Nawakumbusha viongozi wote wa ngazi za juu Serikalini na kwenye Vyama vya siasa. Urais hautafutwi bali urais ndio unakutafuta. Haki itamalaki kote

Capitrait

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
228
328
Kwenye Taifa hili mimi ni mtu mdogo sana, sina mamlaka yeyote yale. Hata kwenye familia yangu sina nguvu yeyote ya ushawishi, naonekana wa kawaida sana sina maajabu yeyote.

Lakini leo hapa nazungumza kitu kimoja kwa viongozi wa juu wa serikali na Vyama vya siasa kwa nguvu na mamlaka makubwa ya andiko hili Takatifu la Bwana bila kujali udogo wala udhaifu wangu maana ndani ya rehema zake naokolewa:

Luka 10
27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

Mathayo 22
37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.

39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Marko 12
30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

32 Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;

33 na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia.

Hakuna yeyote mwenye mamlaka ya kutafuta urais wa Taifa lolote la Mungu, bali urais ndio unakutafuta wenyewe kwa makusudi ya Mwenyenzi Mungu mwenyewe.

Kila mmoja kwenye Taifa hili la Mungu ahakikishe haki inatamalaki kwenye mamlaka yake husika kwa ajili ya utukufu wa Mungu; maana muda na saa chungu yaja tena si mbali ambapo udhaniaye ndiye kumbe siye na udhaniaye siye kumbe ndiye.

Taifa la Mungu linaokolewa. Amen.
 
Back
Top Bottom