Hahahahah, hiko kimashine ni balaa kwa msiokijua. Kwa kutoana ushamba kidogo hio reciever kwa kifupi tu, ni muundo flani wa amplifaya ambao umebuniwa kufanya kazi kama Digital Audio/Video Control Centre. Yani inapokea mawimbi ya sauti na picha toka katika vifaa vingine vya burudani kama tv, simu, radio, game ama deki na kuyachuja ili kutoa sauti au katika vipimo sahihi na kwa mikondo tofauti yani channels, kama ambavyo ilivyokusudiwa katika audio au video contents tofauti.
Ili kuitumia lazma uwe na source ya sauti au picha na pia itabidi uwe na speakers kwa ajili ya output ya sauti.
Uzuri mmoja ni kuwa hizi za kisasa zinakuja na inbuilt radio hivyo unaweza itumia kama radio ya kawaida.
Kwa ufanisi sijawahi ona kitu kinachofanya sound itoke kwa clarity bila distortion kama hizi reciever. Hamna cha hometheatre wala subwoofer inayofikia mziki wa reciever!
Saju b
Baba yenu