tata nchi nzima kwa hiyo ni ishara kuwa lazima njaa itakuwa kali nchini mwaka ujao. Lakini mbona serikali haionyeshi kuwa inao mpango mkakati wa kukabiliana na baa hilo linalo tunyemelea?
Au bado tunasubiri mpaka hali itakapo kuwa mbaya ndio tuanze kukimbizana kutafuta utatuzi? Mipango ya zima moto itaisha lini nchi hii hasa katika maswala ya hatari kama hayo?
Duh. ..naona MOLA Mwenyewe kaamua kukujibu kwa mvua nyingi iliyonyesha Dar es Salaam. ...
 
Back
Top Bottom